Mzindakaya:Mbunge wa muda mrefu CV yake hii hapa

Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Messages
180
Points
195
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined Jul 3, 2009
180 195
Unapozungumzia wabunge walioko bungeni kwa muda mrefu, huwezi kumkwepa Mbunge wa Kwela (CCM), Dk Crisant Mzindakaya, ambaye aliingia mwaka 1965 katika mahojiano haya anaelezea mafaniko ya jimbo lake na jinsi Mkoa wa Rukwa ulivyoamua kujikita kwenye kilimo kama utambulisho wake.

Dk Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya mahakama kumvua ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 kwamba alitumia faulu.

Lakini mwaka 1982 alirejea bungeni kwa 'mgongo' mwingine baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati huo wakuu wa mikoa walikuwa wanaingia bungeni moja kwa moja.

Katika historia ya bunge, mbunge huyo hawezi kusahaulika, baada ya kujijengea umaarufu kama mzee wa mabomu wakati wa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya tatu, alipokuwa akifichua ufisadi mbalimbali ndani ya serikali.

Dk Mzindakaya atakumbukwa zaidi alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba, kutokana na kashfa ya sukari iliyosababisha waziri huyo kujiuzulu.

'Mabomu' mengine ambayo yalimjengea umaarufu zaidi ni pale alipomlipua aliyekuwa Waziri wa Fedha, Profesa Simon Mbilinyi na hatimaye kujiuzulu na kwenye kikao cha bunge kinachoendelea amerusha 'bomu la mkono' kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, ambalo madhara yake ni kidogo.

Hata hivyo, baada ya 'kulipua' wenzake kwa muda mrefu naye ameanza kugeukiwa akidaiwa kukipeshwa fedha kwa ajili ya kujengea kiwanda cha kusindika nyama mkoani Rukwa na kudhaminiwa na serikali ambazo hajarudisha.

Akizungumzia miaka 43 ya ubunge wake, Dk Mzindakaya anasema mafanikio yaliyopatikana ndani ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, hayajawahi kutokea kwenye awamu tatu za uongozi zilizopita na kwamba, maendeleo hayo yamegusa kila sekta.

Wakati Mkoa wa Rukwa unaanzishwa mwaka 1974, niliwaeleza watu kuwa maendeleo hayawezi kuja kwa pamoja, tutafute kitu ambazo kinaweza kuwa utambulisho wetu, nacho ni kilimo,” anasema na kuongeza.
“
Kwenye jimbo langu nilishauri tuanze na vijiji vya Karambazite, Kentula, Kozi, Songambele Azimio na Msanda Muungano, wakati huo jimbo la Kalambo lilikuwa halijatengwa tulianza na vijiji vya Kisungamile, Miunga, Kizombwe na Mwalocha na Wilaya ya Nkasi.

Anasema wakati wanaanzisha kilimo kama utambulisho wa mkoa, walianza kufundisha watu wachache ambao baada ya kuhitimu walifundisha wengine.


Tukachagua kilimo na wakati huo Rukwa tulikuwa tunashika nafasi ya 18 kitaifa kwa pato la mtu (GDP), hivi sasa tuko nafasi ya kumi,” anasema Dk Mzindakaya.

Kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2005 kwenye kilimo, Dk Mzindakaya anasema kazi ya kujenga vibanio mradi wa umwagiliaji Sakalilo imekamilika.

Anasema zaidi ya sh. milioni 4 zimeingizwa kwenye akaunti za vijiji vya Mue na Mnazi mmoja kwa ajili ya kuagiza mbegu za mianzi na michikichi, ambazo baadhi yake tayari zimeoteshwa.

Nasema zao lolote laweza kuwa la biashara, tulikuwa tunabishana na wachumi pale Morogoro kwa sababu, naamini ukiwa na chakula una nguvu zaidi hakuna wa kukutishia,” anasema Dk Mzindakaya na kuongeza.

Kwenye big four tuliingizwa na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1974, lakini hivi sasa tuko mbali zaidi na mwaka huu tunatarajia kuvuna tani milioni 1.6.”

Dk Mzindakaya anasema hivi sasa Rukwa hawahimizi watu kufanya kazi, bali wanachofanya ni kuwafundisha jinsi ya kuongeza kiwango cha uzalishaji mazao kwa heka na kwamba, huwezi kukuta vijana kutoka mkoa huo wakitembeza biashara mitaani, wanajishughulisha na kilimo na wanachohitaji ni kutafutiwa mikopo isiyo ya fedha bali zana za kilimo.

Anataja miradi ya umwagiliaji ambayo imeombewa fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Umwagiliaji wa Wilaya kuwa ni Sakalilo, Maleza, Lwanji, Msia, Ilembo na Nkwilo.

Kwa maoni yake, Dk Mzindakaya anasema anafikiri Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR) iruhusiwe kuuza chakula badala ya kubanwa kununua cha akiba peke yake.

Pia, Rukwa tusizuiwe kuuza chakula nje ya nchi ndio maana nasema zao lolote laweza kuwa la biashara, SGR wananunua kiwango kidogo, kingine ambacho ndio kikubwa kinabaki kwa wakulima hawaruhusiwi kuuza sehemu nyingine hali hii inawapa shida,” anasema.

Anasema mwaka huu, Mkoa wa Rukwa wanatarajia kuvuna tani milioni 1.6, lakini zitakazonunuliwa na SGR ni tani 49,000, huku kiwango kikubwa kikisalia mikononi mwa wakulima ambacho hawawezi kukimaliza kutumia kwa chakula.

Kuhusu sekta ya elimu, Dk Mzindakaya anasema takwimu za elimu Jimbo la Kwela zinaonyesha tangu mwaka 2007/09, wanafunzi wa shule za msingi wamefikia 10,560, huku matokeo ya wahitimu wa kufaulu wakiongezeka kutoka 1,521 mwaka 2007 hadi 2,845 mwaka jana, likiwa ongezeko la asilimia 21.

Upande wa sekondari, anasema jimbo lina shule 17, zikiwemo 15 za serikali na mashirika ya dini mbili na kukidhi mahitaji ya serikali ya kuwa na sekondari kila kata.

Anataja barabara zilizofanyiwa matengenezo kuwa ni Laela Kavifuti-Miangulua, Mpui-Ngoma, Kaengesa-Nankanga na Kasamvu-Ilemba, Miangulua-Mkowe-Chombe, Chombe-Kipeta na Miangulua-Movu.

Zingine ni Mshani-Mlombo, Kaengesa-Sandulula, Chome-Kaoze, Mpui-Msoma na Miangulua-Mkowe-Chombe.

Kuhusu sekta ya ufugaji, Dk Mzindakaya anasema tayari sh3,840,468 zimeingizwa kwenye akaunti ya mradi wa Ujenzi wa Machinjio Laela kwa ajili ya mradi wa machinjio na maandalizi ya mikataba midogo inafanyika na ujenzi utaanza hivi karibuni.

Dk Mzindakaya anataja miradi mingine inayoendelea kuwa ni ukarabati wa josho Kaengesa, nyumba ya mtumishi wa mifugo Kipeta, uchanjaji mifugo dhidi ya homa ya mapafu, chanjo ya kuku na mashamba darasa kuhusu ufugaji nguruwe.

Kutokana na wito wa taifa na sera ya chama kuwa viongozi wawe mfano wa kuigwa, kama mbunge niliahidi nitashirikiana kuendeleza kilimo na ufugaji. Kwa sasa tuna shamba la ngano na mahindi kwa pamoja zaidi ya ekari 250,” anasema mbunge huyo na kuongeza:

Tunaendeleza ufugaji mifugo ya kisasa kwa kuzalisha na kunenepesha mifugo kwenye Ranchi ya Nkundi.

Kuhusu vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (Saccos), Dk Mzindakaya anasema tayari vyama 13 vimeanzishwa Jimbo la Kwela na kukopeshwa fedha kutoka asasi mbalimbali ili kuongeza mtaji.

