Mziray wa APPT Maendeleo ampigia debe Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mziray wa APPT Maendeleo ampigia debe Dk Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Saint Ivuga, Oct 7, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  Mziray wa APPT Maendeleo ampigia debe Dk Slaa Send to a friend Thursday, 07 October 2010 08:08 0diggsdigg

  Sheilla Sezzy, Mwanza

  MGOMBEA urais kwa tiketi ya APPT-Maendeleo, Peter Kuga Mziray ametumia muda wake wa kampeni kumnadi mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa.

  Akiwahutubia wakazi wa Jiji la Mwanza katika viwanja vya Sahara , Mziray huku akimtaja mara kwa mara Dk Slaa alisema wagombea wa vyama vya upinzani ni makini na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kumchagua Dk Slaa.

  Alisema umakini wao upo tofauti na wamgombea wa CCM, Jakaya Kikwete na kudai kuwa amekuwa akitoa ahadi nyingi zisizotekelezeka.

  Alisema kuwa Watanzania inabidi kudhihirisha umakini wao siku hiyo ya Oktoba 31 kwa kuwapigia kura wapinzani na sio wale wa CCM.

  Mziray alisema mbali na kumchagua Dk Slaa, pia wananchi wa Jimbo la Nyamagana wamchague mgombe wa Chadema, Ezekie Wenje katika nafasi ya ubunge kwa sababu ni kijana mwenye uwezo mkubwa na atakayewasaidia kutatua shida zao.

  "Pamoja na kumchagua Slaa, ambaye ni dokta wa kweli wa kusomea nafasi ya ubunge katika jimbo la Nyamagana, kuna wagombea wawili tu, hivyo mchague huyo wa Chadema,"alisema Mziray huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi waliohudhuria mkutano huo, wengi wao wakiwa ni vijana.

  Alisema vijana hapa nchini wamekuwa na maisha magumu kiasi cha kushindwa kuwapa fedha au kuwanunulia zawadi wapenzi wao kutokana na chama tawala kushindwa kuendesha nchi vizuri na kusababisha kupanda kwa bei ya vitu kila kukicha.

  "CCM ndio imewafanya nyie vijana mshindwe hata kuwapeleka ‘ma-girl friends wenu saluni au kuwapa fedha za kuwanunulia zawadi kwa sababu ya ugumu wa maisha, "alisema Mziray.

  Alisema tangu Kikwete aingie madarakani miaka mitano iliyopita, bei ya vitu imekuwa ikipanda kwa kasi na kusababisha watu wengi washindwe kufurahia maisha yao.

  Akiendelea kumpigia debe Dk Slaa, Mziray alisema kwamba anatafuta kura nyingi, lakini: “Tuseme ukweli kuna mzee mzima (akimaanisha Slaa) anatisha sana, na mimi Peter Kuga Mziray ni sawa na mchezaji wa akiba katika timu kali huku akifafanua kuwa timu haiwezi kucheza bila ya kuwa na mchezaji wa akiba."

  Pia mgombea huyo alitumia muda kujisifia kwa kusema kuwa yeye ni msomi aliyesomea Urusi kwa miaka sita na ana shahada ya udhamili na kuongeza kuwa ana magari matatu na moja alinunua mwenyewe nchini Japan.

  Alisema chama chake kina uzoefu mkubwa katika kugombea urais kwani mwaka 2005 walimsimama mwamama, Anna Claudia Senkoro.

  Alisema endapo APPT-Maendeleo itaingia madarakani au chama chochote cha mageuzi, kamwe hawataendekeza urafiki na badala yake watakuwa makini kwa kufuata taratibu na sheria, na Ikulu itakuwa ya kwanza kufunga mikanda kwa kubana matumizi ili wananchi wafaidike na fedha zao.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  nani anaweza kuzuia moto wa DR Slaa?? Aka SIRAHA.
   
 3. K

  Kashishi JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 1,101
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
   
Loading...