Mzungu aponzwa na mkia wa tembo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Raia wa Afrika kusini Rudolf Van Niekerk miaka tano jela au faini ya Sh 65.8 milioni kwa kosa la kusafirisha nyara za serikali, anaandika Faki Sosi.

Akisoma mashtaka hayo Paul Kadushi, Wakili wa Serikali mbele ya Huruma Shahidi Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amedai kuwa mtuhumiwa alikamatwa na nyara hizo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere tarehe 17 Juni mwaka huu.

Kadushi amedai kuwa nyara hizo ni bangili iliyotengenezwa na mkia wa tembo yenye thamani ya Sh.32 milioni bila ya kibari.

Hata hivyo Niekerk Mtuhumiwa Raia wa Afrika Kusini ambaye asili yake ni mzungu amekiri mashtaka hayo.

Shahidi, ambaye ni Hakimu aliyetoa hukumu hiyo awali amesikiliza upande wa mtetezi Gerrad Nangi, wakili wa mtuhumiwa ambapo amedai Mteja wake ni mgeni Tanzania na hajui sheria za nchi.

Aidha Nangi amedai mteja wake ni mgonjwa na anafamilia pia nimsaada mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwani yeye ni fundi mitambo katika kiwanda cha sukari cha kilombero.
 
Mbona utetezi wake haueleweki?

Anasema yeye ni mgeni hapo hapo yeye ni fundi wa kilombero??

Halafu kisheria kuna msemo kuwa kutokujua sheria sio utetezi??
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Raia wa Afrika kusini Rudolf Van Niekerk miaka tano jela au faini ya Sh 65.8 milioni kwa kosa la kusafirisha nyara za serikali, anaandika Faki Sosi.

Akisoma mashtaka hayo Paul Kadushi, Wakili wa Serikali mbele ya Huruma Shahidi Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amedai kuwa mtuhumiwa alikamatwa na nyara hizo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere tarehe 17 Juni mwaka huu.

Kadushi amedai kuwa nyara hizo ni bangili iliyotengenezwa na mkia wa tembo yenye thamani ya Sh.32 milioni bila ya kibari.

Hata hivyo Niekerk Mtuhumiwa Raia wa Afrika Kusini ambaye asili yake ni mzungu amekiri mashtaka hayo.

Shahidi, ambaye ni Hakimu aliyetoa hukumu hiyo awali amesikiliza upande wa mtetezi Gerrad Nangi, wakili wa mtuhumiwa ambapo amedai Mteja wake ni mgeni Tanzania na hajui sheria za nchi.

Aidha Nangi amedai mteja wake ni mgonjwa na anafamilia pia nimsaada mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwani yeye ni fundi mitambo katika kiwanda cha sukari cha kilombero.
Rudia tena hapo;bangili iliotengenezwa kwa mkia wa tembo yenye thamani ya shs 32 milioni? huu ni uongo uliopitiliza,au ni pesa ya Zimbabwe 32 milioni?
 
Back
Top Bottom