Mzee Wilbar Smith asema Afrika inarudi ilikotoka-kabla ya wazungu kuja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Wilbar Smith asema Afrika inarudi ilikotoka-kabla ya wazungu kuja!

Discussion in 'International Forum' started by Richard, Apr 6, 2009.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Wilbur Smith ni mmoja wa waandishi maarufu duniani. Mpaka leo hii alikuwa ameandika vitabu 31 maarufu kama vile When the Lion Feeds, The River God na The Triumph of the Sun, ambacho kimetafsiriwa katika lugha 26.

  Vitabu vyote hivi vina mandhari ya bara la Afrika na mzee huyu ambae alizaliwa Zambia miaka 33 iliopita anapenda kuandika kuhusu bara hilo kuzingatia kwamba amewahi kuwa mshauri wa masuala ya kodi katika serikali ya Zambia.

  Leo jioni hii mzee Smith amezindua kitabu kipya pale Waterstones, duka maarufu la vitabu lililopo sehemu iitwayo Piccadilly mjini London.Mimi nikiwa mmoja wa wapenzi wa vitabu nilipata nafasi ya kwenda kuona kitabu ambacho kinaitwa Assegai.

  Tafsiri sahihi ya assegai ni mkuki na kitabu hiki kinahusu enzi zile za ukoloni ambapo askari wa zamani Leon Courtney ambae amekuwa muwindaji anaingia urafiki na mfanyabiashara tajiri kutoka Ujerumani bwana Count Otto Von Meerbach ambae ana kiwanda cha kutengeneza magari na ndege.

  Lakini baadae baba mkubwa wa Leon anaeitwa Penrod Ballantyne ambae ni kamanda wa jeshi la Afrika Mashariki anamshauri Leon kumpeleleza Count Otto Von Meerbach na kumpelekea habari.

  Badala yake Leon anampenda mke wa Count Otto Von Meerbach aitwae Eva Von Wellberg. Kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia Leon anashauriwa na Count Von Meerbach kuandaa uasi dhidi ya jeshi la Uingereza la Afrika Mashariki kutoka kwa upande wa Ujerumani kwa kuwashirikisha wanajeshi wa zamani wa makaburu walioshiriki vita maarufu kama "Boer War" nchini Afrika Kusini.

  Leon baadae anaachwa kwenye mataa na tena anamwona Eva Von Wellberg akirudi Afrika na mtu mwingine na Leon anatafuta kujua ukweli kuhusu bibie Eva Von Wellberg kwamba ni nani na amejificha nyuma na sanamu kwa minajili gani.

  Sasa mzee Smith akanishanga kidogo kwa kauli yake kuhusu afrika pale alipokuwa akijibu baadhi ya maswali na moja ya maswali hayo lilikuwa swali kwamba je yeye ana imani na bara hili ambalo yeye amekua na kuishi humo?

  Mzee huyu akajibu kwamba Ulaya Magharibi inavyolichukulia bara la Afrika si vile Waafrika wenyewe wanavyolichukulia bara lao kwa maana ya kuwa bara lenye neema na mambo yote mazuri na kwamba waafrika wanafaidi matunda ya kuwa na bara hilo.

  Akaendelea kwa kusema kwamba, waafrika wataendela kulishughulikia bara lao kuelekea mwisho wake na kulirudisha bara hilo kule lilikotoka yaani kabla ya wazungu hawajatia mguu barani humo kwa maana kwamba kutakuwa na mifumo ya ukabila zaidi, udikteta zaidi kuliko mifumo ya kidemokrasia na akamalizia kwa kusema kwamba hio ndo hali ambayo waafrika wanaridhika nayo.

  Ninasikitika sana, kwa sababu nikiangalia habari zote zihusuzo ufisadi, rushwa na midubwana mingine nikabakia natafuta majibu.

  Kwa wale walioko Marekani na Canada kitabu hicho kitachapishwa tarehe 12 April, Norway tarehe 20 May,Denmark tarehe 25 June, na Netherlands tarehe30 July 2009.
   
  Last edited: Apr 6, 2009
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Well kusema tunarudi kule kabla ya Ukoloni...No!

  Fo example-- Kenya has GDP equlivalent to that of Belgium! Bado tuna matatizo ila tunaenda mbele ..sema taratibu!

  Kule Rukwa Barabara kati ya Tunduma hadi Mpanda itakuwa na lami in 2-3 years!

  We are in a transition for change! The transtion is taking so long!

  Rushwa bado zipo--ila rushwa not unique to Africa alone!
   
 3. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280


  Mkuu,

  Tusioogope ukweli!

  Katika bandiko la Richard unaona kabisa kwamba waafrika tunajitahidi kuwa apologetic. Ukweli ni kwamba as a continent we are doomed. Why do I say that?

  Utakuta mtu anakwambia kwamba..sisi tulipata uhuru wetu juzi juzi tuu..kwa hiyo tutaendelea. Lakini anasahau kwamba..sisi tumekuwa na sehemu nyingi za kuangalizia...wakati wenzetu wazungu hawakuwa na nafasi kama yetu. Mfano..wao waliiba na kutunyonya..lakini sisi baada ya kujifunza madhara hayo..ndo tumeyakumbatia.

  Mzalendo naamini wewe unaijua TZ? Mkuu I can assure you umasikini wa Africa huwezi kuu-appreciate kwenye CNN na majarida ya wachambuzi..mpaka uushuhudie. We are damn poor! Kama unaelewa maana ya hilo neno..Mimi nikienda village..unaona kabisa hali ni ile ile haibadiliki.....hata kama nikusaidia nitasaidia wangapi..wananchi gari wanayoiona ni ile ya DC mara moja kwa mwaka..na watoto wanaanza kuikimbiza kwa nyuma..unanipata kaka? juzi nakatiza namanga pale boarder..yaani nilisikitika sana..umeme hakuna..na ni worse kuliko palivyokuwa five years ago...


  Inauma lakini kwa aina ya uongozi tulionao Afrika akina JK ambao hawajui walifanyalo, akina Bashir, Mugabe et al..I can bet my self..hatuendi popote. Nimebahatika kutembea some few African countries..kwa kweli sioni theory ya kumchallenge huyo mzee hapo juu! Tunaweza singizia kila kitu. But WE know the truth deep down in our hearts.
   
 4. T

  The Truth JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 21, 2007
  Messages: 618
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Where did you get this information?
   
Loading...