Mzimu wa Zitto warejea Buzwagi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,889
Mzimu wa Zitto warejea Buzwagi

na Ali Lityawi, Kahama
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MGOGORO uliopo kati ya mwekezaji wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama na wanakijiji waliozunguka eneo hilo, bado unachemka.

Kwa kiasi kikubwa, viongozi wa serikali bado wanakuna vichwa na kufikiri njia za kumaliza mgogoro huo, ambao umekuwa ukichukua sura mpya kila siku na kutishia mazingira ya uwekezaji.

Katika hatua ya hivi karibuni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, alilazimika kusitisha mkutano wa hadhara katika eneo hilo, na badala yake kuitisha kikao kingine cha faragha wakati wa usiku.

Kikao hicho, kilichowahusisha wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, kilivunjwa na naibu waziri huyo mchana, baada ya kutokea kutoelewana baina ya wadau wa mgogoro huo.

Malima alilazimika kuahirisha kikao chake na wakuu wa idara, halmashauri na viongozi wote na kuitisha kikao cha dharura na kamati hiyo baada ya kushtushwa na maelezo ya Mbunge wa eneo hilo, James Lembeli, kuhusu mapunjo ya fidia waliyofanyiwa wananchi.

Hata hivyo, kikao hicho ambacho kilimhusisha pia mbunge huyo na maofisa wa Idara ya Madini, hakikuweza kufikia muafaka na kulazimika kufanyika tena asubuhi ya siku iliyofuata.

Licha ya kuahirishwa, kikao hicho kilifanyika kwa zaidi ya saa tatu, huku kikilazimika kuwajumuisha pia maofisa wa Idara ya Ardhi wilayani humu.

Kufanyika kwa kikao hicho, kulitokana na hoja ya Lembeli, aliyebainisha chanzo cha mgogoro huo kuwa ni ubadhirifu katika kuthaminisha mali za wakazi hao na shinikizo lililokuwepo wakati wa malipo ya fidia.

Lembeli alieleza kwamba, kabla ya kumalizika kwa vikao vya kamati iliyoundwa, ili kujadiliana na mwekezaji juu ya stahili za fidia kwa wakazi hao, malipo yalianza kufanyika licha ya kutofikiwa kwa makubaliano.

Mbunge huyo alisema mthamanishaji wa serikali, akishirikiana na yule wa mgodi, waliorodhesha mali za wakazi wa vijiji vya Mwime, Chapurwa na Mwendakulima kwa penseli, ilhali majina na saini ziliandikwa kwa kalamu ya wino.

Mbunge huyo alisema hali iliyosababisha mtafaruku katika malipo ni baada ya kubainika kuwa fomu hizo zilirejea zikiwa na mali pungufu, na walipothaminishiwa tena zikandikwa kwa kalamu ya wino tofauti na ilivyokuwa awali.

Aliendelea kusema wanakijiji hao walilazimishwa kupokea malipo hayo na baadhi ya viongozi wa serikali ya wilaya, huku wakitambua kwamba vikao vya kamati ya makazi mbadala, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama, haijakamilisha vikao vya makubaliano baina yake na mwekezaji.

Mbunge huyo alibainisha kwamba, kamati hiyo ilifanya vikao halali vitano huku cha sita kikiwa si rasmi kati ya vikao vinane, huku mkurugenzi huyo akihudhuria vikao vitatu wakati anatambua kuwa alipaswa kuongoza vikao hivyo.

Lembeli, alizidi kueleza kuwa baada ya wahusika wa malipo hayo kugundua kuwa fidia waliyopokea hailingani na mali waliyothamanisha, hawakuwa tayari kuendelea kupokea malipo hayo, lakini walitishwa na kulazimika kukubali.

Alisema baadhi ya wananchi waliochunguza kilichokuwa kikiendelea baina ya pande hizo mbili, walilipwa zaidi kwa lengo la kuzibwa midomo.

“Kwa hili sibahatishi, nina ushahidi nalo. Mfano ni Mzee Kubiluha… awali alilipwa sh milioni 32, lakini wanawe walipomsumbua kutokubaliana na malipo hayo na kuamua kufuatilia, alilipwa tena sh milioni 132 zingine,” alisema Lembeli.

Akitoa mfano mwingine, mbunge huyo alisema mzee Charles Muhamali (60), alikataa kupokea pesa baada ya kubaini kuwa amepunjwa. Alikamatwa na kufunguliwa kesi ya kumpiga mlinzi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, ili kumtia hofu akubali malipo hayo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Magese Mulongo, alisema zoezi hilo lilitekelezwa kwa mujibu wa sheria na mkataba wa malipo hayo kuwa wa kisheria, huku akidai kuwa suala la malipo hayo lilifanywa na serikali kuu, kupitia Wizara ya Nishati na Madini.

Hivi karibuni, mgogoro huo ulichukua hatua nyingine mbaya baada ya Jeshi la Polisi kulazimika kurusha mabomu ya machozi katika eneo la mgodi huo, kwa lengo la kuwatawanya wananchi waliodaiwa kufanya fujo mgodini hapo.

