leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,585
- 3,179
Kwa hali ya kisiasa ilivyo hapa Tanzania kwa sasa Tundu Lisu ni tatizo kubwa kwa CCM kuliko ilivyo kuwa kwa Lowasa kwenye uchaguzi wa mwaka 2015,lakini kuung'amua na kuukubari ukweli huu inahitaji jicho la tatu.
Wapo wengi wanajiuliza kwa nini CCM inaonekana kuwa na wasiwasi mwingi mwaka huu wa uchaguzi licha ya kuwa inajivunia kutekeleza ilani yake ya uchaguzi pengine kwa kiasi kikubwa kuliko wakati wowote.
zipo sababu kadhaa ninazoziona Mimi kama;
kete ya mwisho na ya msingi ni kumzuia kugombea au la kuvigawa vyama vya upinzani visiungane na mamluki Kama Ben maembe wamwagwe upinzani.

- Katika kipindi hiki cha miaka miaka Minne CCM imejiweka mbali na wananchi Kuliko wakati wowote ule,hasa baada ya kuteua makada WA chama kushika nyadhifa za kiserikali, mbwembwe za makada hawa na unyanyasaji wa raia huku wakijinasibisha na chama,ulikiondoa chama kuwa cha kisiasa kwa ushawishi na kuwa chama dola cha kimabavu hivyo kuogopewa na kupendwa kinafiki.
- Kuzuia mikutano ya kisisa kwa muda mrefu na kubana Uhuru wa habari kumewafanya wananchi kuwa na kiu ya kujua upande wa pili,hii itafanya mikutano ya wapinzani kuwa na mafuriko ya aina yake na watakacholishwa hapo kitakuwa kipya na CCM hawatakuwa na muda WA kutosha kupangua hoja za wapinzani.
- Kugombea kwa Lisu katika nafasi ya urais na hasa Kama atakuja Kati ya Mwezi April mwishoni au Mei, Watanzania kwa asili yao ni watu wanaomsubiri masihi wao wasie mjua kumbukumbu zipo,Mrema 1995, Lowassa 2015, Then who's next? Bila Shaka ni Lisu na CCM wanalijua hili. Na sababu kubwa ya wananchi ni kuhitaji mtu mtenda haki, shupavu na jasiri. Kuumizwa kwa Lisu na kuwepo kwake nje ya nchi kwa mda mrefu atakuwa mtu mpya kwa wakati sahihi na kila mtu atataka kumsikiliza na ninaamini atavuta watu wengi kuliko Lowassa 2015
- Uwezo wa Lisu kujieleza ni mzuri hili halina ubishi, ninachokiona kwa uwazi agenda ya uchaguzi mwakani huu itakuwa ni haki za binadamu. Kutupwa kwa katiba mpya,makosa yaliyofanywa na viongozi wa chini kuhusiana na haki za watu yataifanya CCM kujitetea kwa mda mwingi kuliko kuelezea sera zao.
kete ya mwisho na ya msingi ni kumzuia kugombea au la kuvigawa vyama vya upinzani visiungane na mamluki Kama Ben maembe wamwagwe upinzani.