Mzimu wa Nyerere wamuandama Pinda sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzimu wa Nyerere wamuandama Pinda sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Jul 24, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ni Waziri Mkuu mwenye huruma na upendo kuliko wote waliopita,amewahi kulia juu ya mauaji ya Albino, ni mtoto wa Mkulima anayejua kijiji na kilimo kwanza nini. Pinda amekaa Ikulu muda mrefu kama mwana usalama toka enzi za Mwalim hivyo anamjua Mwalim vizuri ingawa hakuwa gwiji la siasa.

  Amekuwa akijibainisha kama mfuasi wa sera za Mwalim hasa katika falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea,ni mkubwa sasa katika nafasi ya tatu kutoka kwa Rais huku bara.Nafasi yake inawagusa wote walioko ndani ya Nchi,hivyo lolote analolifanya ama tenda ni taarifa kwa umma.

  Pinda toka ateuliwe baada ya Lowassa inasemekana hajawahi kuzuru katika kaburi la Baba wa Taifa wala kutoa pole akiwa Waziri Mkuu. Tunajua si lazima kufanya hivyo kwani hili ni suala la kibinadamu zaidi ndio maana kuna watu hawakosi katika misiba na wengine misiba ni kituo cha polisi.

  Pinda amefika mkoani Mara mara nyingi tu, hasa Tarime na kwingineko,hivi ni kweli hakujua ama hajui Mwalimu amelala pale Butiama na watu wanatoka mataifa ya mbali kuzuru pale. Binafsi nashangaa na nimeshitushwa na kauli ya Familia ya Mwalim yenye uchungu juu ya Binadamu huyu Kayanza.

  Pengine nadhani aidha alipitiwa ama amezidiwa na msongo wa mawazo ya Kitaifa na kusahau historia ya Taifa hili. Pinda anaendeshaje Nchi bila kujua historia wakati ilikuwa sehemu ya Masomo yake yaani HGL mpaka kuwa Mwanasheria.

  Pinda rudisha utu kwani death is an innevitable destiny,usije ukaipa shida familia yako pindi nawe utakapo kick the moon (pass away). Uzalendo ni pamoja na kujaliana katika shida na simanzi. Haiwezekani mtoto wa Idd Amin, adui mkubwa wa Taifa hili na Mwalim pia kuzuru kabuli na kutoa pole,wewe kiongozi Mkuu unapita tu Butiama.

  Pinda bila Mwalim usingekuwepo wewe,shule umesoma bure,madaraka umepata, pesa unayo,ulinzi unao,usafiri upo,muda unao leo unashindwa kuitembelea familia ya Mwalimu? Msiba hauozi na hata kama ukioza historia haifutiki. Haya yamejitokeza baada ya Madiwani wa Mkoa wako wa zamani kutembelea Shule ya Mwalimu na kuikuta iko katika hali mbaya na isiyo na historia tena. Swali liliulizwa kama Waziri Mkuu anajua hali hii,ikabainika hajawahi kutia mguu si katika shule bali hata katika Kaburi.

  Pinda hata kama hu-anti-social ama una aleji na misiba au makaburi, ukiwa kiongozi wa kitaifa ni muhimu uka-declare interest kwa hayo Wananchi tukakujua na si kuacha tu-feel gap na matokeo yake ni grapevines.

  Panga safari uende na uombe radhi kwa hilo acha mambo ya kujitenga na jamii,umepata yote hayo kwa njia nyoofu aliyojenga Mwalimu. Shame on u Pinda.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  Shame on you! Mi nimeenda kwa gharama yangu, we unashindwa kwenda kwa gharama yetu? Ndo maana huoni uchungu na ufisadi!
   
 3. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Nyerere foundation ya akina butiku inafanya nn kuhusu kuiweka ktk mazingira mazuri na bora hiyo shule ya msingi ya nyerere?butiku anafanya kazi gani pale yeye anatakiwa kulinda mustakabali wa historia ya mwalimu zikiwemo shule,muacheni pinda ajipindie zake kama alivyopinda akipata muda atatembelea kaburi la nyerere
   
 4. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kuzuru kaburi ni kipimo tosha cha kumuenzi Nyerere..Kama sikosei hata CCM walishawahi kufanyia moja ya mikutano yao ya NEC pale Butiama..lakini hatujaona kizuri walichokuja nacho. Hata saa mbovu ina thamani zaidi ya siku..
   
 5. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  'waacheni wafu wazikane wao kwa wao'... By the way ni majukumu tu, akipata nafasi ataenda especialy mwaka huu kwenye kuzima mwenge na maazimisho ya miaka 50 ya uhuru coz yamepangwa kufanyikia butiama
   
 6. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nyerere foundation haina jukumu la kukarabati shule ambayo iko chini ya Serikali na wanafunzi wapo wanasoma.Shule hii ni shule ya Msingi Mwisenge kata ya Mwisenge,barabara ya kuelekea Makoko Serminary Secondary School, wilaya ya Musoma Mjini.Shule hii ni shule aliyosoma elimu ya Msingi Mwalimu Nyerere.

