Mzindakaya, Kimiti na Keenja watangaza kutogombea tena

Code:
Nimeonna TBC News Saa Mbili usiku huu, wabunge wakongwe wawili, Christant Mzindakaya, (Mzee wa Kupasua Mabomu) na Paul Kimiti, wametangaza kutogombea majimbo yao uchaguzi mkuu ujao.

Wametangaza nia yao hiyo mbele ya PM-Pinda, na kueleza sababu ni kuwapisha vijana.

Wamesema ni vizuri ukaondoka kwenye uongozi wakati bado unapendwa na huku unanguvu zako na sio kusubiri mpaka uchoke hadi watu wako wakuchoke!.

Haya, hawa wazee wawili wameonyesha njia, wezee wengine waliobaki jee wanasubiri nini?

Ushauri wa bure kwa wazee hawa wafuatao. (Wataje).... wakiongozwa na Mheshimiwa sana Mzee......

Tangazeni nia zenu, mmeshajichokea sasa msisubiri mpaka mchokwe!
Code:
Muungwana alishasema wazee wote watoke nduki kwenye siasa.

Namsubiri mzee Sitta na Mungai manake wote wawili wanacheza kwenye sabini na kitu hivi kwa umri!
 
Tatizo la uongozi wa Tanzania siyo umri, elimu, wala rangi na jinsi; tatizo ni uwezo. You can quote me.
Mzee Mwanakijiji, Nakuunga mkono kwa asilimia 100% kuwa ' Age an't nothing but a number!', ila pia lazima tufike mahali tukubali baadhi ya hawa Wazee wetu ni 'spent force' they were good, bright and brilliant but now they are only left with 'ukubwa dawa', nothing more to offer. Pia tuweke standard performance ya wabunge wetu, ili ikifikia mahali kuna mbunge, sio waziri, hajawahi kuuliza swali lolote bungeni, hawajawahi changia mjadala wowote bungeni, fukuzia mbali, maana he/she is good for nothing.
 
Mchezo mzima wa 'ubunge' ni kucheza na PR na spin tu,, na wanakula na kulala bure kwa pesa za walipa kodi. Kwa kifupi hatuwahitaji wabunge wala wanasiasa.
 
badala ya "vijana" kungojea "wazee" wang'atuke kwanini wasijitokeze
kwenda kugombea ili wawapige mweleka hao wazee? au ndi ile ile hulka ya kupenda dezo?

inatakiwa vijana wajinadi ni nini watafanya tofauti na "wazee" ili nhi iweze kusonga mbele. hakika kwa hesabu za harakaharaka vijana wanaweza kutumia wingi wao kuwang'oa hao wazee. lakini ukweli ni kwamba vijana hao hao ndio wamewapigia kura hao "wazee".
 
Dah jamaa ameshikilia jimbo tangu enzi zile naanza form one pale Ifunda
mpaka sasa..!!!??? halafi hata asikiki kabisa yaani kama hayupo
Bongo kweli kazi ipo

enzi zile zipi? ninavyofahamu galinoma alikuwa mbunge
kipindi kimoja, kisha uchaguzi uliofuata akapigwa mweleka
na aliyekuwa katibu wa bunge (jina limenitoka) na amerudi bungeni
2005. (kama nimekosea nisahihishwe)
 
Alikuwa George Mlawa kama sikosei
 
Makweta, Ngombare mwiru, Malecela et al, wanasubiri nini?

Eh George Wassira nimemsikia tokea enzi za TANU yajenga nchi jamani hawa wazee wamegeuza ubunge kama uchifu lakini nao vijana ndio hao akina Ngereja,Masha sasa sijui tubaki na wazee au vijana
 
Eh George Wassira nimemsikia tokea enzi za TANU yajenga nchi jamani hawa wazee wamegeuza ubunge kama uchifu lakini nao vijana ndio hao akina Ngereja,Masha sasa sijui tubaki na wazee au vijana

