Mzee Warioba: Miaka 60 ya Uhuru tunaanza kurudi kule kule kwenye matabaka ya Waheshimiwa na Makabwela!

na ndo maana bidhaa zikipanda Bei hazishuki.....!!!
Inflation kwa sasa ni tatizo la Dunia nzima,kule US kwenyewe sasa hivi inflation iko 6.3% na FED wameishiwa mbinu kuipunguza kwa sasa wanahaha kuongeza debt ceiling ili waendelee kukopa mpaka pale Yesu atakapokuja kama atakuja kweli
 
Inflation kwa sasa ni tatizo la Dunia nzima,kule US kwenyewe sasa hivi inflation iko 6.3% na FED wameishiwa mbinu kuipunguza kwa sasa wanahaha kuongeza debt ceiling ili waendelee kukopa mpaka pale Yesu atakapokuja kama atakuja kweli

Oohndio maana tozo imerudishwa kimya kimya kweli inflation Dunia nzima hamkosi la kujitetea
 
Hivi mzee Warioba alijificha wapi wakati nchi ilipokuwa mikononi mwa Masihi.
Mbona hakunyanyua kinywa chake tulipokuwa tunatekwa ovyo!!?
Mzee acha unafiki
 
Tulikuwa na maadui wa tatu adui wa nne aliongezwa baadaye. Maadui hao ni : ujinga, umaskini, maradhi pamoja na dhuluma aliyeongezwa baadaye" anasema Mzee Warioba.
=====

Adui dhuluma alipigigiwa kelele na vita sana awamu ya kwanza na ya tano. Ya tano kwa maana ya kudhibiti kangomba ya korosho, dhuluma ya manunuzinya vifaa vya nishati jadidifu na mengineyo! Hata awamu nyingine adui dhuluma alipigiwa kelele mifano mnayo.

Lakini, nimegundua adui huyu dhuluma ni hatari sana. Inatakiwa mkakati madhubuti kumkabili. Kwa miaka 60 ya uhuru....wale waliojaribu kumdhibiti adui huyu wa"mejeruhiwa" sana. Kama taifa kila mtu kwa nafasi yake afikirie namna bora ya kumuondoa adui dhuluma! Kumbuka adui huyu ana"jeruhi" vibaya sana kila anayejaribu kumdhibiti, kwa hiyo mkakati wa kumdhibiti usiwe wa "kitoto"!!!
 
Mi mama ananifurahisha anavyowapuuza tu hawa watu.......yupo kimyaaaaa km hasikii chochote vilee. Wanabaki maadui wanajibishana wenyewe tu. Nimependa sana hii
 
"Ubabe na unyonge kwa sasa ni wazi ndilo jambo linaloendelea nchini."

Hayo ni maneno ya mzee Warioba akiuponda Utawala unaoendeleza sera za kuwanyonya wanyonge na kuwakumbatia wenye mamlaka na Mali jambo ambalo mzee amesema tulikuwa tumeshaanza kuyasahau.

Msikilize wenyewe ITV kuanzia saa 3 usiku huu
hawa wazee wengine watulie tu, kama wanalo la kuongea waende kimya kimya kumshauri mama kuliko kumlipua huku nje, hawajengi kitu wakifanya hivyo, na zaidi ya yote wataanzisha uadui mpya wapoteze muda kwenye kushughulikiana badala ya kujenga nchi. kwa heshima yake kwanini asimshauri tu internally kuliko kuja kumsemelea kwa watu huku nje?
 
Hivi wakati wa Magu mbona wengi waliufyata mkia?
Wakati maiti zikiwa kwenye viroba kina Warioba walikaa kimyaaaa

Sasa waliokuwa wanaongea wakati huo wako kimya na waliokuwa na woga wa kuongea ndio wanaongea sasa

Maisha ya nchi masikini yote yako sawa kila siku yanabadilika kutokana na mood ya kiongozi aliepo popote pale

Umasikini mbaya sana unatufanya tuwe hivyo bila kupenda
 
Hayahaya vijana wa uvccm changamkieni fursa! Makonda alitoka hivyohivyo

Chapa vibao
 
Ujumbe mzito wa mtume Bob Marley uwafikie watanzania wa tabaka zote ---Emancipate yourself from mental slavery .
 
Back
Top Bottom