Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,605
- 1,704
Tuliwalaumu sana. Tuliwasema sana. Tuliwakejeli sana.
Tukasema wana kasumba. Tukadai hawakumbuki wanakotoka. Tukasisitiza ni vibaraka.
Lakini leo wanafanya mambo makubwa huko Ulaya na Marikani. Leo hii wanatumika kuleta maendeleo ya Wazungu. Licha ya mafanikio yao yote huko bado huku Afrika hali ni mbaya sana mpaka imebidi tutunge maneno mapya - kama vile Kufulia - ili kuelezea jinsi sisi watu ambao Frantz Fanon alituita 'Les damnes de la Terre', yaani, 'The Wretched of the Earth' au 'Viumbe Waliolaanika Ulimwenguni', tulivyopigika kama hii picha hapo inavyodhihirisha.
Je, wakati sasa umefika kukubali hawa Wazungu Weusi watutawale ile tuondokane na ile laana ya Nyani Ngabu ya 'Miafrika Ndivyo Tulivyo'? Je, saa ya wokovu wa Mwafrika imefika kupitia Masihi ambaye ni 'Black Skin White Mask', kama alivyokejeliwa na Frantz Fanon? Je, wakati ni huu wa kuirejea hali inayokejeliwa kizalendo hapo chini na Nabii wetu aliyeshindwa kutufikisha kwenye Nchi ya Ahadi ya 'Egalite' yenye asali na maziwa kwa ajili ya watu wote?
"Some of us, particularly those of us who acquired a European type of education, set ourselves out to prove to our colonial rulers that we had become ‘civilized'; and by that we meant that we had abandoned everything connected with our own past and learnt to imitate only Europeans ways. Our young men's ambition was not to become well educated Africans, but to become Black Europeans! Indeed, at one time it was a complement rather than an insult to call a man who imitated the Europeans a ‘Black European'" - Julius Kambarage a.k.a ex- Black European Julius Cambridge

Last edited: