Mzizi mkavu na wengineo wenye ufahamu; Msaada pls!! Maumivu ya Miguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzizi mkavu na wengineo wenye ufahamu; Msaada pls!! Maumivu ya Miguu

Discussion in 'JF Doctor' started by Rubi, Nov 15, 2011.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kuna mwalimu wangu (umri wake, sijui lakini ni mtu mzima kwenye miaka 50) ambaye amekuwa kama rafiki na kama mama yangu! ana tatizo linamsumbua la miguu kuuma. Miguu yenyewe inavyomuuma ni sehemu ya mbele kwenye ugoko lakini sio kwenye mifupa ni kwenye nyama eneo la kati.

  Sehemu nyingine kama kwenye joint n.k hasikii maumivu yoyote hivyo anaweza kutembea , kuchuchumaa, kubeba vitu n.k. tatizo ni hilo eneo la kati kwenye miguu yote miwili anasema inawaka kama moto, usiku halali na ameshakwenda kwenye hosipitali mbalimbali na dawa mbalimbali ametumia. hata niandikapo hapa yuko anatumia dawa lakini anadai hakuna nafuu. na anasema hosipitali walimwambia watampiga e-ray mara baada ya kumaliza dawa ingawa wamemwambia kuwa wanamashaka kama wataona kitu kwa kuwa tatizo liko kwenye nyamasio kwenye mifupa.

  Kwa kweli kama binadamu nimemuhurumia kwa mateso anayopata na kibaya zaidi anaonekana kukata tamaa mpaka kuhisi labda amerogwa. ingawa tunampa moyo asifikiri hivyo ila maumivu ayapatayo bila kujua ni nini ndio yanayompotezea tumaini.

  Hivyo wa JF najua jukwaa hili ni zaidi ya shule mbali ya kuwa msaada kwa wengi pengine nami nitaweza kupata chochote kutoka kwenu nitakachoweza kumsaidia.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa kuumwa na Mwalimu wako kwa Ushauri wangu kam sijatoa Dawa zangu mimi ningependa umuulize alishawahi kutumia Dawa gani za hospitalini ? Angelikupa majina ya hizo dawa ingelikuwa Vizuri na pia kuhusu suala la kupiga X-Ray ingelikuwa bora zaidi afanye hivyo ili tupate kujuwa Ma Daktari wameona kitu gani kwenye hiyo X-Ray? nitakupa baadhi tu ya dawa kama first aid

  (1)Mwambie awe anakula Mabamia 3 mabichi awe anakula hayo Mabamia kama anavyo kula Matango kila usiku hii itaweza kumsaidia kupona inshallah.


  (2)Dawa ingine ajaribu kutumia Dawa inayoitwa kwa jina ( Diclofenac 100mg) awe anakula asubuhi baada kula chakula kidonge kimoja na usiku baada ya kula kidonge kimoja ajaribu pia hiyo dawa kutumia itaweza inshallah kumsaidia.

  (3) Pika kuzu-bara kwa kiingereza inaitwa (Coriander) pamoja na hinna na siki (kwa kiingereza inaitwa Vinegar Apple)pamoja na unga wa (shairi)ni unga wa ngano kisha uweke au upake pale penye maumivu.

  (4) Ukipika sarjal (quince) pamoja na maji ya shairi (ngano) ikisha upake panopouuma, huponza maumivu.

  (5) Kijiko kimoja kikubwa cha kulia Wali Asali safi ya nyuki ukinywa pamoja na Kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali mafuta ya habbat Sauda kwa kiingereza yanaitwa (Nigella seed oil)huondosha maumivu ya viungo.

  (6)Ukisaga kuzu-bara (Coariander) au maji yake pamoja na Maji ya Busanji(violet) na unga wa lozi kisha paka katika viungo vinavyouma. Inshallah Maumivu yataondoka.

  Muhimu Umfahamishe mgonjwa katika hizo dawa 6 nilizozitaja hapo juu anaweza kutumia Dawa za Kwanza hapo juu yaani namba (1) na namba (2) anaweaza kutumia kwa Kwa wakati mmoja kwa muda kama wiki moja huku anaangalia matokeo yake hakupata nafuu. Anaweza kutumia dawa namba 3 na namba (5) kwa wakati kutwa mara 3 asubuhi mchana na usiku atuymie kwa wakati

  Mmoja akatumia kwa muda wa wiki moja kama bado hajapona anaweza kutumia Dawa namba (4) pamoja na namba (5) kwa wakati mmoja kwa muda wa wiki moja kutwa mara tatu Asubuhi Mchana na usiku. ikiwa bado hajapona anaweza pia kutumia Dawa namba (5) na namba (6) kwa

  wakati mmoja kutwa mara tatu Asubuhi Mchanana Usiku kwa muda wa wiki mmoja kisha atupe maelezo yake amefikia wapi? Inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu atapona tu.
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mzizi nashukuru kwa majibu yako naamini yatawawsidia wengi siyo yeye tu. nitaprint for future use. ila nina swali

  1. Hizo bamia kweli unaweza kuzitafuna mbichi bila kusikia kutapika, maana mimi napenda kula bamia ila nimezoea kula zilizopikwa sasa sijui hizo mbichi kama zaweza pita kooni bila matatizo au waweza kuchangana na kitu kingine kama kwenye saladi na ndimu.

  2. Na hizo bamia akiwa anazitumia atazitumia kwa muda gani mfululizo ili ajue kuwa kuna mabadiliko. je ziwe na ukubwa kiasi gani (i.e urefu wa cm 6 mfano) maana zingine zinakuwa ndogondogo sana na zingine zinakuwa kubwa au haijalishi?

  3. hiyo diclofenac pia atumie kwa muda gani?

  4. Suala la x-ray walimwambia mpaka amalize dawa. Kwa sasa anatumia dawa nitamuuliza majina ya dawa anazotumia na alizowahi kutumia.

  5. Je inawezekana mwanamke anayeingia au kukaribia 'menopouse' akasumbuliwa na tatizo la miguu? maana anasema madaktari wengine katika kuhangaika kutafuta tiba waliwahi kumwambia hivyo?

  ubarikiwe.
   
 4. Akthoo

  Akthoo JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  No. 5 Most probably to be the root cause of the suffering!
   
 5. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  call this no and express your problem 0754076117
   
 6. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa tatizo lake likawa limesababishwa na menopause. Kwa kawaida kina mama wakishafikia umri wa kuanzia miaka 45 mpaka 55 wanakuwa katika kipindi kinachoitwa pre-menopausal ambapo dalili mojawapo ni kuwa na damu za hedhi zinakuwa hazieleweki ( menstrual irregularities), maumivu ya mifupa na joints, kutokwa na jasho mara kwa mara na baadaye kufuatiwa na vipindi vya baridi (hot flushes) na dalili nyingine.

  Huyo mama unaweza kumshauri atumie estrogen suppliments na calcium tablets (Hormonal replacement therapy) nadhani atapata nafuu.
  Diclofenac siishauri sana kwa sababu, ikitumiwa kwa muda mrefu uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo ni mkubwa.

  Mpe pole huyo mgonjwa, naamini mungu atamponya.
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Duh! Uko juu! Yani mtu humu JF akifa kwa magonjwa yanayotibika ni uzembe wake tu!
   
 8. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mkuu itabidi tuanzishe na hospitali ya JF
   
 9. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Mzizi mkavu na mganga wa jadi na wengneo wote wanaotoa ushaur mzur wa manufaa bla choyo...huyo anayeyaongoza maisha ya bnadam yeyote (anayekubal na asiyekubal) awazdshie rehema, baraka na maisha maref
   
 10. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwa maelezo yake ya awali kwanza anasema vidonge hivyo vya calcium ameshavitumia sana kwa maelekezo ya dk. pili hasikii maumivu kwenye joint (viungio) wala kwenye mifupa maumivu yake yako kwenye nyama upande wa mbele wa miguu tena katikati. na kwa kuwa hasikii maumivu kwenye joint ndio maana anatembea bila shida, kuinama, kuchuchumaa na kazi zake anafanya kama kawaida. Tatizo akiwa ametulia au jioni kajipumzisha na wakati wa kulala maumivu yanakuwa makali sana tena yanawaka kama moto kiasi cha kumfanya kukosa usingizi.
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Bamia tatu haziwezi kupita kooni?basi zitakuwa sumu mkuu Atumie hizo bamia kwa mpaka atakpoona mabadiliko yani amepona.
   
Loading...