Mzozo wa Israeli na Palestina: Netanyahu asema oparesheni itaendelea huku Biden akitaka mapigano kukomeshwa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Afisa mwandamizi wa Hamas amesema kuwa anatarajia Israeli na wapiganaji wa Kipalestina huko Gaza kufikia usitishaji wa mapigano "ndani ya siku moja au mbili" wakati mashambulio ya mpakani yakiendelea.

Lakini Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema Jumatano alikuwa "ameamua kuendelea" hadi "utulivu na usalama urejeshwe kwa raia wa Israeli".

Kulikuwa na zaidi ya mashambulizi 100 ya angani ya Israeli dhidi ya miundombinu ya Hamas kaskazini mwa Gaza mapema Alhamisi.

Wapiganaji wa Palestina walilipiza kisasi kwa roketi wakiilenga Israeli.

Mapigano ya Gaza yalianza baada ya wiki kadhaa za kuongezeka kwa mvutano wa Israeli na Wapalestina katika Jerusalem ya Mashariki iliyokaliwa ambayo ilimalizika kwa mapigano kwenye eneo katifu linaloheshimiwa na Waislamu na Wayahudi. Hamas, ambayo inadhibiti Gaza, ilianza kufyatua roketi baada ya kuionya Israeli ijitoe kutoka kwa eneo hilo , na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi

Takriban watu 227, wakiwemo zaidi ya wanawake na watoto 100, wameuawa huko Gaza hadi sasa, kulingana na wizara yake ya afya. Israel imesema angalau wanamgambo 150 ni miongoni mwa waliouawa huko Gaza. Hamas haitoi takwimu za majeruhi kwa upande wao .

Nchini Israeli watu 12, pamoja na watoto wawili, wameuawa, huduma yake ya matibabu inasema. Israeli inasema kuwa makombora 4,000 yamerushwa kuelekea eneo lake na wanamgambo huko Gaza.

Afisa huyo wa Hamas alisema nini?

Nadhani juhudi zinazoendelea kuhusu usitishaji vita zitafanikiwa, "afisa wa kisiasa wa Hamas, Moussa Abu Marzouk, aliiambia televisheni ya al-Mayadeen ya Lebanon.

"Natarajia mapigano kusitishwa ndani ya siku moja au mbili, na usitishaji wa mapigano utakuwa kwa msingi wa makubaliano ya pande zote."

Maoni hayo yanakuja wakati shinikizo la kimataifa likiongezeka kwa Israeli na wanamgambo wa Palestina kumaliza uhasama.


Chanzo cha usalama cha Misri kililiambia shirika la habari la Reuters kwamba pande hizo mbili zilikubaliana kimsingi kusitisha vita baada ya msaada kutoka kwa wapatanishi lakini mazungumzo bado yanaendelea.

Siku ya Jumatano, Rais Biden alizungumza na waziri mkuu Benjamin Netanyahu kwa mara ya nne sasa tangu mzozo uanze.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya White House ilisema: "Rais alimfikishia waziri mkuu ujumbe kwamba anatarajia kupungua kwa mapigano kwa kiwango kikubwa leo katika hatua ya kusitisha mapigano."

Jaribio la hivi karibuni la azimio la Baraza la Usalama la UN linalotaka kusitishwa kwa mapigano, lililozinduliwa na Ufaransa, lilishindwa mnamo Jumatano wakati Marekani iliposema inaweza "kudhoofisha juhudi za kumaliza uhasama "

Nini kinafanyika katika maeneo ya mapigano?

Mapigano yameendelea huku Israeli ikizindua msururu wa mashambulio ya anga huko Gaza mapema Alhamisi, na kuharibu nyumba mbili. Madaktari walisema watu wanne walijeruhiwa katika shambulio la angani katika mji wa Khan Younis.

Israeli ilisema ilikuwa imelenga "maeneo ya kuzindua roketi na mfumo wa kujikinga dhidi ya mashambulizi ya angani" ambayo ni mali ya Hamas.

Ving'ora vya roketi vilisikika katika mji wa Israeli wa Beersheba na katika maeneo karibu na mpaka wa Gaza, wakati wapiganaji wa Gaza waliporusha makombora. Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa.

Nini kilisababisha mapigano?

Mapigano kati ya Israeli na Hamas yalisababishwa na siku kadhaa za kuongezeka kwa mapigano kati ya Wapalestina na polisi wa Israeli kwenye uwanja mtakatifu wa kilima huko Mashariki mwa Yerusalemu.

Eneo hilo linaheshimiwa na Waislam wote, ambao huiita Haram al-Sharif (Patakatifu Pema), na Wayahudi, ambao kwao linajulikana kama Mlima wa Hekalu. Hamas ilidai Israeli iwaondoe polisi kutoka huko na wilaya iliyo karibu zaidi ya Kiarabu ya Sheikh Jarrah, ambapo familia za Wapalestina zinakabiliwa na hatari kufukuzwa na walowezi wa Kiyahudi. Hamas ilizindua makombora wakati makataa yake hayakutiliwa maanani.

Hasira ya Wapalestina tayari ilikuwa imepanda baada ya wiki kadhaa za mvutano ulioongezeka huko Mashariki mwa Jerusalem, uliowashwa na mfululizo wa makabiliano na polisi tangu katikati ya Aprili.

Ilichochewa zaidi na sherehe ya kila mwaka ya Israeli ya kuadhimisha kudhibiti Yerusalemu ya Mashariki katika vita vya Mashariki ya Kati vya 1967, inayojulikana kama Siku ya Yerusalemu.






FB_IMG_1621489400228.jpg


FB_IMG_1621439473835.jpg


FB_IMG_1621343041128.jpg
 
Back
Top Bottom