Katika tukio hilo, wananchi 14 walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kukata uzio unaozunguka mgodi wa Buzwagi kwa madai ya uongozi wa mgodi kukiuka makubaliano ya kuwatengenezea barabara mbadala kabla ya kuziba njia zilizopita ndani ya uzio huo.Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 4 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
mhe.lembeli tumekusikia.wakati wa mjadala wa buzwagi bungeni kati ya karamagi na shujaa zito mbona hukumuunga mkono zito? kwa kuwa sasa umezinduka kaza kamba!

na james peter, mwanza/tanzania, - 18.05.08 @ 08:25 | #11637

Ni jambo lilio wazi Kahama kuwa Brian Whiteley wa Barrick ana nguvu zisizo na mfano kwa viongozi wetu wa Wilaya.
Sioni ajabu mkuu wa Wilaya akidai wananchi walilipwa kwa mujibu wa sheria.
Brian, ikumbukwe ni mpishi tu kwa sifa, ana nguvu hata kituo cha polisi.
Security Manager wa Buzwagi anayejulikana kwa jina la Hoppy anapanga lini FFU wawepo Buzwagi getini.
Ajabu naibu waziri alipokuja Kahama, chakula cha mchana alilia Buzwagi Mgodini- Mnategemea atoe ufumbuzi wa kutetea wananchi?
Kama kweli mchango wa migodi kwa mapato ya Taifa ni 2.3% kama alivyosema Rais, kwa nini watu hawa wawe na nguvu kiasi hiki.
Najiuliza mchango wao kwa uchumi wa viongozi wetu ni asilimia ngapi.
Labda tukijua mifuko ya viongozi wetu inatunishwa kwa asilimia ngapi, tutapata jawabu la kwa nini wachangiaji wa 2.3% waabudiwe kiasi hiki.

na Lemomo, London, UK, - 18.05.08 @ 09:37 | #11646

Sector ya Madini katika nchi zetu bado imekuwa ngeni sana kwa viongozi wetu wa kisiasa. Hili ndilo tatitzo kubwa lililoko. Muwekezaji hasa katika mineral industry huwa anaangalia sehem ambayo kuna udhaifu (loop hole) na hutumia hiyo kujinufaisha.
Ninavyojua kama Mining Engineer matatizo mengi kwenye uwekezaji hapo nchini kwetu yanatokana na
1. Kujifanya tunajua kila kitu
2. Ufisadi (Kupenda kujilimbikizia mali)
3. Umbumbu
4. Kunyenyekea watu
Viongozi wa kisiasa wakiona mzungu hawasemi kitu. Yeye anakuwa ndo Kamusi yao.Ndo maana wao hutumia udhaifu huo kuhakikisha wanavuna vya kutosha.
Ni ukweli usiofichika wenzetu wanatumia sector ya madini kama njia ya kuleta maisha bora kwa wananchi wao. Mfano mzuri ni huu mji wa sudbry. Mining industry ndo zinaujenga.
Migogoro inaweza kuisha kama kutakuwa na ushirikishwaji wa wananchi kuanzia kipindi cha utafiti mpaka kuanza kuchimba (Community involvement in mining investiment)
Wananchi waelezwe faida na hasara kwa uwazi. waelezwe wao watafaidi nini. Hatimaye wapatiwe fidia zao kwa haki. Pili wakati mgodi unafanya kazi kuna meni wananchi wanapata kutokana na mgodi kufanya kazi hapo. Tanzania ni option kuwasaidia wananchi. Hapo ndipo mgogoro unapozuka. Issue ni kuhusisha jamii na kupata viongozi safi ndo migogoro itaisha. Kwa kuangalia hapo serikali ya wilaya yote ni Corrupt kuanzia halmashauri hadi mkuu wa wilaya. Hakuna ufumbuzi hapo. Ukweli na mbunge huyo lazima watamzushia tu kwani wako kwenye mstari mmoja na yeye yuko tofauti.

na Mgumbwa, Sudbury Canada, - 18.05.08 @ 18:09 | #11729

WAKOLONI WA TANZANIA LEO NI WATANZANIA WENYEWE AMBAO HAWANA NIA NJEMA YA KUTETEA WATU WAO. WANAJIKOMBA KWA WAGENI NA KUWANYANYASA NDUGU ZAO. HALAFU WANASEMA WANAWAKILISHA SERIKALI, SERIKALI YA WATU GANI WANAWAKILISHA HAO WANAFIKI?? HAMUONI AIBU NYIE. HAO MNAOJIKOMBA KWAO WANAWACHEKA KILA SIKU WANAPOKUTANA KATIKA VIKAO VYAO!!

na JICKY, UK, - 18.05.08 @ 18:34 | #11736
 
Bubu,

Tutafika,subiri nipashe, watanzania kila kukicha wanang'amua jambo moja, kesho la pili na mtondogoo la tat....., siku yaja viongozi wetu watatamani dunia iwameze, tumuombe mola tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom