Mzio wa Kukosolewa (Allergic to Criticism)

KILIVITE

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
1,302
555
Ukiona Mtu/Kiongozi/chama/timu/Kampuni haipendi changamoto za demokrasia ya kupingwa na kukosolewa mtu/chama/timu/Kampuni hiyo ina mapungufu yafuatayo;

1. Uwezo hafifu wa kuhimili basi ujue kukosolewa;

2. Uwezo hafifu waubongo katika kutafakari na kutoa majibu;

3. Uwezo hafifu wa kujenga kujiamini katika utendaji wa kazi;

4. Uwezo hafifu wa kuchapa kazi inayoonekana na kupimika na kila mtu;

5. Uwezo hafifu wa kujua upungufu na udhaifu wake na namna ya kutatua;

6. Uwezo hafifu wa kufanya jambo lililokamilika kwa asilimia mia moja;

7. Uwezo hafifu wa kufanya kazi kwa ufanisi bila makosa;

8. Uwezo hafifu wa kujibu hoja zilizopangiliwa kwa ufasaha;

9. Uwezo hafifu wa kuwa imara na umoja wa hali ya juu;

10. Uwezo hafifu wa kuondoa kero kwa watu walio karibu.

Tafakarisha ubongo wako,inua uso wako,okoa demokrasia Tanzania!!!
 
Na ukishakuwa binadamu tu basi ni lazima ukosee aidha kwa kujua ama kutokujua.....hapo ndipo umuhimu wa ukosoaji unapokuja ili kunyoosha mambo.

Ukiona mtu hataki kukosolewa basi anajipa mamlaka ya uungu.....na hilo si kweli kwani hata kina farao walishindwa.

" Kitisho kikuu cha uhuru ni kukosekana kwa ukosoaji"
 
Umenena vema Sana Mkuu lakini mhmhmhm! Ni hatari. Umemchana Mkuu wa Kaya moja kwa moja
 
Na ukishakuwa binadamu tu basi ni lazima ukosee aidha kwa kujua ama kutokujua.....hapo ndipo umuhimu wa ukosoaji unapokuja ili kunyoosha mambo.

Ukiona mtu hataki kukosolewa basi anajipa mamlaka ya uungu.....na hilo si kweli kwani hata kina farao walishindwa.

" Kitisho kikuu cha uhuru ni kukosekana kwa ukosoaji"
Seem like I am dreaming
Ungejua hili usungewachukia wapinzani wa chama chenu usingewabeza usinge watusi uzingewakebehi. ..!
Katika maisha maanisha unachonena. ..na nena unachomaanisha...! Usiwe kigeugeu wala kuwa na rangi nyingi
 
Katika muktadha wa ubinaadamu moja kwa moja unatuondolea ukamilifu....kwa hiyo kukosea ni sehemu ya madhaifu yetu kukosolewa ni majukumu ya wale walioyaona makosa yetu.....ndio maana watu wenye hekima hukubali kukosolewa....kwani kupitia kwayo ndio unapata kujifunza mambo mengi zaidi na kuzidi kupiga hatua......

Hatupaswi kuogopa wala kuchukia kukosolewa...kwani hiyo ni ishara kuwa hao wanaofanya hivyo dhidi yetu kwa namna tunayoipenda au tusiyoipenda wanatusaidia sana katika kutuweka sawa na kurudi kwenye mstari....kwa hiyo wanafanya hivyo kwa hali ya upendo ingawa wakati mwingine huwa umejificha.......

Kwa mfano unapokuwa unatoka harufu mbaya kinywani mtu anapokuweka wazi kuhusu hiyo hali yako..akiwa na maana ufanye taratibu za kuepukana na karaha hiyo na kujiepusha aibu mbele ya jamii.......
62bbf6bc262ef9d04a6db3c2648f66fc.jpg
 
Back
Top Bottom