Mziki wa gwaride la chadema nape nauye atauweza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mziki wa gwaride la chadema nape nauye atauweza?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DSN, Apr 12, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  MZIKI WA GWARIDE LA CHADEMA NAPE ATAUWEZA ?

  Ni matumaini yangu mabadiliko ya uongozi wa sekretarieti ya CHAMA CHA MAPINDUZI ni mwanzo wa siasa mpya zenye mwelekeo tofauti,na ule wa sekretalieti iliyopita.

  Kwa vyama vya upinzani hasa chama cha CHADEMA, mabadiliko ya uongozi wa juu wa CCM yataleta hamasa na shauku nyingine jinsi ya kukabiliana na changamoto za kuhamasisha na kuibua ushawishi kwa wananchi, kwenye dhumuni la kupata support na wanachama wa kuwaunga mkono.

  Je Katibu MWENEZI NA ITIKADI mpya Kijana NAPE NAUYE ataweza gwaride la CHADEMA?

  Mimi binafsi namkubali Nauye kama kijana ambae alijitanabaisha awali bila kuficha wala kubugia maneno yeye na ufisadi ni maji na moto, hilo kila mtanzania aliye kijana awe ni kambi CCM ama chama kikuu cha upinzani TANZANIA CHADEMA wote hilo wanalijua. Yaani kwa umri wa kijana wa kizazi kipya ni kamanda mpiganaji.

  Natumia neno kamanda Mpiganaji kwa vijana wa kitanzania neno hilo kamanda Mpiganaji , linamaana kubwa, likibeba ujumbe wa Kijana mwenye kujituma kupambana kwa kwenda mbele na kwa bidii zake mwenyewe bila kusukumwa na mtu ama kumtegemea mtu,yaani mpambanaji anasukumwa na dhamira [Nafsi].

  Kwa vijana wa kileo kuna wapambanaji juu ya mwelekeo na utashi wa kuiona TANZANIA MPYA yenye NEEMA kwa wote.Wapambanaji hawa kwa sasa wako kila kona ndani ya TANZANIA hii, wako kwenye vyama vya kisiasa,wasio na vyama,wenye uzalendo nk.

  Je Nauye ataweza gwaride la Wanachadema wapambanaji wenye kiu ya kuona mfumo mzima wa kiutawala ulio chini ya CHAMA CHA MAPINDUZI ukitoka na kuachia ngazi kwao wao waweze kutawala na kuwapa maendeleo na ustawi Watanzania likiwa ndio lengo lao kuu ambalo tayari liko mikononi mwa CHAMA CHA MAPINDUZI.

  Nauye kama Mpiganaji alikuwa kiungo dhidi ya WANACCM na CHADEMA kwa kigezo cha UFISADI ambacho yeye ni dhahiri alikua mstari wa mbele.

  Sasa kakabidhiwa dhamana ya kuirudisha CCM kwenye macho ya watanzania haswa vijana ambao wengi wao [Kwa sasa ni mashabiki na wapenzi wa chama cha CHADEMA].

  Je amajipanga kwa kuzingatia hali halisia katika kueneza ITIKADI YA CCM haswa kwa KIZAZI KIPYA ambacho wengi wao ndio wapiga kura wa 2015.Ni mwanzo na mwelekeo mpya wa strategies zenye nguvu na ubora usio na shaka katika kushawishi na si kulazimisha kukubalika katika kupata wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHAMA CHA MAPINDUZI, na kujenga wigo mpana wenye matumaini ya ustawi ndani ya chama na nje ya chama kwa ubora utakao kubalika bila shaka.

  Je ataweza kuwabadili wazee [Viongozi wakuu wake] ambao bado wana amini kwenye mfumo wa Seniority and We [usisi], na sio Transparency, Performance, Credibility, Integrity, and Democracy,ambayo ndio taswira [Vision ] ya vijana wa ulimwengu wa sasa.

  Je atakuwa huru kutumia nguvu ya ujana [Youthhood] yenye Positive direction ambayo alishaionyesha toka awali juu ya vita vya mafisadi, bila kupigwa spid governor.Manake kwa generation ya sasa ya DOTCOM GENERATION [DG] kitendo cha kupangiwa bila kushirikishwa na kupigwa kalenda kwenye maaamuzi yenye kuitaji mwitikio [Respond] ya haraka ni kukaribisha mtafaruku usio na tija.

  Je ataweza kujibu hoja za kisomi za makamanda wa CHADEMA, ama atakusanya Makamanda wa CCM,kuandama kama strategy kujibu mapigo ya CHADEMA , ni matumaini atajitayarisha kisomi na kutayarisha timu ya wasomi tena waelevu [Intellegent] sio bora wasomi , manake hata waliomkaanga umoja wa vijana walikua wasomi. Wasomi vijana walio waelevu watamsaidia kimkakati kuandaa mbinu, na maarifa ya kupata wanachama, wapenzi na mashabiki wa chama chake kutoka kada tofauti tofauti. Lakini pasi kuogopa kivuri cha waelevu manake ndio umekua ugonjwa wa chama kuogopa watu wenye upeo mkubwa wa kuelewa mambo, kitu ambacho chama cha CHADEMA kimetumia udhaifu huo kujikusanyia wapenzi, wanachama, na mashabiki toka katika kada ya wasomi [Haswa vyuo vikuu na Mashirika].

  Je Nauye ataweza kuibua taswira [Vision], mipango [Plan],na kutoa ushawishi juu ya mwelekeo wa chama na nchi kwa lugha rahisi, popote pale bila hofu, mashaka wala aibu na kuwa tayari kuwajibika kwa lolote lile.

  Je ataweza kuwashawishi wazee waaamini kuwa sasa hivi ama dunia ya leo ya zama za utandawazi [Globalization] kitendo cha mikakati yoyote isiyo ya haki ya kuhujumu UMMA ama CHAMA CHA KISIASA ni kitendo hatarishi dhidi ya USALAMA WA TAIFA, Chochote kile kisichofaha kwenye jamii ni vyema kikawekwa mbele ya uso wa jamii na umma ukatoa tathimini yake ambayo kesho na kesho kutwa ndio silaha ya maamuzi halali ya jamii au umma.

  Je ataweza kuwashawishi wazee kutambua kuwa TANZANIA ya TANU NA AFRO SHIRAZ iliyokuja Kuzaa CCM yenye enzi ya zama za chama kushika hatamu ziko ukingoni au zimekwisha,na sasa wananchi ndio Wamiliki wa MADALAKA na CHAMA CHA KISIASA kinaazimwa MADALAKA hayo na Wananchi chini ya Sanduku la kura ya maoni. Kama Mwalimu alivyopata kusema CHEO NI DHAMANA.Vivyo hivyo MADALAKA au NGUVU YA KUTAWALA ni DHAMANA iliyopatikana toka kwa wananchi, na si mali ya chama chochote kile, Vyama vya Kisiasa ni Wapangaji tu, ndani ya kila miaka mitano uchaguzi kodi ya upangaji inakua imekwisha

  Je ataweza kuwakumbusha na kuwaimiza viongozi wa CHAMA CHA MAPINDUZI kuwa wanyenyekevu kwa wapiga kura wao na kuwashirikisha kwenye maamuzi ya hatima ya TANZANIA yao ya leo na kesho.

  Safu ya Chadema imejipanga, ilo liko wazi,aitaji mtabiri bali yaitaji ukweli wa nafsi kukubali na kusema hiyo yote ni changamoto, na changamoto si vita au uadui bali ni vichocheo kumpa nguvu muhusika kuongeza bidii ili kupata matunda na matokeo yaliyo bora kutokana na chamgamoto zilizomkabili kama sehemu ya kumuonyesha njia sahihi ya kupata majibu sahihi.

  Nape kwa staili ya uwazi ni dhahiri ni muumini wa sera za DEMOKRASIA. LAKINI JE KWA TIMU MPYA ambayo wengi ni CONSERVATIVES ataweza fungate hilo la WACONSERVATIVE,ambao wanaamini kila jambo likajadiliwe kwenye vikao halali husika vya kichama katika ngazi husika.

  Nape Mziki wa Chadema Unakuitaji Ujipange sana sana sana.


   
Loading...