Mzembe, mvivu huona kila kitu anaonewa kwake kulalamika ndio silaha kuu na huyu ndo Mtanzania

Tatizo kubwa la waTanzania hatuna nidhamu ya kila kitu kwenye maisha yetu ya kila siku......

Nidhamu ni kitu muhimu sana kwenye mzunguko wa maisha ya mwanadamu.......
 
Watanzania wengi ni wavivu na hawapendi kufanya kazi....ukijituma na kutimiza wajibu wako kazini utaonekana kihere here na kinachofuata ni kupigwa majungu na kuzushiwa mambo ya kijinga mpaka ofisi uione chungu........
Ndio tubadilike Sasa sio boss, sio mwenye Mali, sio mtumwaji, wote tuwe productive kwa kila jambo
 
Mafanikio yako na mwanasiasa yana link.
Check ishu ya tozo, kupanda kwa bei za vitu,kesi za uhujumu uchumi tajiri anafunga investment baada ya kufilisiwa na mwanasiasa watu wanapoteza ajira
 
Umasikini wetu ni matokeo ya malezi yetu.
Wazazi wengi hawana elimu ya malezi ya watoto.
Hulea watoto kama bata tu.
Weupe wanajua jinsi ya kuwalea watoto wao kuziona fursa.
 
Mkuuu kuna watu wanapambana sana kufanya kazi kweli kweli lakini ofisi nyingi hazithamini hasa serikali yetu.Binafsi mm niliamua kujituma kweli kweli kwenye kazi yangu ya ualimu ,nafundisha hisabati mazingira yenyewe yakijijini ,unafundisha mda wote inatumika hadi wekend,unatoka kazini saaa 12 ili wanafunzi waweze hisabu.

Unaangaika kila mwaka upate A na B za hesabu kwa kujila kweli kweli lakini no motisha na asante ,yaani akili yako myingi unaiwekeza kwenye kazi za watu wewe unasubiri ukistaafu ndoo ujenge kwasababu salary ni kidogo.

Sasa nikaamua kuwa kama wengne ambao akili yao muda mwingi wanawaza ya kwao na wanafelisha kweli kwenye masomo yao,mambo yamebadilika kwangu angalau lakini kazini kumekwama hakuna cha A wala B.
Kupambana sio kupata,kuna wamepambana Sana tangu ujana hadi uzee na awajatoka
 
Mabadiliko huanza na wewe Kama hyo ofisi unataka ibadilike lazima na wewe ubadilike kivyovyote vile mkuu.

Funga mkanda mkuu
Hakuna motisha Hakuna mabadiliko.
Unajituma unazalisha mwanasiasa ndie anaenda zitumbua kiulaini bila jasho
 
Hakuna motisha Hakuna mabadiliko.
Unajituma unazalisha mwanasiasa ndie anaenda zitumbua kiulaini bila jasho
Sio lazima kumfanyia mtu kazi(kutumwa) Bali unaweza kujifanyia kazi(kujituma).

Kuna tofauti ya kuamka asubuhi nakwenda kwa bwana mkubwa unapewa maagizo unaenda mtaa jioni unarudi na million 5 zote hzo n za be mkubwa usiku unaenda kulala ukiwaza yeah kuamka uende kwa bwana mkubwa.

Bali Kuna wengine asubuh wanaamka wanaanza kutafuta jion ikifika Ana elfu tano hyo n yake na usiku anaenda kulala huku akiwaza kesho ajiongeze vipi ili apate zaidi ya jana.
Screenshot_20210815-180743.png
 
Mafanikio yako na mwanasiasa yana link.
Check ishu ya tozo, kupanda kwa bei za vitu,kesi za uhujumu uchumi tajiri anafunga investment baada ya kufilisiwa na mwanasiasa watu wanapoteza ajira
Wewe ndo umeamua kumuachia kazi ya kuleta ugali mezani mwanasiasa kwangu Mimi BIG NO!
 
Back
Top Bottom