Anasema fedha hizo zimetoka Sccult (T) Ltd sh92,190,000 na Pride (T) Ltd sh. milioni 10.

Matarajio ya siasa

Dk Mzindakaya anasema hajaamua kuwania tena ubunge wa jimbo hilo au la! Kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Sijaamua kusimama au kutosimama, isitoshe jimbo langu nina nguvu hatuna vurugu za kisiasa. Mungu akinifikisha mwakani nitatimiza miaka 44 bungeni,” anasema mbunge huyo.

Anasema aliingia bungeni mwaka 1965, lakini mtiririko wa ubunge wake wa kuchaguliwa ulitiwa doa na mpinzani wake mwaka 1981 baada ya kulalamikia ushindi wake kuwa haukuwa halali na kukubaliwa na mahakama.

Mwaka 1981 ilitokea kesi ya kupinga ushindi wangu kwenye uchaguzi wa mwaka 1980, mpizani wangu alilalamika kuwa sikumshinda kwa haki nikapoteza ubunge, lakini mwaka 1982 nikateuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati ule mkuu wa mkoa moja kwa moja ulikuwa unakuwa mbunge,” anasema.

Mbunge huyo anasema mwaka 1993 alihamishwa kutoka Kigoma kwenda Mkoa wa Rukwa, lakini mwaka 1995 wazee walimfuata kumuomba kugombea ubunge suala ambalo aliona linafaa kwa sababu, alishahamisha vyombo vyake na utakuwa usumbufu kuvihamisha tena.

Nikamwandikia barua Rais Ali Hassan Mwinyi kumuomba niache ukuu wa mkoa ili nigombee ubunge, alinikubalia kwa sharti moja kwamba niendelee kushikilia wadhifa huo, atakubali niache iwapo nitashinda lakini nikishindwa nitaendelea kuwa RC,” anaongeza Dk Mzindakaya.

Katika uongozi wake, ameshakuwa mbunge wa Sumbawanga Mjini, Nkasi na hata Kalambo ya sasa wakati ule ikiwa Sumbawanga Vijijini. Pia, amekuwa mkuu wa mkoa kwa miaka 13, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kwa miaka tisa na Mwenyekiti wa kwanza wa bodi ya Shirika la Viwanda Vidogo (Sido).

Alizaliwa Desemba 31, 1940. Kati ya mwaka 1960-1961 alijiunga Sekondari ya Bugerere nchini Uganda na kupata elimu ya sekondari; mwaka 1964-1965 alikuwa Afisa Maendeleo Msaidizi Wilaya ya Sumbawanga na mwaka 1963-1964 alijiunga Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Arusha ambako alitunukiwa cheti.[

Kutokana na 'kiu' ya kupata elimu, Dk Mzindakaya aliwahi kujiunga Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) hivi sasa Chuo Kikuu Mzumbe na kufukuzwa kwamba hakuwa na sifa.


Mwaka 1973-1975 alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Biashara ya Ndani (BIT) na 1973-1987 alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwanda Vodogo (Sido); Mwaka 1969-1975 alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Tanu; mwaka 1965-1981 alikuwa mbunge wa kuchaguliwa Jimbo la Ufipa Kusini.

Mwaka 1992 alikwenda Dublin, Ireland kuchukua mafunzo ya utawala na mipango ya maendeleo na kutunukiwa cheti.

Kati ya mwaka 1973 na 1981, alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na kati ya mwaka 1982-1995 alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Morogoro, Kigoma na Rukwa.

Mwaka 1990-1992 alikuwa Katibu wa CCM mkoa; mwaka 1990-1997 alikuwa alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM; mwaka 2002 hadi sasa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa na mwaka 1995-hadi sasa ni mbunge wa kuchaguliwa.

