ngulukizi
JF-Expert Member
- Oct 10, 2018
- 510
- 1,431
Yanga SC imeingia katika mzozo na Kampuni ya uwakala wa mechi inayojulikana kama ENDA TOUR ambayo inatambulika na FIFA, kwa KUKIUKA MAKUBALIANO ya kimkataba.
Yanga inasemekana waliingia mkataba na Kampuni hiyo ili iandaliwe kambi ya mazoezi na mechi wakati huu wa maandalizi ya msimu (Pre-season).
Kambi ilipangwa kuwa nchini UTURUKI kwenye Jimbo la Kocael kitongoji cha Kartepe kwenye Hotel ya GREEN PARK, na mtu waliekuwa wanawasiliana nae anaitwa ABDULFATAH FAD.
Kambi ilikuwa ianze tarehe 15/7 /2022 mpaka taerehe 4/8/2022 ikichukua watu 50 wa Yanga ambao ni pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.
Kwa mujibu wa mkataba kama Yanga wangeamua kuachana na kambi hiyo siku 10 kabla ya tarehe 15/7/2022 wangelazinika kulipa 20% ya malipo yote waliyokubalina ya Dola za Marekani 87,000/ ($87,000) ambayo ni zaidi ya 200,000,000/=
Lakini kama wakiamua kughairisha ndani ya siku 9 kabla ya tarehe 15/7/2022 wanalazimika kulipa 100% ya dola 87,000/=
Yanga kupitia kwa CEO wao SENZO MBATHA wameandika barua pepe leo tarehe 14/7/2022 wakieleza kugahirisha kambi hiyo ya Uturuki.
Sababu ikiwa ni ratiba ngumu waliyopokea kutoka Bodi ya Ligi. Akaomba msamaha kwa usumbufu utakaojitokeza.
Senzo alijibiwa kwa kuulizwa kwanini anaghairishaje safari leo ilihali timu nyingine waliyoingia nayo mkataba inakuja kesho, tarehe 15/7.
Pia anakumbuka kwamba wana mkataba ambao unasema ukighairisha kambi zikiwa zimebaki siku 9 kabla ya siku unayotakiwa kuwa kambini unapaswa kulipia 100% ya malipo na kuamliwa KULIPA hiyo pesa ndani ya wiki hii.
Taarifa zinasema ENDA TOUR wanajiandaa kuleta malalamiko TFF kabla ya kwenda FIFA kama ilivyo ada.
BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)C/P