Mzungu anawaambia wahamiaji wa kiafrika msije Uingereza "Don't come to England"

Neter

JF-Expert Member
Dec 30, 2011
698
1,115
British man tells African migrants to "Don't come to England"

Katika video hapo chini mzungu anawaambia wahamiaji wa kiafrika kuwa wasiende Uingereza kwa kuwa wana wahamijai wa kutosha na watu wao ambao inabidi wawatumikie
 
Sawasawa kabisa, tutengeneze nchi zetu ziwe zaidi ya zao kusudi nao wakija huku tuwambie hivyo hivyo.

Tatizo letu tunajua kutamba tu kuwa bara letu ni tajiri lkn tumeshindwa kufanya maisha yetu yawe bora na matokeo yake ndio hayo ya kila moja kutaka kuzamia Ulaya. This is very silly indeed.
 
Waafrika tumekuwa kama Vimbulu kama vile hatuna makazi
 
Ndio, historia inaonyesha bara la Afrika lina "mchango mkubwa" katika maendeleo ya Bara la Ulaya na Bara la Marekani ya Kaskazini kwa karne kadhaa sasa.
Hizo hadithi ama historia zimeshapitwa na wakati. Kama baba yako alisaidia mtu halafu akaja kua tajiri haikupi wewe uhalali wa kwenda kudowea au kung'ang'ania vitu vyake eti kisa baba yako alimsaidia. Hayo yameshapitwa na wakati.

Waafrika tunashindwa nini leo kutengeneza mataifa yetu na kukimbilia mataifa ya wengine, kipindi wanayajenga tulikuwepo? Kama tunataka maisha mazuri na mazingira mazuri ya kuishi tuyatengeneze hapa kwetu.
 
Ndio, historia inaonyesha bara la Afrika lina "mchango mkubwa" katika maendeleo ya Bara la Ulaya na Bara la Marekani ya Kaskazini kwa karne kadhaa sasa.
Tokea ukoloni umeondoka Afrika ni muda mrefu ambao kama tungekuwa serious tungekuwa tumeshaendelea sana, tatizo la Waafrika ni ubinafsi, ukabila, chuki, fitina, wivu na roho mbaya wenyewe kwa wenyewe.
 
Fursa zikiwa nyingi Africa itapunguza hizi aibu. Fursa huambatana na uwezeshaji wa kuzipigania, usimwambie MTU akalime ilihali hakuna vitendea kazi, anategemea mvua, hana nguvu kazi n.k
 
Ndio, historia inaonyesha bara la Afrika lina "mchango mkubwa" katika maendeleo ya Bara la Ulaya na Bara la Marekani ya Kaskazini kwa karne kadhaa sasa.
Sio kweli ni uongo uliopitiliza afrika tatizo in siasa ambazo ndio zenye kujenga mhimili imara wa uchumi, sababu ya upuuzi wa kisiasa ndio maana tuna taasisi mbovu nyingi mno ambazo hazina misingi imara ya kuchochea maendeleo imara, imagine mataifa mengi ya kiafrika yana Uhuru ulio balehe vya kutosha lakini bado misingi ya kisiasa ni mibovu mno ndio maana rushwa imetamalaki, haki hakuna,uonevu,chuki,hofu,ujivuni na ukandamizaji umejaa, kwa hali hii mpaka mwisho wa dunia "we shall be inferior forever" pasipo na haki maendeleo hakuna mkuu.
 
Tokea ukoloni umeondoka Afrika ni muda mrefu ambao kama tungekuwa serious tungekuwa tumeshaendelea sana, tatizo la Waafrika ni ubinafsi, ukabila, chuki, fitina, wivu na roho mbaya wenyewe kwa wenyewe.
Ishu ni hao hao wakoloni bado wanaikoloni Africa, wewe onesha kujitutumua uone watakachofanya, ref, Libya,
Ukoloni mamboleo bado upo na viongozi wa Africa bado hawana power ya kujitoa wanaamua tu na wenyewe wavune kwa ajili yao basi.

Kikubwa ni sisi kwenda huko huko, kutumia hivyo hivyo vya kwetu na vyao, msiogope. Lol.
 
Tatizo la Waafrika wengi hawafahamu kwamba vita kubwa sana inaendelea kati ya mtu mweusi na mweupe. Haitaisha leo wala kesho. Cha kushangaza makuwadi kama toto Tundu Lisu na vibaraka wao wanaangalia matumbo yao tu.
Kwani huyu lisu yeye ndio anasaini mikataba ya mikopo au ya uwekezaji, tuache kujitoa akili tena acha upuuzi, afrika tatizo mifumo mibovu, sisi watu weusi sijui tunakwama wapi, matatizo yetu tunawapa wenye mrengo mbadala, ebu kuwa serious mkuu, hili taifa lina miaka 50+ sasa ya Uhuru, hao wenye mrengo mbadala wana impact gani so far?!
Nani anakaribisha mikataba ya kinyonyaji,nani anaita wawekezaji, nani anaunda taasisi za serikali?
Mbona wengi wetu tuna akili finyu hivi?!
Mkuu jitahidi peleka watoto shule.
 
Tokea ukoloni umeondoka Afrika ni muda mrefu ambao kama tungekuwa serious tungekuwa tumeshaendelea sana, tatizo la Waafrika ni ubinafsi, ukabila, chuki, fitina, wivu na roho mbaya wenyewe kwa wenyewe.
Hands up bro, you're right, wala tusiende mbali wewe anagalia tu mfumo wa nchi zetu, nepotism kila mahali, sio kwa ajira au tenda za biashara,tuna mengi machafu tena machafu hasa na ukithubutu gusa maslahi yao wapo tayari kukumaliza, waafrika tunalaumu bure wazungu.
Cha ajabu ndio tunajaa sehemu za ibada kuomba huruma ya Mungu.
 
Hizo hadithi ama historia zimeshapitwa na wakati. Kama baba yako alisaidia mtu halafu akaja kua tajiri haikupi wewe uhalali wa kwenda kudowea au kung'ang'ania vitu vyake eti kisa baba yako alimsaidia. Hayo yameshapitwa na wakati.

Waafrika tunashindwa nini leo kutengeneza mataifa yetu na kukimbilia mataifa ya wengine, kipindi wanayajenga tulikuwepo? Kama tunataka maisha mazuri na mazingira mazuri ya kuishi tuyatengeneze hapa kwetu.
Kwanza naomba tukubaliane kitu kimoja: Afrika ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Bara la Ulaya. Let's set the record straight. Kwa mfano, leo hii ukichukulia utajiri wa Ubelgiji, kwa asilimia kubwa umejengwa na Congo. Kwa bahati mbaya sina muda wa kuingia kwenye hili, ila kuna mengi yameshaandikwa.

Pili, japo siafiki swala la kuzamia kwa waafrika kwenda Bara la Ulaya au Marekani, ila hili pia ni matokeo ya baadhi ya sera zao barani Afrika, kwa karne kadhaa sasa. Wengi waliozamia wanatoka kwenye nchi zilizopitia machafuko, ambazo kuna baadhi wao walichochea machafuko hayo. Simply "The chickens have come home to roost"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom