Mzindakaya: Wanaovumisha nimekufa ni wapumbavu, bado nina nguvu kama kijana wa miaka 20

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,106
8,044
Mzinda.png
Mwanasiasa mkongwe wa CCM na aliekuwa mbunge wa Sumbawanga, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya akanusha taarifa za mitandaoni kuwa amefariki, asema afya yake ni njema.
 
Hao walio mzushia ni wachawi
Mkuu, kwa wanaoamini uchawi wanasema huyu mzee ni mmojawapo wa wachawi wakubwa hapa Tanzania (Mshana Jr. si ajabu analijua hili). Wakati akiwa mkuu wa mkoa Kigoma eti alikuwa anaingia ofisini alikuwa akirusha kofia yake inanasa hewani tu, hakuna cha gravity wala nini. Wanasema hata Zitto hamfikii huyu mzee pamoja na mikwara yake ya mara kwa mara kuwa ukijaribu kumchezea eti mtakufa ukoo wote mpaka na panya. Hao wachawi kama wamemsingizia basi wasubiri majibu...Kuishi Afrika raha sana!
 
Kifo kinaogopwa, vyeti makaratasi.

Japo kama hauna au vyeti vikipotea ndiyo utaelewa kuwa kuna baadhi ya makaratasi thamani yake siyo Sawa katika dunia.

Haaa haaa haaa haaaa.
 
Mkuu, kwa wanaoamini uchawi wanasema huyu mzee ni mmojawapo wa wachawi wakubwa hapa Tanzania (Mshana Jr. si ajabu analijua hili). Wakati akiwa mkuu wa mkoa Kigoma eti alikuwa anaingia ofisini anarusha kofia yake inanasa hewani tu, hakuna cha gravity wala nini. Wanasema hata Zitto hamfikii huyu mzee pamoja na mikwara yake ya mara kwa mara kuwa ukijaribu kumchezea eti mtakufa ukoo wote mpaka na panya. Hao wachawi kama wamemsingizia basi wasubiri majibu...Kuishi Afrika raha sana!
Ha ha ha haaaaaa Mshana ni gwiji na yule si mwenzetu yuko mbali sana,

Zito ni mzito km jina lake, hapana chezea yule jamaa, uchawi wake si wakuvuruga ila ukitaka kumvuruga utakupoteza kweli, kwa sababu hata me sipendi majaribio kwenye suala LA uhai, utapotea

Sina hakika huyu Mzee uchawi wake ni wakuvuruga au kujenga? Na hawa walomzushia kifo ni wachawi wakubwa wavurugaji ambao hawafai na dini zinawapinga na yeyote mpenda maendeleo anapinga uchawi wa aina hii
 
Zito ni mzito km jina lake, hapana chezea yule jamaa, uchawi wake si wakuvuruga ila ukitaka kumvuruga utakupoteza kweli, kwa sababu hata me sipendi majaribio kwenye suala LA uhai, utapotea
Hako kamjamaa ni hatareeeee,, ukitaka kujua ni jinsi gani kako balaa kamwulize Mudhihir Mudhihir yule jamaa wa Mchinga, aliacha mkono barabarani!! Sijui bado yuko hai kweli?
 
http://mobile.mwananchi.co.tz/Habar...597580-3888412-format-xhtml-mim708/index.html

Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, SK Chris Mzindakaya amesikitishwa na watu wanaovumishwa kwamba amefariki dunia na amewaita ni wapumbavu kabisa.

Akizungumza leo April 13 akiwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete,amesema afya imeimarika zaidi na ataruhusiwa kuondoka hospitalini wakati wowote.
Kwani kulikuwa na umuhimu wowote wa kutukana, si angesema tu anamkabidhi Mungu, sababu uhai ni kutoka kwa Mungu, lakini kama amepanic na kutukana hivyo basi afya yake bado ipo mashakani.
 
Back
Top Bottom