  Mwalimu angependa kuijenga na imani hakuna shule ambayo ingekuwa mfano wake kwa ubora hapa Tanzania,uadilifu wake ndio unaotupa faraja leo.Hatuna haja ya kuibomoa na kujenga upya kwa maana tutapoteza historia,la msingi ni kuiboresha isipotee kihistoria.
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Duh! Sijui hii imefanyika by design or default! Ina maana hata kile kikao chao (CCM) walichokifanyia BUTIAMA hakufika hapo ulipolala mwili wa Mwl!? kama ndivyo nadhani tunatatizo kubwa zaidi ya haya tunayoyaona kwa Macho.

  Eeh Mungu tunaomba uilaze mahal pema roho ya mzee wetu huyu, na tunaiomba mzimu ya kizanaki izidi kuiamsha mizimu ya Mwl ili iwaandame viongozi uchwara wasiotutakia mema, wale wanaotetea wizi, wanaofumbia macho wizi, na wanaohalalisha wizi wa mali za UMMA

  AMEN
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Ungejua hiyo Nyerere foundation inavyopigwa mawe na walafi wala usingesema. Hicho kiwanja tu cha kujenga jengo lao almanusura ishu iende mahakamani. Utawala wa m.kwere ni janga la kitaifa
   
 9. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,405
  Trophy Points: 280
  Pinda amekuwa fisadi siku hizi. Hawezi kulia tena... Angekuwa yule Pinda wa 2008 angelia hata ishu ya Jairo kwa kuwahurumia wakulima wenzake wa zamani. Ila siku hizi mwenzetu amekuwa mkulima wa tumboni.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Nyerere foundation inakufa kwa kuwa JK na Butiku haziivi!!!foundation haina support yoyote toka serikalini kwa sasa!!utakumbuka kuna eneo la foundation kujenga kitega uchumi karibu na ikulu lakini JK katia pini hakuna kujenga na huenda eneo kishapewa mhindi
   
 11. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa mkulima sijui alitendwa nini na Mwalimu - kwanza yeye mizengo ni Mkatoliki. Na tofauti na madhehebu mengine ya Kikristo wakatoliki wanaamini katika kutembelea makaburi na kuyafanyia usafi na hata ukarabati wakiamini kuwa marehemu kapumzika pale akisubiri siku ya mwisho na kwamba hupaswi kupunguza heshima ya marehemu kwa vile kafa. Mhadhama Amigus wa Radio Maria anaweza mkumbusha mizengo. Mtoto wa mkulima kulikuwa na kitu gani mbaya aliyokutenda Mwalimu??!!
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Pinda kuna mengi sana ya kumsema, lakini si hili.

  Hizi ndio kama zile habari za Tea Party movement waliposema Obama si mzalendo kwa sababu havai ki lapel cha bendera ya Marekani kwenye suti yake.

  WTF, hao familia ya Nyerere wenyewe wakiona mifisadi inajazana kuhiji hapo kwao sanasana wataona gozigozi tu.

  Nyerere alikuwa intellectual, na ingekuwa muhimu zaidi kumuenzi intellectually kwa kuangalia ideas zake. Sasa kama mnataka kumsema Pinda kwa hilo hapo mnaweza ku make sense.

  Kwani Butiama kushageuka Maka ya Watanzania siku hizi, kwamba kwenye nguzo tano za uongozi Tanzania kuhiji Butiama ni lazima ?
   
 13. Umutimbaru

  Umutimbaru Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mtoto hapaswi kukumbushwa ila inapobidi kukumbushwa basi ni wajibu wa washauri wake kumkumbusha mambo muhimu kama hayo ya kutembelea kaburi na kupalilia au hata kuweka shada la mauwa. Nijuavyo bado anayo nafasi yakufanya yote hayo
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  As if kwenye kaburi la nyerere ndo kuna majibu ya maisha,huko mi nakuita kuabudu sanamu!
  kama Pinda haamini katika mizimu kwanini wana mtaka aende huko?
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Wabongo ndio maana hatuendelei, imani za mizimu na ushirikina kibao.

  It's not like kaburi la Nyerere linamuhitaji Pinda kuling'olea majani or anything like that.
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kulia haina maana ya tafsi ya huruma, yeye ndio anajuwa kilicho mliza ni siri yake; ila mimi nadhani alikuwa analia kufahamu kuwa wanaouwa albino ni watu waliojuu yake ambao hana la kuwafanya bali kulia tu!
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Anaogopa mwalimu atafufuka na kumsuta jinsi yeye na magamba wengine wanavyomwangusha!
   
 18. t

  takeurabu JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  absolutely yes!
   
 19. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Labda nikumkumbusha ni heri kuonekana mtovu wa nidhamu kwa kukataa uchafu kulikoni kutukuzwa kwa kuukubali uovu.Muda wake kuthibitisha kuwa yuko huru kwa mawazo yake na utashi wake.Kupitia madaraka aliyonayo anaweza kuleta mabadiliko ya mpaka huko anako kuogopa.Cha msingi ni kukubali sio lazima kungangania kufikilia hivyo nia njema ujengwa na maamuzi mema na yenye faida kwa wengi.Cha msingi ni uthubutu na msimamo nao watajua kuwa hata kama yalikuwa ni maigizo maisha hayawezi kuigizwa kwani ufika pointi ukweli uzidi dhidi ya uongo.

  Ni heri kuwa huru kwa faida yake na ya Watanzania kwa kuwa alichagua kuwatumikia kulikuwa kifungoni kwa wachache ambao ujuhi dhamila yao nini?
   
Loading...