Source: Nipashe
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,499
Points
2,000
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,499 2,000
Duu ana uzoefu mkubwa sana ila mm dr sasa imekuwaje??amesomae wapi maana kila sehemu alioenda alipata cert tu sasa kuwa dr amefikaje??anyway amesota sana kwenye siasa ya tanzania
 
M

Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
1,325
Points
0
M

Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
1,325 0
Kwa ubunge ni kweli amebobea. Miaka 44 ni mingi sana. Ila ni kwa vigezo gani amekuwa na hiyo title ya 'Dr'. Hapo ndipo swali linapokuja. Ni muda sasa nimesikia akitambulishwa kama Dr. Nimeangalia lakini sijaona popote waliposema amebobea kwenye fani fulani mpaka akapata hiyo title. Tueleweshane jamani.
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,379
Points
1,250
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,379 1,250
sasa huo udaktari ni wa nini (wanyama, watu, falsafa, honoraria, au ni wakina [Maji marefu na Matunge]?). Manake sijaona kwenye andishi lako mahali alipotaja kupata chati cha huo udaktari!

Kuhusu maendelea yaliyotokea akiwa kiongozi ni machache mno. Shule 17 tu katika jimbo! Inanikumbusha miaka ya 90 ambapo K'njaro ilikuwa na sekondari karibia 100 ndani ya majimbo 6, sijui leo zitakuwa ngapi, manake kata nyingine zina shule hadi 6. Kiwango cha vijana wanaochaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni kidogo sana (27%) wakati mpango ni kuwa na zaidi ya 50% kwenda sekondary. Mwendo huu unaonyesha kuwa wananchi kwenye jimbo hili wameandaliwa kuendelea kuwa wakulima wadogo wadogo tu!

Ametaja barabara zilizojengwa, ila hakusema ni kwa kiwango gani, kwani hata wanavijiji hufanyia matengenezo barabara zao, lakini hazipitiki kwa muda wote!

Sijaona alipozungumzia suala la afya, maji, makazi ndani ya jimbo lake. Hivi ni viashiria vya maendeleo! Watu wanaweza kuwa wanavuna lakini wanaendelea kulala kwenye vibanda vya nyasi, kunywa kangara na kimpumu na kusubiri msimu mwingine wa kilimo ufike.
 
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Messages
180
Points
195
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined Jul 3, 2009
180 195
Mzindakaya alifukuzwa Mzumbe kwa sababu alifoji, udaktari pia ni forgery. Miaka 44 hakuna cha maana. Sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa Mkapa baada ya kupewa bilion 9 za kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa
 
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Messages
180
Points
195
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined Jul 3, 2009
180 195
Mzindakaya alifukuzwa Mzumbe kwa sababu alifoji, udaktari pia ni forgery. Miaka 44 hakuna cha maana. Sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa Mkapa baada ya kupewa bilion 9 za kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa
 
K

Kagoma

Member
Joined
May 21, 2009
Messages
29
Points
20
K

Kagoma

Member
Joined May 21, 2009
29 20
It is also a surprise to me and probably to everyone....Dr kapewa na nani na kwa lipi? Huyu ni kilaza tu as far as Academics is concerned.
 
S

Son of Alaska

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2008
Messages
2,813
Points
0
S

Son of Alaska

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2008
2,813 0
sasa kwanini alifukuzwa mzumbe? ukiwa na elimu ya sekondari si unaqualify na yeye si kasoma sec uganda au maneno ya mtaani kwamba yeye kwa proffession alikuwa ni utingo wa bus ni kweli?
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,552
Points
2,000
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,552 2,000
Mzindakaya alifukuzwa Mzumbe kwa sababu alifoji, udaktari pia ni forgery. Miaka 44 hakuna cha maana. Sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa Mkapa baada ya kupewa bilion 9 za kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa
clarify please
 
M

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Messages
2,534
Points
1,225
M

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined May 8, 2008
2,534 1,225
Ashauriwe apumzike 2010 ili akasimamie kiwanda chake cha nyama.
 
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,622
Points
1,225
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,622 1,225
Huyu ana elimu ya kilaza hana la maan aalilofanya zaidi ya kusifiwa kwneye usangoma.

Dactari wa mitishamba! mtu gani miaka yote hatoki jimboni kwake unafikiri wana jimboa wanampenda kiasi hicho na ndumbanangai zimo.

Msiumize vichwa, hana ellimu huyo!
 
