Mzindakaya ana maslahi Binafsi kwenye uwindaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzindakaya ana maslahi Binafsi kwenye uwindaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, May 24, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  MWANASIASA maarufu na Mbunge mstaafu wa Kwela (CCM), Dk Chrisant Mzindakaya, ameiponda Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, kuwa inaingilia kazi za Serikali katika ugawaji vitalu vya uwindaji. Dk Mzindakaya alisema mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo kwenye kikao kilichopita na baadaye kupitishwa kama maazimio, kuwa zoezi la ugawaji vitalu vya uwindaji utangazwe upya kwa kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma ni kinyume na sheria.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Mzindakaya alisema sheria namba 5 ya mwaka 2009, inaeleza wazi uwiano wa ugawaji vitalu ambao asilimia 85 ni wazalendo na asilimia 15 ni wageni. “Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wanataka kampuni zaidi za kigeni zipate vitalu vya uwindaji iwapo ugawaji huo utarudiwa wakati sheria inaeleza wazi,” alisema Dk Mzindakaya.

  Alisema wajumbe hao wa kamati mchana wanatetea wazalendo kupewa upendeleo, wakati huohuo wanataka kuzipendelea kampuni za kigeni ili zipate vitalu zaidi.

  Lakini, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Utalii, James Lembeli na makamu wake, Abdulkarim Shaha, walipopigiwa simu kwa nyakati tofauti kuzungumzia suala hilo hawakupatikana.

  Dk Mzindakaya alisema kampuni kubwa za kigeni zinahangaika huku na kule kuhakikisha zinapewa fursa kubwa ya kupata vitalu zaidi ya asilimia 15 iliyopo katika sheria. Alisema Bunge halina mamlaka ya kutengua uamuzi wa waziri pale anapotekeleza sheria: “Vitalu vimekwishagawiwa kwa wazalendo walio wengi uamuzi wa waziri usitenguliwe.”

  Uwindaji wa kitalii upigwe marufuku

  Dk Mzindakaya alishauri Serikali itunge sheria kuzuia uwindaji wa kitalii kwa kuwa eneo hilo ndilo kichaka cha walarushwa na kwamba, iboreshe vyanzo vingine vya mapato kama utalii wa picha.

  “Lawama nyingi zinazotokea kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii ni kutokana na biashara ya uwindaji wa kitalii, tuzuie kwa kuwa haliongezi pato kubwa la Serikali,” alisema.

  Alisema Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zimezuia uwindaji wa kitalii na wanaingiza mapato kwa utalii wa picha. Dk Mzindakaya alisema athari za uwindaji wa kitalii ni kubwa zikiwamo kuuawa kwa wanyama.

  My take

  Waswahili wanasema ukiona umerusha jiwe gizani halafu ukaskia mtu anatoa mlio, basi jua huyo limempata. Jana Mzindakaya alitoa mlio na kutokwa povu kwa kutoa kauli inayopingana na maazimio ya Bunge juu ya suala la kubatilisha na kuamuru zoezi zima la ugawaji wa vitalu kurudiwa upya. Kauli ya Mzindakaya ingekuwa na mashiko iwapo tu yeye asingekuwa mnufaika na mmiliki wa Vitalu. Anachokifanya sasa hivi ni kutetea maslahi yake binafsi na sio maslahi ya Taifa.

  Kamati ya Bunge ilielezea vizuri sana na kwa uwazi mkubwa ni wapi kamati ya kugawa vitalu haikuwa fair na wapi kulikuwa na dalili za nepotism na harufu ya ufisadi . Tulielezwa, kamati ya kugawa vitalu iligawa vitalu kwa kampuni ambazo hazikuomba vitalu na kuwaacha walioomba. Aidha, kamati ya Bunge iliainisha kampuni ambazo zilipewa vitalu huku records zao za utendaji zinaonesha wanarecord mbaya ya kutolipa kodi, ada mbalimbali pamoja na utendaji mbovu kwa ujumla. Moja ya kampuni hizo ni ile inayomilikiwa na familia ya Kawawa. Napata shida kuelewa kama Mzindakaya aliisoma na kuielewa ripoti ya kamati ya bunge, na kama ameisoma sielewi ni wap haelewi na kama ameielewa iweje kaja na argument ya kibabaishaji.

  Ni kweli sheria ya wanyamapori namba 5 ya 2009 imeweka bayana kuwa asilimia 85 ya vitalu wapewe wazawa. Lakini asisahau kuwa sheria ile haikusema asilimia ya 85 ya vitalu wapewe wajumbe wa NEC-CCM, Wabunge, watoto wa viongozi wastaafu na ndugu zao. Aidha, sheria ile ya wanyamapori haikusema pia kuwa wakati wa utekelezaji wake sheria nyingine za nchi kama ya manunuzi ya umma n.k zivunjwe. Mzindakaya anapaswa kufahamu kuwa Tanzania ina wananchi takriban 40 Milioni. Na wananchi hawa wote wana haki sawa ya kumiliki rasilimali zilizopo. Hivyo, lazima kuwepo na mfumo uliowazi na unaojali haki ya kila mwananchi bila kuangalia cheo au chama chake au nafasi yake kwenye jamii. Nakushauri mzee wangu uwe mpole maana inaonyesha ulipewa vitalu kimagumashi ndo mana unaogopa zoezi la ugawaji likirudiwa huenda hutopewa.

  Lakini pia sipati picha kwa nini kwenye wanyamapori serikali inataka wazawa wamiliki 85% ya vitalu vyote, ila inapofika kwenye madini wazawa hawasikilizwi wala kuthaminiwa. Hapa lazma kuna siri kubwa ndani yake. Si ajabu wazawa hawa wanaotetewa kwenye kumiliki vitalu vya uwindaji ni wa koo za kina Aloyce Kimaro, Kawawa, Mkapa, Mzindakaya, Sokoine, Meghji, you name it. Hii si sawa hata kidogo, mbaya zaidi makampuni yenu ndo yanaongoza kwa ubabaishaji na huduma duni na ndio wengi wenu mnaishia kuwakodisha vitalu wazungu hao hao ambao sheria inataka wapewe 15% tu ya vitalu vyote, sasa hapa zana nzima ya wazawa kwanza ipo wap km sio kurubuni wananchi????Mnatoa povu mpewe vitalu, mkishapewa kesho yake mnawauzia/kuwakodisha wazungu vitalu hivyo ili warun business ya uwindaji. Sasa kama hamuwezi hiyo business mnaombaga vitalu vya nini kama sio ubabaishaji???

  Mwisho, naunga mkono hoja ya kamati teule ya Bunge ya Maliasili.


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [/TABLE]
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na dhana ya kupigwa marufuku uwindaji wa kitalii. Lakini kitu ambacho sijaelewa, unataka wageni waongezewe vitalu?
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  naona fisadi mzindakaya yuko sahihi atleast kwa hili..namsihi arudishe maji ya wanakijiji aliyojimilikisha kunywesha ng'ombe wake wakati watu wanakosa maji ya kunywa!
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  hivi vikongwe fisadi mzindakaya na kingunge nikipewa ruhusa tuu dakika moja tu nawabadilisha wanakuwa RIP kwa kipigo.
   
 5. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Nae ana kakampuni nn?
   
 6. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kupigwa marufuku uwindaji wa kitalii kama alivyoshauri Mzindakaya sio suluhisho la kuinyanyua tasnia ya uwindaji na wala hakuna faida yoyote zaidi ya hasara. Kuna a lot of technical flaws in the industry worth to be addressed first kabla ya kufkiria kuifunga na kusema hailipi kiuchumi. Industry haiwezi kulipa kama waliopewa hawana uwezo wa kuiendesha, kama wanafanya watakavyo wao sababu ya majina yao au kama hawalipi kodi na mapato serikalini.

  Kama tulivyoacha huru sekta nyingine kama madini na kwingineko, huku pia ilipaswa tuache huru ili waombaji wapimwe kwa uwezo wao na sio kwa utaifa wao na nani anamjua nani au wa nafasi za waombaji serikalini kama ilivyo sasa, mfumo huu wa sasa utaendelea kufurahiwa na familia za wakubwa na viongozi na sio kulifaidisha taifa. Sisemi wapewe wazungu, ila nasema lazma tuhakikishe wanaopewa wamepimwa kwa kigezo cha uwezo wao na sio kufanya mambo ya kibabaishaji. Ikumbukwe kuwa siku ya mwisho sisi kama taifa tutahitaji mapato na sio blah blah na siasa. Wenzetu walioendelea mto yeyote anapewa fursa kama hizo as long as anauwezo wa kuifanya biashara hiyo kwa kulifaidisha taifa. Sisi nchi maskini ndo tunafanya mambo kienyeji yanayoishia kutudidimiza zaidi badala ya kutuendeleza.

  Hizo 85% tunazotaka wazawa wamilikishwe haziwezi zikatufanya wote kama taifa tulidhike. Sisi tunachohitaji ni mapato ili nchi yetu iendelezwe na si vinginevyo.
   
 7. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Naye pia ni mhanga wa hilo zoezi ndo mana ametoa mlio.
   
 8. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Yupo wrong, hajaweka maslahi ya taifa mbele. yeye anataka uyeye kwanza. Kamati haikusema vitalu vikibatilishwa watapewa wageni. walichosema ni zoezi zima limegubikwa na wingu la nepotism na ufisadi. Mzindakaya aliyapata wapi haya ya kusema kuwa kamati inataka kuwapa vitalu hivyo wageni????Hapa Mzindakaya anatafuta huruma ya Taifa ili tumsaidie kumnufaisha yeye km yeye. Zoezi hilo ni kweli halijatendea haki wazawa walio wengi na hivyo sharti lirudiwe ili wanaopata au kukosa wakose/wapate kwa haki.
   
 9. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  maige mwizi, mzindakaya mwizi, kwenye hilo zoezi la kugawa vitalu hao wanaoitwa wazawa ni uongo mtupu ni madalali wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa kigoma ndio wameunda vikampuni vya ovyo ovyo wakapewa vitalu na badala yake sasa biashara imedoda, Kamati ya bunge ilifanya kazi nzuri ya kumuumbua maige
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mzindakaya yupo right, kama sheria inampa mamlaka waziri kugawa vitalu sasa hapo mnategemea nini?
   
 11. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Waziri hajaambiwa tu agawe kiholela, zipo taratibu mule zimeaisnisha sifa za waombaji wanaotakiwa kupewa vitalu. Hakuna excuse hapo, kilichotokea ni ubabaishaji tu hakuna jina lingine la kukipa kitendo kilichofanywa na Maige.
   
 12. b

  bdo JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Nasikia huyu Mzindakayo ali-disco alipokuwa anasoma IDM mzumbe, while akiwa RC morogoro?
   
 13. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu fisadi Mzindakaya anadaiwa pesa nyingi sana na wizara ya maliasili ambazo hajazilipa mpaka sasa kutokana na kumiliki vitalu kitapeli!!!
   
Loading...