Mzozo waibuka katika kikao cha madiwani Shinyanga kufuatia upotevu wa Bilioni moja


Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
5,629
Likes
6,195
Points
280
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
5,629 6,195 280
Mzozo na malumbano mazito yametwala katika kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakihoji upotevu wa fedha zaidi ya Shiligi Bilioni moja kati ya mabilioni kadhaa ya miradi ya maendeleo huku wakilalamikia kukalia meza mbovu na viti vya plastiki na kulazimika kubebanisha viti viwili viwili wakati wa vikao kwa hofu ya kuanguka wakati fedha nyingi zinatumika tofauti na taratibu na shwria ya manunuzi.
Malumbano hayo yaliyoibuka katikati ya kikao juu ya upotevu wa fedha za miradi ikiwemo dampo la kutupia taka ngumu yameibua hoja nyingi huku madiwani wakilalamika baadhi ya wakandarasi kupewa kazi bila tenda kutangazwa wazi hali iloyotajwa kuwa ina viashiria vya rushwa.

Kufuatia hali hiyo Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mh.Agnes Machia akalazimika kutuliza malumbano hayo na kumuomba Mkurugenzi kujibu hoja zinazolalamikiwa na waheshimiwa masiwani huku baadhi ya yao wakiomba baraza ligeuke kuwa kamati bila mafanikio.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bw.Geophrey Mwangulumbi akawataka wadiwani wanaolalamika wapeleke malalamiko maandishi ili aweze kuyafanyia kazi na kurudisha mtejesho.

- ITV
 

Forum statistics

Threads 1,236,754
Members 475,220
Posts 29,267,790