Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,169
Yulembunge machacha (enzi zake) wa Kwela, Chrisant Mzindakaya, ameitaka serikali kutoa kauli haraka iwezekanavyo kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Benjamin Mkapa.
Amesema leo Bungeni kuwa Mkapa anasakamwa wakati ni mtu si tu mwenye sifa katika anga za kimataifa, bali amelifanyia mambo makubwa taifa hili.
Ameshangazwa na wabunge ambao nao wamejiunga katika orodha ya watu wanaomsema vibaya rais huyo akisema kuwa wanajifedhehesha kwani hata ukumbi wa bunge ambamo wanakaa na kujadili mambo kadha umejengwa kutokana na juhudi za mkapa.