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Messages
180
Points
195
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined Jul 3, 2009
180 195
Huyu ana elimu ya kilaza hana la maan aalilofanya zaidi ya kusifiwa kwneye usangoma.

Dactari wa mitishamba! mtu gani miaka yote hatoki jimboni kwake unafikiri wana jimboa wanampenda kiasi hicho na ndumbanangai zimo.

Msiumize vichwa, hana ellimu huyo!
umelewa hii direct quote ya Mzindakaya "isitoshe jimbo langu nina nguvu hatuna vurugu za kisiasa. "
 
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Messages
180
Points
195
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined Jul 3, 2009
180 195
clarify please

Alizaliwa Desemba 31, 1940. Kati ya mwaka 1960-1961 alijiunga Sekondari ya Bugerere nchini Uganda na kupata elimu ya sekondari; mwaka 1964-1965 alikuwa Afisa Maendeleo Msaidizi Wilaya ya Sumbawanga na mwaka 1963-1964 alijiunga Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Arusha ambako alitunukiwa cheti.
Kutokana na 'kiu' ya kupata elimu, Dk Mzindakaya aliwahi kujiunga Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) hivi sasa Chuo Kikuu Mzumbe na kufukuzwa kwamba hakuwa na sifa.
 
G

Gagnija

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2006
Messages
7,279
Points
2,000
G

Gagnija

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2006
7,279 2,000
Mzindakaya akiwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, alitaka kutumia cheo chake apate admission ya chuo bila kuwa na sifa za kusoma advanced diploma, chuo kikamkatalia. Huyu bwana ana kiu sana ya kupata vyeti na si elimu!
 
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Messages
180
Points
195
Lengeri

Lengeri

Senior Member
Joined Jul 3, 2009
180 195
Mzindakaya akiwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, alitaka kutumia cheo chake apate admission ya chuo bila kuwa na sifa za kusoma advanced diploma, chuo kikamkatalia. Huyu bwana ana kiu sana ya kupata vyeti na si elimu!
hata wanawe kina Vicky, David Jackline ni Form four failures
 
S

Son of Alaska

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2008
Messages
2,813
Points
0
S

Son of Alaska

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2008
2,813 0
Mzindakaya akiwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, alitaka kutumia cheo chake apate admission ya chuo bila kuwa na sifa za kusoma advanced diploma, chuo kikamkatalia. Huyu bwana ana kiu sana ya kupata vyeti na si elimu!
kumbe application yake ilikataliwa,i thought alifukuzwa chuo
 
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,968
Points
1,225
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,968 1,225
Hivi kaanza lini Elimu yake na alihitimu lini?
 
M

MzeePunch

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2009
Messages
1,413
Points
1,195
M

MzeePunch

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2009
1,413 1,195
Ni mtu wa kutumiwa tu huyo kutokana na kuwa na elimu ndogo. Sasa hivi ana tender ya kumtetea Mkapa.
 
Masanilo

Masanilo

Platinum Member
Joined
Oct 2, 2007
Messages
22,296
Points
1,250
Masanilo

Masanilo

Platinum Member
Joined Oct 2, 2007
22,296 1,250
Duu ana uzoefu mkubwa sana ila mm dr sasa imekuwaje??amesomae wapi maana kila sehemu alioenda alipata cert tu sasa kuwa dr amefikaje??anyway amesota sana kwenye siasa ya tanzania
Jamani huo ni Udr wa CCM mbona hamhoji wa Kamala, Mary Nagu, Makongoro Mahanga, Matayo David Msuya, Nchimbi Emmanuel?
 
I

Idda

Member
Joined
May 22, 2009
Messages
64
Points
0
I

Idda

Member
Joined May 22, 2009
64 0
Mzindakaya alifukuzwa Mzumbe kwa sababu alifoji, udaktari pia ni forgery. Miaka 44 hakuna cha maana. Sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa Mkapa baada ya kupewa bilion 9 za kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa
Kweli Lengeri?
 

Forum statistics

Threads 1,335,156
Members 512,245
Posts 32,497,406
Top