Mzimu wa Uwanja wa Sokoine Unavyoimaliza Yanga

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,709
10,204
TIMU YA WANANCHI NA MZIMU WA UWANJA WA SOKOINE MBEYA.
Mwaka 1986, Tukuyu Stars kutoka Bagamoyo, Tukuyu, Rungwe, ilichukua ubingwa wa Tanzania Bara ikiwa ni mara ya kwanza timu kutoka wilayani kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara. Nilikuwa darasa la saba.
Mwaka huo Yanga ilipoteza mechi zote mbili kwa kufungwa na Tukuyu Stars. Mechi ile ya Dar es salaam na mbeya. Alifungwa Dar bao 2-1 kisha akafungwa bao 1-0 bila katika uwanja wa Sokoine. Kona ya beki nambari tatu Daniel Chundu.
Mwaka 1987, Yanga ya Said Mwamba Kizota ilirudi tena uwanja wa Sokoine, katika mechi ambayo ilitokea tafrani na wachezaji wa Tukuyu Stars kuwagwaya wa Yanga, huku Yanga wakiongozwa na Kizota, waliwatembezea kichapo wachezaji wa Tukuyu Stars huku mchezaji pekee wa Tukuyu Stars aliye-resist alikuwa Mwana- Kigoma, Hussein Idd ambaye alipata kuhudumu katika Yanga mwanzoni mwa miaka ya themanini. Mechi hiyo iliisha kwa sare tasa 0-0.
Julai mwaka 1991, Yanga chini ya Kocha Mziray ilikuwa uwanja wa Sokoine kupepetana na Tukuyu Stars.
Stephen Musa "Master" alimpiga kanzu Willy Mtendawema na kipa Sahau Kambi alipomsogelea akaukuta mpira uko kwenye nyavu ya goli lile linalotazamana na shule ya sekondari ya Mbeya Day!
Yanga chini ya Mziray (nilimsikia Mziray kwa masikio yangu akimwambia jamaa mmoja simkumbuki jina baada ya mechi kuisha pale katikati ya uwanja kuwa " We are going to appeal". Tukuyu Stars walikatiwa rufaa eti kwa sababu mchezaji Michael Kidilu alivaa jezi na kukaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba wa Tukuyu Stars.
Michael Kidilu alikuwa amepata kadi nyekundu katika mchezo uliotangulia kabla ya mechi hiyo na Yanga.
Mechi hiyo iliamuliwa kurudiwa tena na Waziri wa wakati huo wa michezo Mh. Charles Kabeho.
katika mechi hiyo ya marudiano ambayo nilibahatika pia kuiona uwanjani hapo, Yanga walishinda kwa bao la kona ya utata. nyavu zilikuwa zimetoboka na wakati kona inapigwa katika goli lilelile linalotazamana na shule ya Mbeya Day, golikipa Joshua Kilale alikiwa amebana kwenye nguzo ya mwanzo mpira ulipopigwa ukaingilia nyavu za pembeni zilizokuwa zimetoboka na refa kuamuru kuwa ni goli. ( yaani mfano wake ni kama vile siku ile singida walipofunga goli mechi yao na Yanga pale Namfua na mpira kuingilia nyavuni kutokea kwa nje na watu wakifiri ni goli lakini picha za marudio zikaonyesha mpira umeingilia kwa nje)
siku ya mechi hiyo ya 1991 mpita uliingilia kwa nje lakini kwa chini na nyavu kweli zilikuwa zimetoboka. ikazuka vurugu lakini mpira uliendelea na Tukuyu walilala kwa bao hilo 1-0.
wakati huo ilikuwa nadra sana mechi kuchukuliwa video lakini bahati nzuri kampuni ya Ghana Building contractors ilikuwa na vifaa hivyo na bwana mmoja kika alirekodi tukio la mechi yote hiyo na nilibahatika kuiona video hiyo jioni tukiwa na wachezaji wa Tukuyu Stars hakika mpira haukuingia kupitia ndani ya nyavu bali nje ya nyavu.
Mzimu mwingine wa uwanja wa Sokoine uliwakuta Yanga mwaka 1992, safari hii Tukuyu Stars wakiwafanyia Yanga uhuni wa mwaka.
Uhuni wa hali ya jiuu kwelikweli na Yanga kutikisika vilivyo.
Tukuyu Stars walicheza na Refa wa mechi hiyo kama kumbukumbu zangu ziko sawa alitoka Dodoma. Vyanzo vyangu vya habari vilinipasha kuwa wafadhili wa Tukuyu Stars walimpatia refa huyo roli zima lililojaa magunia ya mahindi. piga picha lori Isuzu tani saba linejaa magunia ya mahindi!
siku ya mechi huku Yanga ikiwa imekamilika ilikiwa kila ikipiga bao, refa anakataa kwa madai kuwa ni off side. lakini Tukuyu wakienda hata "100" refa anaacha na hapo Yanga wanakuja juu si kitoto. ile ya Nsajigwa aliyowaka juzi ni cha mtoto! hiyo ikapelekea
Refa wa mechi hiyo atoe kadi sana kwa wachezaji wa yanga na mwisho kupelekea kutoa kadi nyekundu kwa Hamisi Thobias Gaga. hapo refa keshawspa Tukuyu bao mbili ambazo zote kina Justin Njcodrmus Mtekere alikuwa wanafunga wakiwa wameotea.
yanga wlifanya ujanja kama huo unaodaiwa kufanywa na Mbeya city juzi. kwenye vurugu za kadi nyekundu aliyetakiwa kutoka ni Gaga lakini Yanga walimtoa Issa Athumani Mgaya na Gaga akawa anaendelea kucheza. Lakini hapa mwamuzi wa akiba alikuwa makini akamshtua refa kuwa aliyetakiwa kutoka ni Gaga na bado yumo uwanjani na kwamba Yanga wamemtoa Issa. Refa ilibidi amtoe Gaga na Issa kuamriwa kurudi uwanjani. mwisho wa mechi ikawa sare ya 2-2 Yanga wakichomoa bao zote mbili huku refa akiwa amewafanyia uhuni wa hali ya juu wa kuwatoa mchezoni. Ni mechi ambayo Tukuyu Stars walibebwa lakini hawakubebeka.
Chanzo changu kilimuuliza tefa yule wa kutoka Dodoma kuhusu mambo ya mpira na alisema waziwazi kiwa hakuna uchawi katika soka bali mchawi ni refa tu basi.
katika mwaka 1997 timu ya Yanga katika ligi ya Muungano iliamua ueanja wa Sokoine uwe uwanja wake wa nyumbani kama mnakumbuka uwanja wa Uhuru zamani uwanja wa Taifa ulifungwa kupisha ukarabati ulioghatimu bilioni 3 ( hapa prsa laxima zilipigwa kwa sababu kwa maoni yangu hakuna kilichofanyika maana uwanja ulikuwa kayika hali ileile.)
Sasa Yanga ikiwa jijini Mbeya haikufanya vizuti sana na mzunguko wa pili ikahamia Dodoma. Mzimu wa uwanja wa Sokoine uliwakuta kwenye mechi ya kihistoria ya kwanza mjini Mbeya ya watani wa jadi.
Yanga walipata bao la mapema baada ya kumfunga kipa Issa Manofu lakini Simba ikaja kusawazisha kupitia mpira uliotakiwa uwe indirect kick lakini George Masatu akaupiga direct kick huku mpira ukimkuta Joseph Katuba akiwa hajajiandaa na refa kulala kati. Wachezaji a Yanga wakamfuata line two aliyekuwa upande ule wa geti la kuingilia magari na kumzonga sana lakini uamuzi haukubadilika na mechi ikaisha kwa sare ya 1-1.
Mzimu wa uwanja wa Sokoine uliwakuta tena Yanga mwaka 2003 wakati dalili zote zilionyesha kuwa Yanga wapo katika nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa lakini walipoyeza mechi kwa Tanzania Prisons kwa kufungwa mabao 3-2 huku Yanga wakiwa juu ya msimamo wa ligi na Mtibwa pia akiwa wa pili na uwezekano wa kuwa bingwa lakini Simba iliyokuwa nafasi ya tatu ndiyo ikaja kuchukua ubingwa huku Yanga na Mtibwa zikipoteza mechi zao katika kile kilichokuja kuelezwa na kuwa maarufu sana kuwa "watu wa kazi wa Simba walicheza mechi zote tatu yaani ile ya Mbeya, ya Mtibwa na ya kwao wenyewe Simba.
Hayo ndiyo matukio ya timu ya Wananchi na mzimu wa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo wamekuwa wakikumbana na visa vituko na mikasa.
Tukio la juzi ni kama marudio tu ya yaliyokuwa yakitokea zamani.
 
Mkuu nimeipenda andishi lako, kumbe ni suala la historia.
 
Next time Hebu tupe kisa cha CCM Kirumba, n'a Toto africa dhidi ya Mnyama Simba. Maana Simba ndani ya Kirumba akiona toto africa ugeuka nyau.
 
Bado nacheka nikiukumbuka UHUNI ule wa Mbeya City FC waliotufanyia Yanga SC wiki iliyopita. Kina Asagwile Ambokile sio watu wazuri kabisa.
Kinachonichekesha mpaka sasa ni maajabu ya Wahuni wa KARIAKOO, Kuzidiwa maarifa na Wahuni wa MWANJELWA.
Sikuelewa kitu mpaka nilipomuona Shadrack Nsajigwa Mwandemele akilalamika mbele ya Camera za AZAMTV, sikuelewa mapema dakika chache nikaelewa ule uhuni wa Mbeya City kuendelea kumtumia Mchezaji ambaye tayari kapewa RED CARD!
Shadrack Nsajigwa Mwandemele ni Brother wangu, mtoto wa Makandana-Tukuyu, ni sahihi, alipaswa kulalamika kiasi kile kwani alikuwa ni Kocha mwenyeji; (anawaelewa vizuri sana wahuni wale).
Uhuni wa Mwanjelwa ni wa muda mrefu, kipindi Abiria unaibiwa mali zako kabla hata hujashuka kwenye BUS na Mwizi hajulikani.
Niliyemsikitikia ni yule REFARII wa mchezo, MUHA mwenzangu yule wa Mwanga Sokoni-Kigoma, wahuni wale kiukweli wamemkaribisha Jijini Mbeya.
Brother Nsajigwa:
NEXT TIME IF YOU WANT TO CATCH WOLVES USE WOLVES.
 
Mwalaye ce mtama!!1
 
umenifanya nicheke kwa sauti mkuu eti ....Wahuni wa kariakoo kuzidiwa uhuni na wahuni wa mwanjelwa...
 
umesahau mechi ya mwaka Jana Yanga na Mbeya city..Yanga anakufa 2-1..faulo inatokea pembeni ya uwanja refa anamuonyesha mchezaji wa Mbeya city filimbi mpaka apulize ndio apige....wanaanza mpira fasta huyu huyu Raphael Daudi anapiga mjishuti kama goli lake LA juzi..Yanga waliwaka mpaka mabomu ya machozi yalipigwa
 
Back
Top Bottom