Miaka ya zamani kulikuwa na kozi zilikuwa zinatolewa na Eastern Block ikiongozwa na USSR zilizokuwa hata za miezi sita katika nyanja za propaganga, espionage na mambo ya siasa ambazo wengi wa wahitimu walipomaliza walijiita madokta. Lakini nahisi sio madokta wale wa kusoma kutibu au wa level ya Phd. Ni madokta wa mambo mambo kama wanayoyafanyasasa huo udaktari ni wa nini (wanyama, watu, falsafa, honoraria, au ni wakina [Maji marefu na Matunge]?). Manake sijaona kwenye andishi lako mahali alipotaja kupata chati cha huo udaktari!
Kuhusu maendelea yaliyotokea akiwa kiongozi ni machache mno. Shule 17 tu katika jimbo! Inanikumbusha miaka ya 90 ambapo K'njaro ilikuwa na sekondari karibia 100 ndani ya majimbo 6, sijui leo zitakuwa ngapi, manake kata nyingine zina shule hadi 6. Kiwango cha vijana wanaochaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni kidogo sana (27%) wakati mpango ni kuwa na zaidi ya 50% kwenda sekondary. Mwendo huu unaonyesha kuwa wananchi kwenye jimbo hili wameandaliwa kuendelea kuwa wakulima wadogo wadogo tu!
Ametaja barabara zilizojengwa, ila hakusema ni kwa kiwango gani, kwani hata wanavijiji hufanyia matengenezo barabara zao, lakini hazipitiki kwa muda wote!
Sijaona alipozungumzia suala la afya, maji, makazi ndani ya jimbo lake. Hivi ni viashiria vya maendeleo! Watu wanaweza kuwa wanavuna lakini wanaendelea kulala kwenye vibanda vya nyasi, kunywa kangara na kimpumu na kusubiri msimu mwingine wa kilimo ufike.
Miaka ya zamani kulikuwa na kozi zilikuwa zinatolewa na Eastern Block ikiongozwa na USSR zilizokuwa hata za miezi sita katika nyanja za propaganga, espionage na mambo ya siasa ambazo wengi wa wahitimu walipomaliza walijiita madokta. Lakini nahisi sio madokta wale wa kusoma kutibu au wa level ya Phd. Ni madokta wa mambo mambo kama wanayoyafanya
mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh! ndiyo maana siku hizi maana hana sumu tena kama alivyo kuwa zamani...Mzindakaya alifukuzwa Mzumbe kwa sababu alifoji, udaktari pia ni forgery. Miaka 44 hakuna cha maana. Sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa Mkapa baada ya kupewa bilion 9 za kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa
Ni kweli kuna mambo mengi ameyafanya mazuri na tunahitaji kuwa na watu wengi wa aina yake ndani ya mfumo wa utawala. Mfano alisaidia sana kubadili tabia za waluguru za kucheza ngoma toka juma tatu mpaka jumapili kwa kuwalazimisha kulima mashamba na kupiga marufuku ngoma hizo katikati ya wiki.Nasikia hata Kigoma alijitahidi sana kupigania kilimo. Lakini kinachojadiliwa hapa ni kweli yeye ni Dokta?I like Mzindakaya, he knows how to make things happen! Tangu 1965 hadi leo na huenda hata kesho, tunahitaji calibre ya watu kama hawa na wala siyo maneno-maneno.
Haya wasomi wekeni changamoto zenu nanyi hapa mme-achive nini tangu mlipomaliza shule hadi sasa?
Kumbe........Je, huyu Bwana Crisant Majiyatanga Mzindakaya hajawahi kuwa Waziri mdogo wa Uchukuzi hapo awali? Pengine hili lilitokea wakati akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara:
Mafaili ya TAKUKURU ya wakati huo yana kisa kwamba Bwana Crisant Majiyatanga Mzindakaya alichukua vifaa vya ujenzi wa nyumba yake na kuvisafirisha kwa lori la serikali kutoka Dar mpaka Sumbawanga! Wengine walitia hofu kuwa huenda baadhi ya vifaa hivyo vilikuwa ni mali ya serikali! Nyerere aliyajua hayo na baadaye kamtimua Bwana Crisant Majiyatanga Mzindakaya, mbali ya majambo yake mengine yasiyo ya ki-maadili!
Kama nakumbuka vizuri aliyekuwa mkuu wa baraza la Mzumbe alikuwa Marehemu Amon NsekelaAlizaliwa Desemba 31, 1940. Kati ya mwaka 1960-1961 alijiunga Sekondari ya Bugerere nchini Uganda na kupata elimu ya sekondari; mwaka 1964-1965 alikuwa Afisa Maendeleo Msaidizi Wilaya ya Sumbawanga na mwaka 1963-1964 alijiunga Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Arusha ambako alitunukiwa cheti.
Kutokana na 'kiu' ya kupata elimu, Dk Mzindakaya aliwahi kujiunga Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) hivi sasa Chuo Kikuu Mzumbe na kufukuzwa kwamba hakuwa na sifa.
Na deni hill bado Anadaiwa Kiwanda hakifanyi kaziMzindakaya alifukuzwa Mzumbe kwa sababu alifoji, udaktari pia ni forgery. Miaka 44 hakuna cha maana. Sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa Mkapa baada ya kupewa bilion 9 za kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa