Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Waulize wakongwe wa JF watakuibulia nyuzi inayo zungumzia kutembelewa kwa na Mwl usiku hapo mahakama ya samaki.
Ballantine na JD, nlikuwemo humo ndani.
Sikuwai kumuona akipiga John Mtembezi.
Hizo ni whisky kali pia ndo vilikua vyombo vyake.
Simpre.
 
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu.

Aliongea kwa lugha nzuri kama mwanasheria na mtu muungwana. Akamuelezea Mwalimu Nyerere jinsi alivyokuwa akimfahamu tangu alipokuwa kijana kabisa. Tukumbuke kuwa mwaka 1961 Mzee Warioba alikuwa ni mmoja wa vijana waliokuwepo pale uwanja wa Uhuru siku ya tarehe 9 mwezi Desemba. Hivyo anamfahamu vyema hayati Mwalimu.

Akiwa anaendelea kujenga hoja ya unyenyekevu(humility) wa hayati Baba wa Taifa akaongelea suala moja lililoniacha nikiwa nimezama katika fikra nyingi aple aliposema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi hata mara moja kuhutubia kanisani.

Nikaona kamera ikizungushwa na akaonyeshwa Amani Karume mdogo wake na rais wa zamani wa Zanzibar, macho yake yakawa yanatazama juu hewani kama alikuwa na mawazo fulani yaliyomjia kichwani muda huo.

Kwamba Mwalimu Nyerere alipenda mno kujishusha na hakulewa na madaraka.Siku zote alikuwa tayari kujiweka katika nafasi ya mtu wa kawaida pasipo uwepo wa dalili wala viashiria vya makuu, ni kama Mzee Warioba aliamua kusisitiza kwa viongozi wa sasa waendelee kujishusha wawe ni watu wa kawaida wasiwe ni Miungu watu.

Nikakumbuka miaka ile ya 1980 pale kanisani Saint Joseph Hayati Baba wa Taifa alikuwa siku moja moja akipenda kusali. Kilichokuwa kikituonyesha kwamba yeye ni rais ni kwamba kile kiti chake kirefu kilikuwa kikikaliwa na watu watatu tu. Yeye mwenyewe katikati kushoto mlinzi mmoja na kulia mlinzi mwingine. Hakuwa na mbwembwe za kutaka kupewa kipaza sauti wakati misa ikiwa inaendelea ili eti aanze kutoa maagizo mle mle kanisani.

Hoja kama hii ya Warioba ni nzito na pengine katika utu uzima wake alionao kwa sasa ni wakati muafaka kufikisha ujumbe kama ule ule aliousema Askofu Niwemugizi kwa Samia kule Kagera. Kwamba cheo chako kipo leo na kesho kinakwenda kwa mtu mwingine, hivyo tumia busara siku zote katika maamuzi yako.

Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.

Pia ni kama ile picha maarufu ya Bilionea Bill Gates aliyoipiga akiwa kapanga foleni huko USA kavaa jeans yake kama vile ni mtu wa kawaida tu.

Anajishusha na kutojikweza siku zote, jaribu kumuweka Gates na pesa zake na ushawishi wake katika nafasi ya hawa matajiri wanaomiliki mabasi ya mikoani na vituo kadhaa vya kuuza petroli, namna wanavyotaka wanyenyekewe kama vile wao ndio wanaowapa binadamu wengine uhai na kuuondoa!.

Tutamkumbuka sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kawaida mwenye ucheshi mwingi na busara nyingi. Lakini ndani kabisa ya nafsi yake akiwa mtu wa kawaida kabisa.

Ukikutana nae pale ikulu katika zile koridoo karibu na yule Simba aliyekaushwa miaka ile anakuwekea mkono kichwani na kukuuliza hujambo mwanangu!?. Ni kama jana tu lakini inakaribia miaka 40 sasa.
Katika issue ninayomsifu Mwalimu Nyerere ni kuwa hakuwahi kujilimbikizia Mali. Ndio maana familia yake hasa watoto wake wanaishi maisha ya kawaida sana.
 
Atleast mbele za Mungu JPM hatajibu kwa Mungu wake kwa nini watu aliowaongoza waliacha kumtegemea Mungu wakategemea barakoa. Hilo swali halitamuhusu. Alisitiza wazi kumtegemea Mungu wa Mbinguni kwa kila jambo na kumuweka wa Kwanza kwa kila kitu.
Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa coroa hiyo hiyo iliyoua mapadre na maaskofu ndio iliyomuua na yeye.

Waliomtegemea Mungu kumzidi yeye waliiogopa Corona iliyokuwa ikiwaua mchana na usiku sembuse mtu aliyeletewa injili kwa mitumbwi ya wazungu!.
 
Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa coroa hiyo hiyo iliyoua mapadre na maaskofu ndio iliyomuua na yeye.

Waliomtegemea Mungu kumzidi yeye waliiogopa Corona iliyokuwa ikiwaua mchana na usiku sembuse mtu aliyeletewa injili kwa mitumbwi ya wazungu!.

Hawatakuwa na uhalali wa kuhimiza na kusema tumtegemee Mungu.
 
Back
Top Bottom