Mzimu Wa Nyerere Bado Waiandama Zanzibar, Sasa Wataka Nyerere Mwengine: Makala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzimu Wa Nyerere Bado Waiandama Zanzibar, Sasa Wataka Nyerere Mwengine: Makala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 22, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Zanzibar yataka Nyerere mwengine

  Na Ally Saleh 'Alberto'

  Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kuwa kipenzi kikubwa sana cha wananchi wa Zanzibar. Na hilo ni kwa sababu nyingi ambazo kwa ukweli au dhana walizihusisha nae. Kama ningeruhusiwa kuwasemea Wazanzibari nigethubutu kusema kuwa Nyerere hakuliliwa sana wakati alipofariki kama vile ambavyo watu hawakutaka kumfurahia wakati wa uhai wake.

  Lakini hii haina maana kabisa kuwa Nyerere hakuwa na heshima mbele ya Wazanzibari. Ukweli ni kuwa heshima yake ilikuwa ni ya hali ya juu kwa sababu wengi walimuona kuwa ni mtu mwenye uwezo sana wa kujenga hoja na ambaye daima hakuogopa kusema fikra zake wakati akiwa kwenye siasa na nje ya siasa.

  Wanajua pia mchango wake katika suala zima la kuunganisha watu wa Zanzibar kupigania uhuru wao. Yeye ni chanzo kikuu kilichopelekea kuundwa au tuseme kuunganisha nguvu za Shirazi Association na African Association na kuzaliwa Afro Shirazi.

  Binafsi wakati mmoja nilishangaa mwaka 1985 nilipopata maagizo kuwa Mwalimu ametaka kupata maelezo kutoka kwangu kuhusiana na taarifa niliokuwa nimeitoa kwenye Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC. Taarifa hiyo ni kuwa Wazanzibari walikuwa wanapendelea Rais wa Zanzibar Ali Hassan Mwinyi abakie kuwa Rais wa Zanzibar na asiende kushika wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

  Wakati huo ilikuwa tayari minon’gono ilikuwepo kuwa Mwinyi anaandaliwa kuwa Rais wa Muungano na ilhali alikuwa kipenzi cha Wazanzibari kwa hatua zake ambazo zilikuwa zimeanza kuifungua Zanzibar kibiashara na kiuwekezaji, lakini muhimu zaidi kwa Wazanzibari ilikuwa ni kurudishiwa uhuru wa maoni na haki za binaadamu.

  Hivi kwa Wazanzibari ndivyo alivyokuwa Mwalimu kuwa hakuweza kuacha kitu chochote kile bila ya kukiulizia na kama si kukiulizia basi kukisema na zaidi ya hapo hata kukikemea. Na mifano ya hiyo iko mingi sana ingawa mara mbili tatu aliwaangusha Wazanzibari kwa baadhi ya mambo kuyaachia na kutishia hata uhai na usalama wa Zanzibar.

  Nyerere hakuwa mkali au tuseme alikuwa mzito wa kumgomba au kumkosoa Rais Abeid Karume na wengine tunaamini ni kwa sababu kwa wakati ule alikuwa anataka Zanzibar ibakie katika Muungano wa Tanzania kwa gharama yoyote ile.

  Maana Nyerere hakutoa sauti yake wakati wananchi walipokuwa wakichukuliwa usiku usiku na kupotea, wala Karume alipokuwa akiwamaliza viongozi wenzake na wala Karume aliposimamia zoezi la ndoa za lazima hasa dhidi ya Waasia wa Kizanzibari.

  Lakini pia Nyerere alikuwa kimya kwa sera nzuri za Zanzibar kama elimu bila malipo, afya kwa wote, maji kwa wote na hata suala la kupewa ardhi wananchi, pamoja na makosa yake, hakuwa akiziunga mkono na kuzipa nguvu stahiki. Nyerere hakuonekana kusaidia kuhimiza mafanikio hayo na tuseme mpaka anaondoka la Zanzibar lilikuwa la Zanzibar na la Tanganyika la Tanganyika.

  Tulimuona Nyerere aliyebadilika baada ya kuundwa kwa CCM na pengine ndio maana hakuwa na sauti wakati Afro Shirazi Party ilipokuwa hewani, ila baada ya kuja kwa CCM Nyerere alisogea karibu zaidi kukemea matukio ya Zanzibar na kwa hilo ndilo ambalo Wazanzibari watamkumbuka Nyerere.

  Wengi tunakumbuka Nyerere alipokuwa mtu wa mwanzo kabisa kusema kuwa njia bora kabisa ya Zanzibar kukabili uwili wake wa siasa, maana siasa za Zanzibar ni uwili wa CUF/CCM ni kuundwa kwa Serikali ya pamoja, lakini wakati huo Dk. Salmin Amour alikataa kabisa wazo hilo.

  Pengine kwa wakati ule sauti ya Nyerere haikuwa kubwa kwa sababu mabaki ya Afro Shirazi Party yalikuwa bado yana nguvu na kwa hakika wengine kati yao walikuwa na uchungu wa Nyerere kuingilia kuizuia Zanzibar isiwe na uhuru wa kuwa na ushirikiano wa kimataifa kupitia Jumuia ya Kiislamu (OIC).

  Na hatujasahau mbele ya Nyerere mabaki ya Afro Shirazi yaliposimama kidete kumkataa Salim Ahmed kuwa Rais wa Zanzibar na mawazo kama hayo ya kuwa Mpemba na Muarabu hatawali Zanzibar kwa hakika mpaka leo yapo na yanapepea.

  Kwa kupinga wito wa Mwalimu kufanya serikali ya pamoja Zanzibar ilikosa fursa muhimu sana ya kutandika msingi mzuri wa siasa za ushindani kwa kuendekeza mawazo kuwa kwa mujibu wa siasa za Zanzibar hasa kwa jicho la kihistoria basi vyama vya CUF na CCM haviwezi kuwa na serikali ya pamoja – ilhali vyama kinzani zaidi duniani tumeona vimeweza kufanya hivyo na mfano wa karibu ni huko Zimbabwe.

  Naamini kama Nyerere angekuwapo basi asingekubali kabisa kuundwa kwa makundi ya vijana yaliyopewa jina la Janjaweed ambayo kila kipindi cha uchaguzi hupewa satwa kubwa kufanya kila watakalo katika kuviza demokrasia na kujenga mazingira ya nguvu ya kukipa ushindi Chama cha Mapinduzi Zanzibar. Na pia asingeridhi kabisa kwa vyombo vya dola kuonekana wazi wazi kulalia kwa upande wa chama tawala.

  Nyerere katu asingekubali kabisa kuwa CCM Zanzibar iko tayari kufanya lolote lile lakini lazima ushindi wa uchaguzi ubakie na zaidi CCM Tanzania Bara ikinyamaza kimya na kubariki matendo hayo, yawe ni ya kupandikiza wapiga kura na kufanya ghilba mbali mbali.

  Angekuwepo Mwalimu asingefurahi kabisa kuona Wapinzani wanafikia mpaka kufanya matumizi ya nguvu kama vile uripuaji wa baruti, ususiaji wa vikao vya Baraza la Wawakilishi na kukataa kushirikiana na Serikali.

  Mwalimu angekuwepo angekasirika sana kuona nchi hii sasa inagawanyika kwa ugomvi wa rasilmali kama vile suala la mafuta, mgawano wa michango ya wafadhili na hata namna ambavyo uchumi wa Zanzibar unavyokabwa koo kwa taasisi kama Mamlaka ya Kodi (TRA) isivyokuwa na huruma kabisa kwa visiwa hivyo.

  Naamini kuwa Mwalimu angekuja Zanzibar mara nyingi kadri ambavyo ingewezekana lakini asingekubali suala la Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi liwe kidonda kwa chama chake na hata Serikali za Zanzibar na Tanzania na kuhakikisha kuwa misingi ya demokrasia iliyowekwa ya kuwa kila raia anaweza kupiga kura apate fursa hiyo na sio kuvizwa kwa visingizio vya kukosa cheti cha kuzaliwa au ruhusa ya Sheha

  Kwa fikra zangu naamini kuwa Zanzibar ina vitu kidogo sana vya kumuonyesha Mwalimu na yeye kuweza kuridhika kuwa visiwa alivyoviwacha vimesonga mbele kidemokrasia na kuhakikisha haki, usawa na umoja. Katika sheria hilo limefanikiwa lakini katika uhalisia au ukweli wa mambo hilo liko mbali sana.

  Mwalimu hangesita kuikemea Halmashauri Kuu ya CCM, moyo na injini ya chama hicho kwa kubariki ya dhulumati ya kisiasa na kiraia inayoendela Zanzibar. Naamini angekuwa zamani ameshakutana na Rais Kikwete na Rais Karume kuwauliza mbona hawachukui uongozi?

  Kama nilivyokuwa nimesema mwanzo kuwa Nyerere hakuwa kipenzi kikubwa cha Wazanzibari. Lakini sasa hivi wanamuhitajia sana maana wanaona wametupwa na Watanzania wenzao kuanzia taasisi za haki za binaadamu na hata wasomi wakubwa wakubwa.

