Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Bwana Godbless Lema ameendelea kuandamwa na kashfa ya kumnadi Diwani wa CCM Sombetini Bwana A Mawazo katika uchaguzi mdogo.Bwana Lema mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Arusha mjini amejikuta akishindwa kutoa majibu ya kuridhisha wapiga kura ni sababu zipi zilimfanya amfanyie kampeni Bwana A Mawazo mwana CCM na kumwacha mgombea udiwani wa CHADEMA,CUF na TLP ?.Ikumbukwe Bwana Mawazo alikuwa diwani wa TLP kabla ya kujiunga na CCM.
Mkutano wa Dr W Slaa Mbauda ulibakia kama karata pekee ya kumwokoa Lema dhidi ya kashfa ya kuuza ubunge mwaka 2005 na kumfanyia kampeni Mawazo lakini bado hakuweza kujitoa kwenye kashfa hizo na hata Dr Slaa ilielekea alikuwa akijua dhambi yake.Alimtaka awe makini kwani anaweza kumtosa ???????.
Wagombea udiwani wa CHADEMA wameonekana kuwa na nguvu zaidi ya mgombea ubunge hasa baada ya mkutano wa Dr W Slaa.Madiwani wa kata za Kimandulu,Elerai na Moshono wameendelea kuvutia wapiga kura wengi kuliko mwanzo,Bwana Lema amekuwa akitegemea kubebwa na madiwani wa kata hizo zaidi tofauti na mwanzo wa kampeni zake madiwani walikuwa wakimtegemea zaidi ili kuwafikia wapiga kura wengi.
CCM inafanya vizuri kata ya Kati ilipo ngome kuu ya Mama batilda,mkutano wake maeneo ya St Thomas Hospital ulivutia watu wengi sana huku mgombea udiwani wa kata ya kati akiwa na uhakika wa kushinda kata hiyo.
TLP inaringia kata ya Sokoni 1,Sombetini,Lemara na Ungalimited.wapiga debe wa TLP wanatumia udhaifu wa Bwana Lema hasa kitendo chake cha kumpigia debe mgombea wa CCM.