Mzozo wa wafanyabiashara Arusha ,MONABAN alia na Jaji

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
84
271
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasan ametakiwa kuwamulika majaji wa mahakama kuu ambao baadhi yao wamekuwa na tabia ya kupindisha haki baada ya kurubuniwa kwa kupokea rushwa.

Hatua hiyo umekuja kufuatia kulalamikiwa kwa maamuzi yaliyotolewa na jaji Moses Mzuna katika shauri la madai ya ardhi namba 1/2021 ambapo jaji Mzuna alitoa ushindi ambao lililalamikiwa kwa kukiuka taratibu na kumpa ushindi mdai ambaye ni William Taitas.

Katika shauri hilo Taitas alikuwa akimlalamikia Dkt Philemon Mollel (Monaban)kwamba alivamia eneo lililoachwa na marehemu Baba yake na yeye Kama msimamizi wa mirathi aliamua kukusanya Mali za marehemu kwa kuamua kufungua shauri mahakamani wakati msimamizi wa mirathi halali Jimmy alikwishauza baadhi ya mali zingine mwaka 2009.

Maamuzi ya jaji Mosses Mzuna aliyoyatoa Mei 7 mwaka huu na kumpa ushindi Taitas, alimtaja Mollel Kama mvamizi ,Jambo ambalo Mollel hakuridhika na maamuzi hayo na kuamua kukata rufaa mahakama ya rufani.

Mollel anadai kwamba hukumu hiyo ilijaa upendeleo usiomithirisha kwani jaji Mzuna hakuzingatia kwamba eneo hilo alilipata kihalali kutoka kwa Mtoto wa marehemu aitwaye Jimmy Taitas.

Jaji Mzuna anadaiwa kutoa upendeleo wa wazi kwa Taitas bila kuzingatia kwamba maamuzi yake yanaweza kuleta athari kwa waahusika .

Wakili wa Mollel, Kapimpiti mgalula

Alisema kwamba hawakuridhishwa na maamuzi ya mahakama kuu hususani mahakama kuu haikueleza kwamba mikataba ambayo Mollel aliingia ni batili au sio batili, pia uwekezaji aliouweka kwenye eneo Hilo haukuzungumziwa.

Na kwamba mahakama kuu haikuzingatia kuwa Mollel alishakabidhiwa hati za umiliki, pia muuzaji Jimmy taitas Mollel aliwahi kukiri mahakamani kwamba ni kweli aliuza Hilo eneo madai ambayo hayakuzingatiwa.

Kufuatia maamuzi hayo ya mashaka Mollel amemwomba rais Samia kuingilia kati kwa kutuma mamlaka zake kuweza kuchunguza na kuitisha upya shauri hilo ili ukweli uweze kujulikana.

Kufuatia mkanganyiko wa maamuzi ya jaji Mzuna, jaji wa mahakama hiyo Abdalah Gwae alilazimika kuingilia kati na kuwaita mahakamani pande zote na kuwataka kukaa kwa amani wakati wakisubiri maamuzi ya mahakama ya rufani huku kituo Cha mafuta kikibaki chini ya ulinzi wa polisi

Mollel analalamikia kufungwa kwa kituo cha mafuta na kusitishiwa biashara zake zingine pasipo kufuata utaratibu .
 
Si wanasema amekata rufaa? Kelele za nini? Kwa nini asisubiri majibu ya rufaa? Anataka rais aingilie maamuzi ya mahakama? Huyu jamaa ni bure kabisa.
 
Si wanasema amekata rufaa? Kelele za nini? Kwa nini asisubiri majibu ya rufaa? Anataka rais aingilie maamuzi ya mahakama? Huyu jamaa ni bure kabisa.
Ndio waliokuwa wagombea ubunge Jimbo la arusha mjini mwaka 2015, angepata ushindi wa ubunge angekwenda bungeni kutunga sheria.
 
Tajiri wa Machame safari bus , naye alivamia eneo la yatima na kujenga kituo cha mafuta, kule kilimanjaro soon atakimbilia kwa Rais.
 
Yani kila anayeshindwa kesi aombe Rais aingilie Kati? Si akate rufaa Kama anaona ameonewa.
Huyo anaona ushahidi hauko upande wake sasa anataka kugeuza liwe jambo la kisiasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom