Mziki mkubwa kanisani utasema hawajui kama huu ni mwezi mtukufu wa Ramadan kwa waislamu

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,080
Wanabodi kuna kanisa moja hapa Wilayani Ruangwa mkoani Lindi Jamaa wamefungua mziki kwa sauti kubwa sana. Nimebaki tu nashangaa hivi wanajisikiaje kufungua mziki kwa sauti kubwa kiasi hiki?

Au Wana furaha gani zaidi ni Bora wangeweka sauti kubwa wakiwa wanahubiri lakini mbaya zaidi wanaweka tu miziki ya Singeli Bongo Fleva na miziki ya Ulaya, Kama hiki kwa kweli siyo vizuri kwa maoni yangu sijui wengine.
.
Shindu Namwaka, Ruangwa Lindi Tanzania muda huu.
 
Wanabodi kuna kanisa moja hapa Wilayani Ruangwa mkoani Lindi Jamaa wamefungua mziki kwa sauti kubwa Sana,nimebaki tu nashangaa hivi wanajisikiaje kufungua mziki kwa sauti kubwa kiasi hiki?

Au Wana furaha gani zaidi? ni Bora wangeweka sauti kubwa wakiwa wanahubiri lakini mbaya zaidi wanaweka tu miziki ya Singeli Bongo fleva na miziki ya Ulaya, kitendo kama hiki kwa kweli siyo kizuri kwa maoni yangu sijui wengine.
.
Kanisa hilo mara nyingi ibada zao ni usiku yani kuanzia saa moja 1 usiku hadi saa saba 7 za usiku wao ni maubiri tu Redio yao wakiwa wamefungua kwa sauti ya juu dah.
.
Shindu Namwaka, Ruangwa Lindi Tanzania muda huu #tujikinge na tujilinde na Corona
 
Kwenye title umesema "Kwani hawaoni ni mwezi mtukufu wa Ramadan kwa waislamu". Kwahiyo ikiwa ni mwezi mtukufu kila kitu kisimame?
Kupigiana kelele sio poa kwa ujumla ila kusema sijui mwezi mtukufu hoja yako imekosa mashiko.
Nimeongezea tu nyama
 
Ni Ujinga tu kudhani kwa resma au Ramadhani ina mhusu kila mtu kuna watu kama mimi hatuna dini..

Sasa kama hatuvunji Sheria za nchi kwanini tuwe affected na kushinda kwenu njaa?
Ubinadamu pia upo ni sawa ila tusilazimishane sasa
 
Wanabodi kuna kanisa moja hapa Wilayani Ruangwa mkoani Lindi Jamaa wamefungua mziki kwa sauti kubwa Sana,nimebaki tu nashangaa hivi wanajisikiaje kufungua mziki kwa sauti kubwa kiasi hiki? au Wana furaha gani zaidi ni Bora wangeweka sauti kubwa wakiwa wanahubiri lakini mbaya zaidi wanaweka tu miziki ya Singeli Bongo fleva na miziki ya Ulaya, Kama hiki kwa kweli siyo vizuri kwa maoni yangu sijui wengine.
.
Shindu Namwaka, Ruangwa Lindi Tanzania muda huu.
Kanisa linapiga "Singeli, Bongo Flava na miziki ya Ulaya..."
Napata mashaka sana na shutuma zako! Si ajabu una chuki tu na kanisa au imani ya kikristo!

Kanisa gani linapiga miziki aina hiyo uliyotaja!? Kama hoja yako ilikuwa ni kelele mtaani kwenu ungeenda moja kwa moja bila kuingiza Imani za wenzio!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ki ustaarabu makanisa yanakuwa na odium ni sound proof. Hata mziki uwe mnene hakuna usumbufu kwa jirani.

Wakristu wakisema kuna azana inawaamsha lakini asana ni dakika tano tu imekwisha. Tena wengine ndiyo alarm yetu ya kuwa hi kazini.
 
Oya umeshindwa kurekodi hiyo miziki tuhakikishe

Kabla hatuja toa comment
 
Kama funga yenu ni kwa ajili ya Mungu na wale wanaopiga mziki kanisani wanamtukuza Mungu yuleyule, japo kuwa umesema kuwa wanapiga nyimbo za bongo fleva lakini hiyo umechomeka wewe mwenyewe,kwa kuwa kanisani hakuna kitu kama hicho, wasiwasi wako nini wakati wote mko kumuomba na kumsifu Mungu yuleyule?.
 
Back
Top Bottom