  Wanamkumbuka Nyerere kwa sababu jumuia ya kimataifa inaburura miguu kwa sababu wapiga kura hawaandikishwi kwa kisingizio au maelezo ni kwa ajili ya sheria. Si Watanzania wenzao – wasomi na taasisi za haki za binaadamu na wala si jumuia ya kimataifa inayohoji – hivi kweli sheria ambayo inatenga idadi kubwa ya watu kutoweza kupiga kura ina uhalali gani na uchaguzi unaofanywa chini ya msingi huo unaweza kuwa na uhalali gani?

  Nyerere asinge nyamza. Angesema, akateta, akahoji mpaka akajua mwisho. Kama wangeweza kumpelekea salamu hizo hii leo kaburini kwake wangempelekea ujumbe wa wazi kabisa: Anaweza kumleta Nyerere mwengine aje awasemee? Asaa pengine atasikilizwa kwa kuwa amemleta yeye.

  Lakini sote tunajua haliwezekani. Na ndio maana kumbukumbu ya miaka kumi tokea kufa kwa Mwalimu Nyerere haina maana yoyote ile kwa wengi wa Wazanzibari – hasa wanaoona hivi hivi kuwa nchini mwao wenyewe haki ya kupiga kura haiwezi kupatikana na kwa hivyo kuchagua na kuchaguliwa ni dhana tu kwao lakini haina mashiko.
   
 2. L

  Lampart Senior Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona huyu Sh. Ally Saleh hakumjua Nyerere kabisa.
  Sh. Ally Saleh kila siku anaendeleza fikra na mawazo ya chama chake tu. Leo tena anaona Nyerere angelisaidia? Anyway, NDIVYO MIAFRIKA TULIVYO! Kusambaza chuki tu kila siku. At least Zanzibar hakuna ufisadi kama huo wa Bara!
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuna jambo moja limezuka ambalo kidogo linanifurahisha sana na jambo lenyewe ni hili la kusema laiti Nyerere angekuwepo hili na lile lisingetokea!

  Kwani hayo yote mabaya yaliyotokea huko Zanzibar na kuyaunga kwake mkono hakuona ubaya wake???

  Kwanini Wazanzibari wanataka kuamini kuwa kama Mwalimu angekuwepo asingevumilia kuona hayo yanayotokea hivi sasa Zanzibar???

  Ni kweli Mwalimu alitaka sana Muungano ila inafika hatua sasa huu Muungano umekuwa kero kiasi kwamba sioni kama kuna hatua za dhati zinachukuliwa kuuokoa huu Muungano!

  Binadamu sisi ni flexible sana na Mwalimu ni binadamu na mapungufu yake mwenyewe.Sitaki kusema angekuwepo angehakikisha huu Muungano upo kwa sababu ni yeye aliyesimamia Ujamaa na alikuwepo hadi kushuhudia ukifa.

  Singeshangaa sana kama hata angekuwepo leo akaona Muungano umekufa ilhali na yeye yupo.

  Kwani hakuona machafu yote ya enzi za Mwinyi???Alimchukilia hatua gani?????????

  Tuache ndoto za alinacha!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Oct 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hawa wazenj hawaeleweki, eti wengi hawakumlilia Mwalimu lakini huyu mwandishi anadai kuwa Mwalimu asingevumilia kuona hili au lile! Mimi huwa nawaona wazenj ni watu wa kuangalia vitu negatively tu kuhusu Bara! Pamoja na wao kuajiriwa na kusoma bure bara hilo hawalisemi! Nimesoma na wazenj wengi ambao wamepata elimu hiyo almost bure na wamekuwa treated equally na wabara! Bara imekuwa jalala la kutupia madhaifu yao yote hata pale isivyostahili!
   
 5. L

  Lampart Senior Member

  #5
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Dear Nd. Kevo,

  Umesahau Nyerere alimfanya nini Mwinyi pale Kilimanjaro Hotel? Au siku zile mwezetu ulikuwa nje ya nchi ukila kuku kwa mrija?
  Unajua Mwinyi mara ngapi aliuacha urais kwasababu ya maneno ya Nyerere na akawa anarejeshwa na Thabit Kombo?
  Nani kwani aliyowasukumia kaburini akina Hanga na Othman Sherrif?
  Nyerere alikuwa hataki upuuzi, lakini kuhusu Zanzibar asingeliingilia hivyo kama huyu mwandishi anavyodanganya na hata kama angeliingilia basi SMZ isingelimsikiliza kwa yote. Mbona serikali ya mseto aliyokuwa akiitaka haikuwa?
  Hao mafisadi unadhania wangelikuwa na immunity hii ya leo? Chenge kuhusu radar zamani angelikuwa Keko au angelikuwa keshapotea kabisa. Nyerere hakuwa mtu wa mchezo hata kidogo!!
   
 6. L

  Lampart Senior Member

  #6
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nd. Buchanan,
  >wamepata elimu hiyo almost bure<
  Usiseme bure. Maneno hayo akiyasema mkoloni siku zile. Huku anakunyonyeni na huku anajidai kuwa anatoa services bure. Zanzibaris deserve more from Mainland than what they get now.
  We will NOT be better off without Zanzibar!!!
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono mia mia kwa maoni yako! Mwandishi wa makala hii namuelewa na naamini amefikia pahala pa kukata tamaa kuona utawala bora visiwani na hivyo anaishi na LAITI,
  Kifo chaq Nyerere ni miakan 10 nyuma na tatizo linalowakuta Wazanzibari kwenye Muungano na hata utawala wa SMZ ni zile zile hata miaka mingi Nyerere akiwa yu hai.
  Iwapo mikataba inayolalamikiwa ikiwa imetiwa saini wakasti wa uhai wake, harakati za kudai haki ya Zanzibar ni yeye Nywerere alikuwa kinara wa kuzizima tunahitajia nini.
  LA HASHA WAZANZIBARI WANAONA BORA NYERERE ABAKI AMEPUNZIKA HUKO ALIKO NA WALA HAWAHITAJI MTU KAMA YEYE!
   
 8. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Hapa ndipo inapoonesha hata Wasomi wanaojidai kuwa ni wasomi hawajaelimika. Hivyo huyu Bwana anashangaa kitu gani juu ya attitude ya Wazanzibari wakati huo wake ndio mtazamo wa wengi wao!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Oct 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapa ndipo ninapokuwa tempted kuamini kale kausemi "changu changu, chako changu!" Kaazi kweli kweli! Ndio maana wanaupenda Muungano kwa ndani, nje ni blah blah tu!
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  sijuwi kama unaelewa unachokizungumza kama wazanzibar wanasoma bure bara si kwa hisani ni kwa taratibu za kinchi, unajuwa kuwa elimu ya juu ni suala la Muungano?
  Haikuwa na maana kuwa kabla ya hapo zanzibar hakukuwa na wasomi, ustake kufanya kama bara inawajibu fulani wa kihisani juu ya zanzibar, watu wanafuata taratibu ndugu. Kama wazanzibar hawakumlilia Nyerere wanasababu zao zinahitaji kuheshimiwa, nini kazi? kuna vijana wangapi kutoka bara wamo kaitka vikosi vya SMZ huku wazanzibar wenyewe wakiachwa? kuna nafasi ngapi za JWTZ zinakuja kwa wazanzibari wanaozipata ni wabara wanaotoka au wanaokuja kujiandikisha huku..kwa kupitia migongo ya jamaa zao huku...don't talk about equality you make me poke...
   
 11. M

  Mchili JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Why do you think Zanzibaris deserve more from mainland? Are you sure we won't be better off without Zanzibar?
   
 12. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wazenji wanasoma bara bure?Hebu weka maneno yako sawa, nafikiria zenji unakuja kusoma Dar hapo university kwa mkopo.
  Pili hata kama miaka ya zamani walipewa elimu bure, unaonekana kama kufikiria kama wanasaidiwa badala ya kufikiria kama ni haki ya kimuungano kupewa elimu hiyo.

  All in all, muungano huu wazenji hawataki hata kuusikia....sijuwi watanganyika wanang'ang'ania nini na wanafaidika nini na huu muungano.Kama tutakumbuka Mwalimu alisema siku wazanzibari wakiwa hawataki wanaruhusiwa kutoka kwenye muungano, nafikiria wazenji hizo siku zishafika au ziko njiani...

  Watanganyika na Nyerere wamekaa kama wamerogwa, enzi za Nyerere hata chakula kulikuwa hakuna watu wakila sembe la njano.Mwinyi ndio afadhali kaja kuondosha hivyo vioja vya Mwalimu vya Ujamaa....au kafanya nini Nyerere katika kuleta maendeleo ya Tanzania au Tanganyika?Mie naona baada ya kutoka madarakani ndio watanzania wameanza maisha, kwa ufupi naweza kusema Nyerere amelostisha nchi hii kwa kuitia kwenye Ujamaa kwa muda wote wa miaka 22 ya utawala wake.Na hiyo ni fact, penda au usipende...kiongozi anapimwa kwa maendeleo, na hilo hakulifanya Nyerere.Uhuru alipewa kwenye karatasi, hata zenji viongozi walipewa uhuru sawa na alivyopewa Nyerere....hata kiongozi yeyote angelikuwepo angepewa tuu hiyo karatasi ya uhuru!
   
Loading...