Mzozo wa Tigray Ethiopia: Waziri mkuu aamuru mashambulio dhidi ya mji wa Mekele

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,865
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray kwanza kushambulia mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle.

Amesema wanajeshi watajaribu wasiwajeruhi raia na wito kwa watu katika mji huo kusalia majumbani mwao.

Hatua hilo inajiri baada ya muda wa mwisho uliyotolewa kwa wapiganaji wa Tigray kujisalimisha kumalizika siku ya Jumatano.
Chama cha TPLF, ambacho kinadhibiti mji wa Mekelle, kimeapa kuendelea na mapigano.

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na maelfu ya wengine kutoroka makwao huku vikosi vya muungano vya Ethiopia vikiteka miji kadhaa ya Tigray kutoka kwa wapiganaji wa TPLF.
Hata hivyo ni vigumu kupata maelezo kuhusu mapigano hayo kwasababu mawasiliano ya simu na huduma za intaneti katika jimbo la Tigray yamekatizwa

tygray

Mzozo huu unahusu nini?​

Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa kwa misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja, national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.

Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.
Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "

Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzozo wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.

ethiopia

Kwa upande wake, Waziri Mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanahujumu mamlaka yake.

Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".
Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi ya majeshi.
 
Kila mwananchi amepewa siraha kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mauaji ya kimbari
Hii inanikumbushia ile series ya game of thrones,
Cersei alipoona mji unavamiwa na anakuja kuondolewa alikusanya watu wote kwenye mji ili adui wake apate wakati ngumu kufanya maamuzi

Akivamia mji basi itabidi aue maelfu ya watu wasio na hatia na ataonekana katili wa ajabu, akiacha kuivamia ataendelea kumpa Cersei muda wa kutawala na kumpa muda wa kujipanga zaidi na vita
 
nakumbaka aisee ila subiri tuone ethiopia itachukua hatua gani maana kila mtu ktk mji wa makele kapewa silaha aina ya ak 47
 
Tigrey wamemwambia pm wa ethiopia kuwa hawajui vizuri watigrey na watamtia adabu
 
Silaha walizogawa kwa wananchi zinakuja kua janga kubwa sana kwao.
Nchi haitatawalika
 
Mwanzo walikua wanatetea jimbo lao sasa hivi ndio wanaenda kuchukua nchi na kuuondoa uongozi wa waziri mkuu Abby Ahmed madarakani.
 
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray kwanza kushambulia mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle.

Amesema wanajeshi watajaribu wasiwajeruhi raia na wito kwa watu katika mji huo kusalia majumbani mwao.

Hatua hilo inajiri baada ya muda wa mwisho uliyotolewa kwa wapiganaji wa Tigray kujisalimisha kumalizika siku ya Jumatano.
Chama cha TPLF, ambacho kinadhibiti mji wa Mekelle, kimeapa kuendelea na mapigano.

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na maelfu ya wengine kutoroka makwao huku vikosi vya muungano vya Ethiopia vikiteka miji kadhaa ya Tigray kutoka kwa wapiganaji wa TPLF.
Hata hivyo ni vigumu kupata maelezo kuhusu mapigano hayo kwasababu mawasiliano ya simu na huduma za intaneti katika jimbo la Tigray yamekatizwa

tygray

Mzozo huu unahusu nini?​

Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa kwa misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja, national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.

Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.
Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "

Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzozo wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.

ethiopia

Kwa upande wake, Waziri Mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanahujumu mamlaka yake.

Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".
Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi ya majeshi.
Sisi Waafrika kiukweli tujitazame Vizuri na tujitathmini pia.

Tunanunulika kwa vipande vya mikate ama kwa thamani ndogo saana.

Nyuma ya #TPLF kuna watu ambao wanawapa Nguvu na msaada mkubwa tu ili kuidhoofosha serikali ya Abby Ahmed.

Kwa namna ya pekee kitu ambacho kitaweza kuisaidia kwa sasa ni pande zote mbili yaani Serikali na TPLF kukaa mezani na kufanya mazungumzo ya pamoja yenye malengo ya kumaliza mgogoro huo kwani kwa sasa ndio njia pekee ya kuondoa changamoto hiyo.

Tunaamini kuwa njia ya #Mazungumzo inaweza kutoa matunda na sio kupigana kwani tangu mgogoro huo ulipoanza umeharibu uchumi wa nchi hiyo, kuongezeka kwa uharibifu wa makazi, Wananchi kukosa makazi na vifo vingi.

#WAAFRIKA TUACHE PROPAGANDA ZA NCHI ZA MAGHARIBI TUNALIHARIBU BARA LETU NA KUPOTEZA WATU WETU NA KUHARIBU UCHUMI WETU, MUNGU IBARIKI AFRIKA.
 
Back
Top Bottom