Hope unamzungumzia Steven Wassira mkuu
 
enzi zile zipi? ninavyofahamu galinoma alikuwa mbunge
kipindi kimoja, kisha uchaguzi uliofuata akapigwa mweleka
na aliyekuwa katibu wa bunge (jina limenitoka) na amerudi bungeni
2005. (kama nimekosea nisahihishwe)
Ni George Mlawa na kabla yake huko nyuma ndiyo Galinoma, Mpakani (RIP) nk. Lakini hukumuuliza lini alikuwa form one. Inawezekan 2005
 
Ni George Mlawa na kabla yake huko nyuma ndiyo Galinoma, Mpakani (RIP) nk. Lakini hukumuuliza lini alikuwa form one. Inawezekan 2005

ndio maana nimeuliza "enzi zile zipi?". naamini mzee galinoma
amekuwa mbunge jumla ya vipindi viwili. muda mrefu unajumuisha
wakati galinoma akiwa katibu mkuu ulinzi.
 
Nimeonna TBC News Saa Mbili usiku huu, wabunge wakongwe wawili, Christant Mzindakaya, (Mzee wa Kupasua Mabomu) na Paul Kimiti, wametangaza kutogombea majimbo yao uchaguzi mkuu ujao.

Wametangaza nia yao hiyo mbele ya PM-Pinda, na kueleza sababu ni kuwapisha vijana.

Wamesema ni vizuri ukaondoka kwenye uongozi wakati bado unapendwa na huku unanguvu zako na sio kusubiri mpaka uchoke hadi watu wako wakuchoke!.

Haya, hawa wazee wawili wameonyesha njia, wezee wengine waliobaki jee wanasubiri nini?

Ushauri wa bure kwa wazee hawa wafuatao. (Wataje).... wakiongozwa na Mheshimiwa sana Mzee......

Tangazeni nia zenu, mmeshajichokea sasa msisubiri mpaka mchokwe!

Walishachelewa sana; wote wamekuwa kwenye siasa tangu miaka ya sitini chini ya Kambarage na Kawawa ambao waliacha shughuli hizo zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Tanzania inabidi tuwe na term limit za miaka minane minane katika elected offices zote yaani udiwani, ubunge, na urais.
 
Je, mnaoshabikia kung'atuka kwa wazee, mna hakika gani kuwa hawawaandai watoto wao kuwarithi. Kumbukeni mtoto wa nyoka ni nyoka tu tena wakati mwingine ndio mkali zaidi kwani ana ari, kasi na nguvu mpya. Ninavyoijua CCM hawa pamoja na kung'atuka ndio watabakia eti wazee wa busara wa CCM na watakuwa na influence kubwa katika teuzi mbali mbali za wagombea wa CCM - kwanza pesa wanazo na pesa ndio hivyo tena, rushwa mbele kwa mbele.
 
Tena vijana ndio hatari zaidi , maana karibu vijana wote walio ingia kwenye siasa wali ingia kwa kudhani JK ni mtu wao so madili nje nje . Ni uadilifu tuu , kuwapisha vijana sio jibu, vijana ndio tumelelewa kwnye mazingira ya rushwa njenje so sidhani kama kutakua na tofauti sana.
 
nawaunga mkono sana hawa wazee na wamefanya jambo la busara sana, ila wajue bado wana kazi ya kuhakikisha kuwa wanaandaa watu wenye uwezo wa kufanya yale yote mazuri walioyaacha.

hao wazee wengine na mafisadi waliobaki nadhani wameona njia ya kufuata sasa wasingoje mpaka kura ya maoni.
 
Haleluya bwana asifiwe!! zile njozi zetu zinaanza kutimilika tarrritiiiiiiiiiibu!! Tutafika tu safari ni hatua
 
Makweta, Ngombare mwiru, Malecela et al, wanasubiri nini?

Kingunge Mwiru kaacha kugombea longtime,wa kumlaumu kwa Kingunge kuwepo mjengoni ni Rais JK aliyemteua kuwa mbunge na baadae kumpa uwaziri kabla kikongwe huyu hajaamua kukaa pembeni!
 
Back
Top Bottom