Mzungu ang'ata sikio la mhamiaji mjini Glasgow nchini Scotland wakisubiri chips na kuku KFC. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzungu ang'ata sikio la mhamiaji mjini Glasgow nchini Scotland wakisubiri chips na kuku KFC.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Richard, Feb 5, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mtu mmoja ambae inasemwa kuwa ana asili ya kigeni ameng'atwa sikio na kijana wa kizungu wakti wakisubiri chips na kuku ndani ya mgahawa maarufu uitwao KFC uliopo kwenye mtaa wa Renfield mjini Glasgow nchini Scotland.

  Mtu huyo ambae inasemwa ana miaka 28 alikuwa akisubiri order yake na ndipo kijana huyo wa kizungu alipoingia mgahawani humo akiongozana na kijana mwenzie na msichana.Walipoingia kama kawaida wakaona kuna mtu wa kumchokoza na wakamwona mtu huyo kuwa ndio waanzishe zogo nae.

  Mtu wa watu alipoona kwamba hawezi mambo ya zogo ikabidi atoke aende zake bila kuchukua chips na kuku ambazo alikwishaagiza.Kijana huyo wa kizungu alipoona hivyo aliamua kumfuata mtu huyo na kumshambulia na hatimae kufanikiwa kung'ata sikio lake karibu lote na kumsababishia jeraha kubwa mtu huyo.

  Mtu huyo bado yupo hospitalini iitwayo Glasgow Royal Infirmary ambapo amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji.

  [​IMG]

  Tukio hilo limetokea hapa.

  Polisi wa kutoka kituo kikuu cha polisi cha Strathclyde wanafanya uchunguzi wao.Haya mambo ya chuki sijui yataisha lini.
   
Loading...