Mzozo wa mpaka wajaza Wamalawi ubalozini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzozo wa mpaka wajaza Wamalawi ubalozini Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 12, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Hofu ya mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi, jana ulisababisha kundi kubwa la raia wa nchi ya Malawi wanaoishi Tanzania kujazana kwenye ofisi ya ubalozi wao uliopo barabara ya Rose Garden Mikocheni B jijini Dar es Salaam, baada ya kutumiwa ujumbe kuwa wanahitajika kuonana na balozi.

  Raia hao walijazana ubalozini hapo tangu saa 3 asubuhi wakisubiri kuambiwa kile walichoitiwa na balozi wao.

  Hata hivyo, raia hao baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila kuambiwa lolote, mmoja wa maafisa wa ubalozi huo, aliwateuwa wawakilishi watatu ili kuweza kuzungumza na Balozi Flossie Chidyaonga.

  Wawakilishi hao baada ya kukutana na Balozi Chidyaonga, walimfahamisha wameenda hapo ili kuitikia wito uliowataka kufika ubalozini ili kukutana naye, kutokana na taarifa zilizosambazwa kwa ujumbe wa simu kuwa Wamalawi wote waishio jijini Dar es Salaam, wanahitajika.

  Lakini Balozi Chidyaonga alisema taarifa hizo si za kweli, kwani hakuna afisa yeyote wa ubalozi aliyetumwa kutoa taarifa hiyo.

  “Hapana taarifa hizo si sahihi, hakuna aliyetumwa kuwaita kufika hapa…nashangaa kuwaona mmejazana katika ofisi hii, naomba muwataarifu wenzenu balozi hajatoa taarifa hizo walizozisikia,” alisema Balozi Chidyaonga kwa lugha ya kinyasa.

  Balozi huyo alisema, kama mwakilishi wa Rais wa Malawi, Joyce Banda, anafanya kazi kupitia taarifa toka kwa bosi wake huyo, lakini mpaka sasa hajapewa taarifa zozote za kuitisha kikao cha kukutana na raia wake.

  Hata hivyo, Balozi Chidyaonga alisema kutokana na taifa la Tanzania kuingia katika zoezi la Sensa kwa watu wake, aliwashauri raia wa Malawi waishio nchini kuhakikisha wanapata vibali vya kuishi katika nchi hii ili wasitibue hesabu za Watanzania.

  “Naomba muwafahamishe na wenzenu, kama hawana vibali vya kuishi Tanzania waje hapa kujitambulisha kisha waende ofisi za Uhamiaji kule Posta kulipia dola 50 (sawa na Sh.80,000 za kitanzania), wawe na amani zaidi ya kuishi,” alisema balozi huyo.

  Aidha, balozi huyo alisema Tanzania ni nchi nzuri yenye amani ambayo hakuna raia anayeulizwa utambulisho wake, labda anaweza kuulizwa hayo iwapo atafanya kosa litakalomfikisha kwenye vyombo husika.

  Hivi sasa raia wa Malawi waishio nchini, wameingiwa na woga kutokana na utata wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi ambapo kuna utata kuhusu mpaka katika Ziwa Nyasa huku kila upande ukidai ni mali yake.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  tanzania ni nchi nzuri ambayo hakuna mtu anaulizwa uraia wake. Viongozi wetu wanapenda kusifiwa kijinga namna hii. Nje watu wanaishi kwa kufungiwa ndani, huku kwetu tunaendekeza upumbavu. Wameandikisha kwenye vitambulisho wasomali wengi sana. Hili halifichiki, kwani inafahamika kabisa kina kinana wanafanya biashara za watu ila ndo waliopewa madaraka makubwa kwenye genge la uhalifu linaloongoza nchi hii
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Tena kama hivi vitambulisho vya mpiga kura Wanyarwanda kibao wanavyo, Warundi kibao wanavyo so huwa nashangaa sana wanaposema mtu awe na moja ya hivi vitu i.e kitambulisho cha mpiga kura. Sasa hivi wimbi kubwa la wanywarwanda ambao wanavitabulisho vya mpiga kura wanaingia nchini kwa sababu wamesikia kuwa tunatoa vitambulisho vya uraia so wanawahi na wao waandikishwe kabla ya 'dedilaini' Kweli tusipokuwa makini 70% ya wageni watapata uraia bila jasho hivyo siku moja kutufanya watumwa kwenye nchi yetu.
   
 4. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  balozi wetu malawi nae anasemaje? au ni bata kama kawa
   
Loading...