Mziray AMEJISHUSHIA heshima yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mziray AMEJISHUSHIA heshima yake

Discussion in 'Sports' started by Bongolander, Aug 8, 2010.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nimesoma makala moja iliyotolewa na kocha wa zamani S Mziray kwa kupongeza kuitwa kwenye timu kwa Mchezaji J Kaseja na Chuji. Sina hakika kama kweli kocha wa timu ya taifa anachagua wachezaji au anachaguliwa wachezaji, kama anachagua wachezaji basi atakuwa anajua anachofanya, kama anachaguliwa wachezaji basi atakuwa hajui undani wa wachezaji hao, hasa yule aliyeshangilia kuona timu ya taifa inafungwa.

  Kitendo cha Mziray kusifu uamuzi huo kinaonesha ufinyu wa mawazo, yeye kama kocha alitakiwa kuwa kiongozi au kuwasaidia makocha wageni kuweka nidhamu kwenye timu.

  Nitasikitika sana kuona kuwa Maximo ameondoka na nidhamu yake, sisi tunabakia na mafamba.
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sioni hoja hapo. Kwani adhabu ya ukosefu wa nidhamu ni kumfungia mchezaji milele? Huyu naye akiona hawana nidhamu si atawatosa? Yaani wewe unaona ni nafuu zaidi kulinda nidhamu kwa kupoteza michezo kila kukicha ilihali tunao wachezaji wenye uwezo? Sikubaliani na wewe katika hili. Mziray kama kocha anajua anachokifanya. Mchezaji asiye na nidhamu huwa ana adhabu yenye mipaka na siyo kumfungia maisha.
   
 3. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi naona Mziray yupo sawa kabisa, maana alianza kulizungumza jambo hili siku nyingi sana. Jambo moja nimeliona ni udhaifu, unafiki, woga wa TFF. Lazima watueleze kwanini wachezaji hawa wameitwa tena Taifa Stars. Ina maana hawa jamaa walikuwa hawana ubavu wa kusema NO kwa Maximo. Ina maana walikuwa wanafahamu kuwa Kaseja na Chuji wanaonewa na Maximo ila kwa vile walikuwa wanamgwaya ndio maana walikuwa wananyamaza tu. Hawa wameonyesha udhaifu mkubwa sana wa kiutendaji

  Sasa lazima watueleze kwanini wachezaji hawa wamerudishwa, wala wasimsingizie kocha mpya kuwa ndiye kateua hii timu- si kweli kabisa ni wao wenyewe TFF

  Hongera Mziray- ulimponda Maximo toka siku ya kwanza watu kibao wakakupinga leo hii matokeo yamejionyesha TZ haijapata taji lolote zaidi ya maneno kibao

  Pia najua ulisema huyu kocha mpya ni yale yale ya kuangalia CV badala ya kuangalia mafanikio na watu kama kawaida watapinga tu- anyway ngoja tuone muda utatuthibitishia
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  I respect your opinion.......nakumbuka kunamhcezaji mmoja anaitwa Romario Faria alileta kejeli na akawekwa kando mpaka leo, japokuwa timu yake ilimiss lakini waliona nidhamu ni jambo lenye manufaa in the long run, kuliko ushindi wa siku 2.

  So let us see kama Taifa stars itakuwa inashinda baada ya jamaa hao kurudishwa na TFF.
   
 5. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu sasa ni ubishi usio na msingi. Kocha mpya kakiri hajateua timu kwa sababu ya msingi Alichelewa kuja hivyo hawafahamu wachezaji. likaundwa jpo likiongozwa na Kayuni wala Mziray hakuwemo ndio wakawarudisha hao unaowapinga. Sasa Mziray kutoa mawazo yake tatizo liko wapi? Acha hizo kati ya hao watatu, Mziray, Chuji na Kaseja kuna mmoja alikumegea demu wako ndio maana una hasira nao sana.
   
 6. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kaka acha hasira,mbona mkali kwa jamaa!
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwani uliambiwa Taifa Stars ilikuwa inakosa ushindi wakila siku kwasababu ya kaseja na Chuji...Tatizo Maximo hakuwa wazi utovu wa nizamu alioufanya Kaseja mpaka siku anaondoka...2 kaseja ndiyo kipa bora hapa Tanzania ukikataa basi wewe mbishi hivyo basi acha Taifa stars ifungwe ikiwa na watu tunao waamini kama chuji, kaseja, Boban tutalizika maana hatutakuwa na ang'ekuwepo Kaseja...Hata timu hujiamini inapokuwa na wachezaji wenye uwezo...
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,760
  Trophy Points: 280
  Nasubiri kumwona maliga vs chuji majaaaaaaaaannnnnniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 9. p

  phenomena Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je unawakumbuka paul gazza,paul ince na boban wa crotia kwa kiwango chao kibovu cha nidhamu lkn walifanikiwa kuwika ktk timu ya taifa.pia nadhani hamna asiyemjua rooney mtoto mtukutu kama ferguson angeamua kutompanga kwa sababu ya utukutu wake leo angekuwa wapi na hakuna asiyejua mchango wa rooney old trafford.mziray yuko sawa
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Interesting argument, lakini pamoja na utukutu na manjonjo yao yooote, sijawahi kusikia wakishangilia timu zao zinapofungwa. Kusema kweli nakubali kuonekana mjinga, lakini nakubaliana na uamuzi wa Maximo wa kumuweka Kutomchagua kaseja(nina haki ya kutoa maoni hata kama ni mabaya). Siwezi kukubali ujinga wa Kasema wa kushangilia timu yake kufungwa kisa hakupangwa yeye golini. Uliowataja Kina Gazza, Boban, Ince na hata Bobic, utovu wao ulikuwa kwa mademu, jeuri, pombe na kuzozana na wenzao. wakiwekwa benchi walikuwa wanafanyakazi zaidi ili wapewe namba tena, hawakushangilia timu zao zilipofungwa, si klabu wala timu za taifa.
   
 11. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Matatizo ya Taifa Stars hayataisha kwa kuwaita Chuji na Kaseja
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tatizo huyu mziray ni mnafiki na mpika majungu sana,
  tangu nimeanza kumjua na kusoma makala za nyingi,
  huwa zimejaa mizengwe, maximo alipewa jukumu la kuwa
  kocha mkuu wa staz, na alisimamia uamuzi wake,
  tatizo la watanzania tumezoea mwalimu wa timu ya taifa,
  kuitiwa wachezaji kama huyu ***** paulsen,
  kawaona wapi hawa kina kaseja, chuji kuwa ni wazuri?
  kama tff kutawaita? maximo hakuwa na kosa kwa wenye akili,
  lakini alikuwa na kosa kwa sababu wengi wetu tunapenda sana
  kiongozi kufanya yale tunayoyaona mawazoni mwetu.
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu unachosema ni kweli. Unapokuwa kocha ni vizuri unafanya maamuzi na unayasimamia maamuzi yako na unawajibika kwa maamuzi yako. That is what Maximo did, na kocha yoyote mwenye akili anafanya hivyo. Nakumbuka Zakaria Kinanda alifanya hivyo japo alitukana nwa na watu.

  Mziray is very hypocritical, and when it comes to the manners i would say he is rotten to the core. Klabu alizofunidha hajawahi kuwa na maendeleo endelevu, kwa kuwa kila mara aliacha madonda makubwa sana yaliyoivuruga timu....ukiuliza wachezaji aliowafundisha Mziray ni mtu wa namna gani unaweza kusikitika sana....Nakumbuka Abubakar Salum alipokuwa kwenye peak, alikuwa analalamika sana kuwa jamaa anamtendea maovu, si yeye tu wachezaji wengi.

  Mziray ni hodari wa kupika majungu na ni hodari wa kubomoa, kila alipofanya kazi hakuweza kuweka msingi endelevu,isipokuwa aliweza kuweka matatizo endelevu. So, sioni ajabu kwa yeye kusifu uendelezaji wa utovu wa nidhamu.
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Monsignor, heshima zikufikie mkuu, sina kinyongo na wachezaji wala mtu yoyote kwenye timu ya taifa, labda ni uzalendo tu unaonikereketa. Nakubali kuwa tuna maoni tofauti inawezekana siko sahihi inawezekana uko sahihi.....nashukuru kwa kunifungua macho. Sikujua kama kocha mpya alichaguliwa wachezaji, labda tusibiri na yeye atakapoteua wa kwake. Naheshimu maoni yako mkuu.
   
 15. p

  phenomena Member

  #15
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka me ninavyojua maximo mpaka anaondoka hakuwahi kutangaza utovu wa nidhamu alioufanya kaseja na yameshaongelewa mambo mengi kuhusu kilichomtoa kaseja stars maximo ndo mwenye ukweli moyoni mwake.Tena kwangu mimi naona maximo hakuwa sahihi ilitakiwa atangaze hadharani utovu wao wa nidhamu walioufanya.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kukaa nje pia wameshajirekebisha katika nidhamu..sidhani kama bado wataendelea kurudia makosa
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hakutangaza hadharani, lakini ukiwauliza watu waliokaribu watakwambia hiyo ndio sababu[alishangilia Ivo Mapundo alipofungwa Goli na kum-jibe Maximo kuwa hawezi hata kuchagua golikipa mzuri], unajua ukiwa kocha ukianza kuropoka kwenye vyombo vya habari ndio kukosa nidhamu kwenyewe. Kuna baadhi ya mambo yanaishia kambini, na kuna baadhi ya mambo hayatakiwi kusemwa, yanatekelezwa kwa vitendo tu. Ukiangalia makocha wenye uwezo hawafundishi soka wala maadili yanayoendana na soka kupitia media, wanafanya hayo uwanjani. Media ni kuwaacha wa-speculate tu, kama ni kuongea nao ni kuongea nao kuhusu mambo yayaweza kuingia kwenye media.

  Simaanishi kuwa Maximo ni malaika, inawezekana kabisa alikuwa na makosa fulani kwenye ufundishaji wake.
   
 18. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kushinda au kushindwa kwa starz sio makocha....Je klabu zetu wanapotokea zikoje..? wachezaji wabadilike..
  Kucheza eti kwa kumkomoa mtu ni upuuzi...
  La muhimu Maximo katuachia ni kusimamia uamuzi wako NO MATTER WHAT...
   
 19. M

  Mubii Senior Member

  #19
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi sikupenda kitendo cha Maximo 'kufungia maisha' wachezaji kama Kaseja na Chuji. Binadamu hufanya kosa na anatumikia adhabu stahili. Lakini naona Maximo ali 'over do' hiyo adhabu. Alitakiwa awasamehe lakini haikuwa hivyo. Sisi katika dini tunafundishwa kusamehe mwenzio ni muhimu sana ili Mwenyezi Mungu aweze kukusamehe. Sasa Maximo kashikilia msimamo wake mpaka ikaonekana inakera watanzania wengi. Hata siku zake za mwisho wake kama kocha wa Stars udhaifu wake ulionekana zaidi katika maeneo wanayocheza hao 'aliowafungia maisha'. Kipa ile mechi na Brazil ilikuwa aibu tupu na kiungo kilipwaya. Jamani hapa tujifunze ili tusirudie makosa. Hivi ndivyo binadamu anatakiwa kuishi. Tuwe tayari kusamehe na tusikae navyo muda mrefu. Hata Mungu hapendi kutokusamehe.
   
 20. p

  phenomena Member

  #20
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka haupo sahihi, kuwaeleza raia ukweli angeonekana vp hana nidhamu.Kutongaza kwake ndo kulimfanya yeye aonekane mnafki,na kuhusu hizo habari za wa2 wa karibu mbona yameshaongewa mengi coz binadamu hakosi cha kuongea.wapo wanaosema kaseja na maximo walikutana ugoni,wapo wanaosema kaseja alikimbia na mpira wa dawa kulevya uliokuwa unatoka brazil enzi hizo starz ilipoenda brazil.je haya yote kayafanya kaseja?2ache kusikliza maneno ya mtaani maximo ndo alitakiwa kusema ukweli kama ameshindwa yeye ya nini sisi kuongea?
   
Loading...