Mzimu Wa Gadafi unavyompa shida Sarkozy Ufaransa.

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
300
422
[http://dsh7tu7hoh3mx]

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy aendelea kushikiliwa na polisi

21 Mar 2018, 04:30 pm| By Azam NewsUHALIFU

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameonekana akiwa na Polisi nyumbani kwake leo asubuhi mjini Paris na kisha kuondoka na maafisa hao ambao wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo.

Inaelezwa kuwa baada ya ukaguzi uliofanyika kwenye makazi yake, Sarkozy amerejeshwa Polisi kwa mahojiano zaidi ambako amewekwa mahabusu tangu jana ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu kashfa inayomkabili ya kupokea mamilioni ya fedha za kampeni za urais kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya, marehemu Muammar Gadhafi kinyume cha sheria.

Chanzo kimoja kimelitaarifu shirika la habari la AP kuwa Rais wa zamani wa Ufaransa anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Nanterre mjini Paris.

Polisi wanachunguza uhalali wa fedha alizotumia katika kampeni za kuwania urais mwaka 2007 ambapo mara kadhaa Sarkozy amekuwa akikana shutuma hizo.
 
Ina maana Viongozi wa Ulaya wamezidiwa akili Na kina Magu
Wenzao wana kinga ya kutoshtakiwa
 
Gadafi alikua kichwa Na Hela ilishakaa sehemu Yake ingawaje maono yake naona tayari wachina wameanza kuyafanyia Kazi kwa kutumia fedha yao kununulia mafuta ghafi
 
Back
Top Bottom