Mzimu wa Lissu ndio tatizo kubwa kwa sasa kuliko mtu yeyote hapa Tanzania

Lissu angeitumia kwa ustadi mkubwa kete ya 2020 angeshinda uchaguzi mapema sana maana Marekani wapo nyuma ya wapinzani kwa 100%

..Marekani na washirika wake wako INDIFFERENT / HAWAJALI kinachoendelea hapa Tz.

..kusini mwa AFRIKA chama kinachojua machungu na misukosuko ya wapinzani kuungwa mkono na Wamarekani ni chama cha ZANU cha Zimbabwe.
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia mia moja, cdm wasimame kama chama pekee na mgombea awe Tundu Lissu. Ni ukweli usioacha shaka kuwa Lissu ana mvuto na uwezo mkubwa wa kujenga hoja, huyu ndio mgombea pekee anayeweza kunifanya nipige kura, na ndiye mgombea anayeweza kurudisha hamasa ya siasa iliyouliwa na Magufuli kwakuwa hawezi siasa za ushindani. Huyu ndiye mgombea wa upinzani anayeweza kuamsha hamasa ya umma kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Jambo pekee watakaloweza ccm ni kumfunga jela na sio zaidi ya hilo.
Ninakuhakikishia kwamba hilo la Tundu Lissu ndilo linalowanyima usingizi huko ndani ya CCM.

Uwe na hakika kwamba watafanya kila lililomo katika uwezo wao kuzuia asiweze kuwa mgombea.

Pamoja na hilo la kuzuia pasiwepo na uchaguzi ulio huru na wa haki, pengine jambo la pili kwa umhimu kwao ni kumzuia Lissu asigombee.

Haya mawili yanatakiwa yapigiwe hesabu kubwa kuhakikisha kwamba CCM hawawaburuzi waTanzania juu yake.
 
Muda wa kupangua hoja za wapinzani hauta kuwepo. Hili ni tatizo kubwa sana. Kwahiyo njia pekee iliyobaki Ni kuiba kura .time huru ya uchaguzi ni muhimu
 
..kifungo kitawasaidia kama ni cha muda mrefu, miaka 15+.

..bahati mbaya kesi alizonazo TL ni za tuhuma ndogo-ndongo.

..sasa baada ya kujaribu kumuua na kushindwa, wakimfunga kwa hivi vikesi vyao visivyo na kichwa wala miguu, umaarufu wa TL utaongezeka.
Haijalishi mkuu.

Unataka kujisahaulisha maajabu ya CCM ya leo?

Wewe unaloona haliwezekani au ni la aibu hata kulionyesha mbele za watu, kwao lililo mhimu ni matakwa yao, basi!
 
Lissu angeitumia kwa ustadi mkubwa kete ya 2020 angeshinda uchaguzi mapema sana maana Marekani wapo nyuma ya wapinzani kwa 100%
Sijui una maana gani mkuu 'technically' kwa hii ya "Marekani wapo nyuma ya wapinzani kwa 100%"?

Kwa wenye ufahamu, hilo ni kama 'nzi kuchafua mchuzi'.

Tafakari kidogo juu ya hilo.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom