Mzungu kacharuka kuombwa michango huko ubalozini

very true watanzania wanaboa sana eti unapangiwa kiasi kabisa Nina madeni kibao na issue zangu nyingi kweli nitakupa nikijisikia na simu sipokei buget 20m eti muisika Ana 3m? kwaiyo 17m zitoke kwa watu real
 
Ukweli mtupu Waswahili tubadirike.

..............Nitarudi baadae kuendeleza hapo alipoishia mzungu ........lakini kwa Kiswahili.
Utakuwa umefanya la maana kwani wengine tumesoma shule za TAPA aka WAZAZI na ukichanganya sina hela ndio kabisa hakipandi (angalau ningekuwa na glass ya wine)
 
Kanikumbusha mzungu fulani alipinga tusimchangie pesa ya fungate, akasema la sivyo sote tutajumuika kwenye hicho chumba.
 
Kuna baadhi ya watu hawana hata mshipa Wa aibu. Unakuta labda kutokana na sababu mbali mbali MTU hamjawasiliana miaka kibao iwe ndugu ama rafiki. Akiaanza vikao vya kuoa ama kuolewa anakutafuta ili akupe kadi ya mchango Wa harusi...inakera na kuudhi mno.
Yeye kwenye kuoa ama kuolewa kajipanga, sasa anakulazimisha na wewe ushiriki kwenye mipango yake pasipo hata kujali mipango yako. Ukihoji wanasema oooh wewe mchoyo na mbinafsi hutaki ushirikiano. Hivi huu ushirikiano UPO kwenye Harusi, sendoff ,kipaimara na birthday tuuu????, mbona kwenye elimu na matibabu hatushirikishani???.

Ifike mahali tubadirike, udugu au urafiki usiwe kwenye hiyo michango chango yenu. Usipochangia eti MTU anakununia kabisa tena wakati mwingine ya mtu ambaye hata haumfahamu ..aghraaaah......
 
Yeah, this is pure madness...
Sasa hapo umkute Lufufu anatafsiri hii lugha!
Mungu amrehemu.
 
Inauma sana! Kuna jamaa eti amejenga nyumba ya wastani na ni nzuri sasa anataka kuhamia na amePrint card za mchango wa kufanya sherehe ya kuhamia!

Kwanza, nampongeza kwa kujenga .

Nyumba ni yake, atakayeishi ni yeye, aliyeamua na kupanga hiyo part ni yeye, Ila gharama ya hiyo part mchangie.....sijui watu wengine wakati mwingine huwa wanawaza nini?????
Kama pesa ya kufanya party hana si ahamie kimya kimya???....muhimu ilikuwa ujenzi hiyo party ni mbwembwe tu. Au kuna watu anataka awalike aje awarushe roho kwa kujenga Nyumba???!!!!!.
 
Mimi nimeshaacha kuchangia huu ujinga siku hizi, harusi yangu sikuomba mchango kwa mtu nilifanya kile nilichoweza..
 
Back
Top Bottom