Mziki wa Rap na Ufumbuzi wa Somo la Hisabati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mziki wa Rap na Ufumbuzi wa Somo la Hisabati

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by IshaLubuva, Dec 17, 2008.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2008
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna wakati mwingine unaweza kusikiliza maelezo au maoni ya mtu fulani halafu maoni/maelezo hayo yakakupa manufaa au yakakupa madhara ya kudumu. Hivyi ndivyo somo la Hisabati na wenzake wa Sayansi ambavyo wamekuwa wakihubiriwa kuwa ni wagumu na matokeo yake wanafunzi wengi kuyaogopa na kuamua kutoyasoma. Lakini kitu cha msingi ambacho tunatakiwa kukizingatia ni kwamba binadamu, kama ambavyo tunavyoitwa majina tofauti, ndivyo na akili, uelewa, busara, fikra na vitu vingine vyote tulivyoumbwa navyo tunatofautiana. Ni kweli mtu mmoja anaweza kuwa na mfanano na mtu mwingine katika baadhi ya vitu hivyo lakini asilani hatuwezi kuwa na mfanano wa asilimia 100 kwa 100.

  Ugumu wa somo la Hisabati kwa Mwanafunzi mmoja unaweza kuwa unasababishwa na mambo kadhaa; mathalan, Mwanafunzi huyo anaweza kutokea kutompenda Mwalimu wa somo hilo kwa sababu za hulka ya kibinadamu, au mwalimu kutokuwa na mbinu makhsusi za kufundishia somo, n.k. Sasa Mwanafunzi huyo akisema somo la hisabati au sayansi ni gumu na Mwanafunzi mwingine anayekuja nyuma yake akachukulia hivyo, atajikuta anaathirika pasipo sababu za msingi. Sijui ni Mwanafunzi gani aliyeanza kusema kuwa somo la Hisabati/Sayansi ni gumu na hivyo kuwafanya fomu wani wote wanapoanza kusoma kuyaogopa masomo hayo.

  Sasa Suluhu Imepatikana. Huko Marekati katika Mji wa Califonia, Mwalimu mmoja kwa jina akiitwa Kajitani[​IMG] amegundua namna ya kuwafanya wanafunzi wake kulielewa somo la Hisabati na mwisho wa siku kupasua pepa. Mwalimu huyo kama ilivyo kwa Walimu wengine wa Hisabati alikabiliwa na tatizo la Madenti wake kutopandisha nondo za namba alizokuwa akiwamwagia. Lakini wakati wa utawala binafsi, aliwasikia Madenti walewale wakifloo mistari ya JeyZii kama hawana akili nzuri hivi. Ticha huyo baada ya kurudi homu, akaskuti na kutona na mistari ya Rap za somo la Namba. Kesho yake kwenye kipindi aliingia kama kawa na kuanza kufundisha. Si unajuwa tena Maticha wengi wa somo la namba wanavyokuwaga na Mkwara (Kwa wenzangu waliopitia pale Mlimani naamini mnamkumbuka Ngowi wa ST 100), alianza kufindisha akiwa siriazi; lakini baada ya muda akabadili mapigo na mambo yakawa hivi:

  "Sit back relax let out a little smile because the rapping mathematician is the hot new style."

  Akaendelea kuchana mistari kama hivi;

  "No need for instruments or radio stations because I can break it down like order of operations." Lecture ikawa ni Rap ya namba hadi dakika 80 zikaisha.

  Na haya ni maoni ya baadhi ya Madenti wake:
  "I think he's weirder than me,

  "He's like one of the best teachers I have ever had,"

  Mwalimu huyu alitunukiwa zawadi ya Mwalimu wa mwaka katika mji wa Califonia

  Habari hii inapatikana katika When Rhythm Meets Arithmetic, CBS Evening News Meets The Teacher Who's Gotten Students To Rap Their Heads Around Math - CBS News

  Changamoto kwa Maticha wetu wa masomo ya Namba, Fizikia na Kemia (ambayo inaaminika kuhitaji kreming kapasiti ya hali ya juu) kuja na singo za topic mbalimbali ili kuwavutia na kuwawezesha madenti wa leo ambao sikuhizi kila wanapokuwa na fursa ndogo wao utawaona wakirusha mikono kama wendawazimu kumbe wanachana mistari ya Bongo Fleva
   
 2. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Huyu Ticha ni Kipanga kweli, manake amegunduas dawa ya kuwafanya hawa vijana wa kizazi hiki waelewe namba ni kuwadumbikizia materials kwa staili ya maisha halisi wanayoyaishi kwa sasa. Ni kweli mara nyingi mtu ni rahisi kukumbuka kitu au tukio ambalo lilikufurahisha au kukuchukiza sana. Na kwa vile vijana wa leo wameonekana kupenda sana Bongo Fleva na kwamba mwanafunzi hata wa Vidudu/Chekechea anaruhusiwa kurekodi na kupanda Jukwaaani, kama yule mtoto wa Kinyamwezi anayeishi DSM, sijui anaitwa Rehema vile; itakuwa vema walimu wetu nao wakachukua staili hiyo ya kushusha materia kwa kufokafoka.
   
Loading...