Mzindakaya, Kimiti na Keenja watangaza kutogombea tena

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Nimeonna TBC News Saa Mbili usiku huu, wabunge wakongwe wawili, Christant Mzindakaya, (Mzee wa Kupasua Mabomu) na Paul Kimiti, wametangaza kutogombea majimbo yao uchaguzi mkuu ujao.

Wametangaza nia yao hiyo mbele ya PM-Pinda, na kueleza sababu ni kuwapisha vijana.

Wamesema ni vizuri ukaondoka kwenye uongozi wakati bado unapendwa na huku unanguvu zako na sio kusubiri mpaka uchoke hadi watu wako wakuchoke!.

Haya, hawa wazee wawili wameonyesha njia, wezee wengine waliobaki jee wanasubiri nini?

Ushauri wa bure kwa wazee hawa wafuatao. (Wataje).... wakiongozwa na Mheshimiwa sana Mzee......

Tangazeni nia zenu, mmeshajichokea sasa msisubiri mpaka mchokwe!
 
........Ni kweli kabisa wapishe vijana, hongera Mzindakaya na Kimiti.
Vijana nafasi hizo tuchangamkie.
 
makweta jamani makweta atuitaji atufie bungeni huyu babu nae loh
toka mdogo waziri waelimu ni.........makweta
awachoki kunanini bungeni huko tuachieni tuingie??
 
Ni uamzi mzuri. Hata wale wakuteuliwa kama Kingunge watangaze kwamba hawatakubali viti vya kuteuliwa tena, WAMEZEEKA!
 
Makweta, Ngombare mwiru, Malecela et al, wanasubiri nini?

Kwa muono wangu mitizamo kama hii inaashiria kuwa wengi tumegubikwa na hulka za ubaguzi wa kirika na jinsi gani tunapenda kutumia kauli mbiu ya UJANA kama nyenzo ya kuhalalisha uroho wetu wa UHESHIMIWA.


omarilyas
 
Cheyo wa Ileje, mimi nikiwa primary school alikuwa katibu mkuu wa wizara ya Afya enzi ya Kambarage!! Inaelekea bado anautaka Ubunge!!Watu wa sampuli hii ndio wanataka wafie bungeni maiti zao zipelekwe kwa Ndege.!!
 
- Ungetegemea baada ya yote yaliyotukuta as a nation tutakua tumeamka, hivi Lowassa, Kikwete, na Rostam, Masha, Ngereja, Nchimbi na the likes ujana wao umetusaidia nini taifa kwa miaka mitano iliyopita?

- Binafsi siwezi ku-endorse ideas za kuwanyma uongozi kina Butiku na Quaresi, ambao ni wazee na sio siri tunawahitaji zaidi sasa hivi kuliko anytime in the past! na kuliko vijana wote combained tulionao kwenye madaraka ya taifa! Uchaguzi wa rais uliopita tuliambwia haya haya na sasa bado tena yale yale,

- Rostam na umri wake mdogo ametufanyia nini wanachi na taifa hili? Sometimes tunakuwa kama tumelogwa hili taifa!

Respect.


FMEs!
 
Mimi nitakunywa kinywaji Murua nikiona Lipumba na Maalimu Seif hawagombei tena!

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Wengine Prof. Raphael Mwalyosi, Prof. Idris Mtulia na Maprofesa wengi tu waliojazana kwenye bunge wanafaa nao waachane na siasa wamekuwa wazee na waende wakafundishe vyuo vikuu huko ujuzu hauzeheki....
 
Huyu siyo Marhum jamani?, hebu nirekebisheni kumbukumbu zangu.

Ni kweli Mzee Sanga alikwishafariki...sielewi kwa nini huyu jamaa "Mende dume" ameweka jina la mtu aliyekwishatangulia kwenye haki!

Kuna fununu kuwa Mzee Bakari Mwapachu (Tanga mjini) pia nae anastaafu!
 
Tatizo la uongozi wa Tanzania siyo umri, elimu, wala rangi na jinsia; tatizo ni uwezo. You can quote me.
 
Itakuwa vizuri wote waliokula chumvi nyingi washinikizwe kung'atuka. Mrema alias Nyau wa Kikwete naye anasubiri nini?
 
Kwa muono wangu mitizamo kama hii inaashiria kuwa wengi tumegubikwa na hulka za ubaguzi wa kirika na jinsi gani tunapenda kutumia kauli mbiu ya UJANA kama nyenzo ya kuhalalisha uroho wetu wa UHESHIMIWA.


omarilyas
Inawezekana juu ya muono wako. Hebu leo tuorodheshe wazee woote wamefanya nini tokea uhuru? Au unadhani bado wanauwezo wa kufanya km hawakuwahi kufanya? wanaziweza mbio za teknolojia kuleta maendeleo. Nadhani list itapendeza wakitupisha wale mafisadi na wazee hao. Hata kina Qares waliwagi kufanya nini? Butiku? Warioba?? wengine walikuwa mawaziri wakuu, wanakumbukumbu gani ambayo tutawakumbuka???
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom