Mzindakaya aidai serikalini fidia Bwawa la Kawa kujengwa ndani ya Ranchi yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzindakaya aidai serikalini fidia Bwawa la Kawa kujengwa ndani ya Ranchi yake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Candid Scope, Mar 27, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MRADI wa ujenzi wa Bwawa la Kawa lililoko katika Jimbo la Nkasi Kaskazini, uliotekelezwa na Wizara ya Maji umeibua utata mkubwa baada ya kubainika kuwa bwawa hilo limejengwa katika eneo linalomilikiwa na mwekezaji, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya.

  Utata huo uliwekwa hadharani hivi karibuni pale Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Maji jijini Dar es Salaam ili kuangalia mikakati ya Wizara hiyo katika kutatua kero ya maji nchini. Hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Cheyo ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), kuwa ‘mbogo’ akitaka kujua ni kwa vipi, Wizara hiyo iliidhinisha ujenzi wa bwawa wakati ikijua kuwa eneo hilo ni shamba la Dk. Mzindakaya.

  Katika majibu yake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Sayi alisema kuwa wizara yake ilijenga mradi huo bila kujua kuwa eneo hilo ni la mwekezaji na kukiri kuwa ni kosa kubwa kwa wizara kufikia uamuzi wa kujenga mradi mkubwa kama huo bila kujua uhalali wa eneo husika. Hata hivyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini ambako ndiko mradi huo ulipo, Ally Kessy Mohammed (CCM) alieleza kutokukubaliana na utetezi huo wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, kwamba wizara hiyo ilijenga mradi huo bila kufahamu juu ya uhalali wa eneo husika. “Mwenyekiti si kweli kuwa Wizara haikuwa ikijua kuwa eneo hilo ni la mwekezaji. Kama kweli Wizara ilikuwa haijui kuwa eneo hilo ni ranchi ya mwekezaji, kwanini bwawa likajengwa katika eneo lisilofaa?

  “Nasema hivyo kwa sababu usambazaji wa maji kutoka katika bwawa hilo kwenda kwa wananchi ni mgumu sana, lakini ni rahisi sana kusambaza maji hayo katika ranchi hiyo ya Dk. Mzindakaya,” alihoji Kessy. Mbunge huyo alisema mradi huo ulioigharimu serikali Sh bilioni 1.1, ulilenga kutoa huduma ya maji katika vijiji vya Nkundi, Kalundi na Fyengereza, ingawa pamoja na mradi huo kukamilika lengo lake la kuhudumia vijiji hivyo limekwama kutokana na utata uliojitokeza. “Mheshimiwa Mzindakaya anadai fidia ya mradi huo kujengwa katika ranchi yake ili aweze kuwaruhusu wananchi kutumia maji hayo wakati serikali imetumia mamilioni ya shilingi kuugharamia kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.

  “Sakata hili limesababishwa na Mzindakaya kwa sababu, akijua kuwa eneo hilo ni lake na shughuli yake kubwa ni ufugaji alipeleka ombi serikalini kuomba mradi huo kujengwa katika eneo lake kwa ajili ya vijiji hivyo huku Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ikiwa haijui lolote. “Sasa ikiwa alipeleka ombi hilo kwa ridhaa yake mwenyewe kuruhusu ujenzi wa bwawa la Kawa katika ranchi yake, kwanini anawazuia wananchi kutumia maji hayo?

  Ikiwa hiyo ndiyo hali halisi kwanini anadai fidia serikali wakati ombi la ujenzi wa bwawa hilo alilitoa mwenyewe. “Zaidi ya hayo Mbunge wa zamani wa Nkasi Kaskazini, Ponsiano Nyami aliwahi kutoa taarifa bungeni juu ya hatari iliyopo ikiwa mradi huo mkubwa utajengwa katika ranchi hiyo, lakini kwa bahati mbaya wizara haikuchukulia manani tahadhari hiyo na iliendelea na mipango yake ya ujenzi,” alisema Mbunge Kessy..............

  Source: Habari Leo
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi yale mabilioni aliyokopa na kudhaminiwa na BOT kishayarudisha?
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wao wanatembelea wizara kama nani? Cheyo anafanya kazi ambayo siyo yake! Kikwete anatembelea Wizara, Cheyo nae anatembelea wizara, Mh fulani nae kesho atatembelea wizara etc huku nikuingilia kazi za serikali kinyume na mgawamyiko wa mamlaka katika mihimili ya dola. Mbaya zaidi wanatembelea kuuliza mambo amabayo inabidi waende darasani ndio wayaelewe.

  Bwana Mkubwa, bwawa halijengwi kila eneo, au si kila eneo linafaha kujenga bwawa, kwahiyo inakuwa vigumu kuamini kuwa Mzindakaya aliomba bwawa lijengwe katika eneo lake. Tafuta sababu sahihi iliyoperekea hilo bwawa kujengwa hapo na nini chanzo cha mvutano, unaonekana unajua kuna tatizo lakini hujafuatilia kiundani kujua kwanini bwawa lilijengwa hapo na kwa makubaliano gani, na kwanini sasa hivi kuna mvutano.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mzindakaya alishinikiza mradi wa kujenga bwawa ndani ya lanchi yake ili anufaike na mradi huo katika ranchi yake bila jasho la kuhangaikia kutafuta maji. Leo naona kuna kitu anachohofia mpaka kudai fidia serikalini
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa uzito wake haiyumkini atalipwa fidia kubwa tu.
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  dU SHAMBA LA BIBI MWE SIJUI TUKIMBILIE WAPI KILA KIONGOZI ANA KA EPA KAKE,KWA MTU KAMA MZINDAKAYA HUKO SIKUWATENDEA HAKI WATU WALIOMUWEKA HAPO ALIPO YAANI WAPIGA KURA WAKE,HAINGII AKILINI KWELI MPAKA BWAWA LIJENGWE ENEO LAKO WEWE USIWE NA HABARI ,NA USUBIRI MPAKA LIKAMILIKE NDIO UANZE UFISADI WA KUDAI ETI BWAWA LIMEJENGWA SEHEMU YAKO BILA MATAKWA YAKO,AKINA MZINDAKAYA NDIO SAMPULI YA VIONGOZI TULIONAO ENZI HIZI ,WANATUMIA GHIRIBA NYINGI KUJINUFAISHA,NA KIBAYA ZAIDI MZINDAKAYA ANAWAFANYIA HIVYO WATU WAKE AMBAO NDIO WALITEGEMEA WAPATE MSAADA KUTOKA KWAKE,KWANZA HATA RANCHI YENYEWE KAIPATA KWA MIZENGWE.
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  NASKIA ANAUZA NYAMA NJE YA NCHI?JE Analipa kodi stahiki?
   
 8. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ...Inasemekana pia tayari benki imeshamnyang'anya kiwanda (kiko under receivership) baada ya kushindwa masharti ya mkopo..

  Suala la yeye kuweka influence ili bwawa lijengwe shambani/ranchi ya/kwake inawezekana ni kweli maana mkulu yule ni mjanjamjanja sana...:gossip:
   
Loading...