BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
Mzimu wa ufisadi wawafuata makandarasi
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima
SAKATA la ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), linaonekana kuibua tuhuma nyingine kadhaa baada ya waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Bulk Building Company Limited, kutishia kutoa siri za wakurugenzi wa kampuni hiyo wakidai kuwa wanapaswa pia kuchunguzwa.
Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar es Salaam, walisema wana mashaka na jinsi kampuni hiyo waliyokuwa wakiifanyia kazi awali ilivyopata moja ya zabuni za kujenga jengo hilo.
Walisema kampuni hiyo ilipata zabuni ya kusuka vyuma kwa njia walizodai kuwa zenye mashaka kutokana na usiri wa mkataba wa zabuni hiyo na uhamisho pamoja na kufukuzwa kwa wafanyakazi wanaojaribu kuhoji au kukosea utendaji kazi wa kampuni.
Walisema uamuzi wao wa kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu zabuni hiyo unatokana na vitendo visivyoridhisha walivyofanyika na kampuni hiyo kabla ya kutimuliwa kwa madai ya kufuatilia siri za kampuni na kusambaza kwa watu hatari.
"Tumeamua kuitoa siri hii kwa sababu tulifanyiwa vitendo visivyoridhisha na viongozi wa kampuni, wakati sisi tunajua wanafanya nini, historia ya kampuni hii ni yenye mashaka sana katika utendaji kazi. Serikali ikiifuatilia itagundua mengi," alisema mmoja wa watu hao ambaye jina lake tunalihifadhi.
Akizungumzia madai hayo, mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Attu Mwakitwange, alisema watu wengi wamekuwa wakiiandama kampuni yake kwa sababu imepata mafanikio makubwa kwa haraka.
Alisema washindani wao kibiashara wamekuwa wakisambaza maneno ya kuchafua jina la kampuni bila mafanikio na kuongeza kuwa kama kuna kasoro, basi ni za kawaida, ambazo kila kampuni inaweza kuwa nazo.
Alipoulizwa kuhusu madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kutokamilisha kazi zake nyingi inazopata, alisema hilo liko juu yake na kwamba anayeweza kulizungumzia ni kiongozi wake ambaye hakumtaja jina.
Hata hivyo alisema kuwa, atawasiliana na bosi wake na atatoa maelezo kuhusu tuhuma zinazoelekezwa katika kampuni yake wiki ijayo.