Mzee wangu ananichanganya

Afrika Furaha

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
329
9
Mzee wangu simuelewi kabisaaaaa. Mwaka wa 4 huu amekuwa akinisisitiza nitafute mwanamke mwenye sifa zifuatazo :-
- Awe na elimu isiyopungua form six, na kama ana six awe na mpango wa kusoma zaid ya hapo
- Asiwe mzungu, mhindi wala mchina
- Awe anaingiza kipato kama kazi au biashara
- Asiwe "mtoto wa mjini"
Na mbaya zaidi atataka amu-interview kama ana uwezo wa kujieleza, kabla hajaamua kumkubali. Ninacho shangaa, hajawahi kunieleza kama mapenzi ni muhimu au sio muhimu. Na kali zaidi mke wake mwenyewe (maza) kaishia la 7. Naona kama kuna mbinu za kunitafutia mke hivi . . . .
 
Muulize...kama ikitokea tofauti na matakwa yake na wewe umependa itakuaje!?!Kweli mzee wako ana lake jambo...awe na uwezo wakujieleza kwani anatafuta kazi jamani?
 
hilo la asiwe mtoto wa mjini namuunga mkono!watoto wa mjini hawana uvumilivu atatafuka kidumu pembeni au atakuambia anarudi kwao hana shida!
 
Mpotezee huyo ! Atakuchanganya zaidi ukiendelea kuchukua ushauri wake. Yeye muuhusishe tu katika hili mchezo mzima unatakiwa uucheze wewe kwani wewe ndiye utakaye kuwa na huyo binti.

Ooh ajue kujieleza anataka kukuchakachulia halafu binti awe na uwezo wakudanganya kwa kukupa maelezo tele

mmh hiyo kali
 
Hakuna ubaya kupewa ushauri na baba yako. Labda yeye amejifunza kitu kwa kuwa mama yako alimaliza la saba.

Mbona vigezo vyepesi tu? Labda cha mtoto wa mjini ndo kigumu
 
Sasa Gaijin huo ni ushauri au masharti hayo?
wengi tunathamini ushauri wa wazazi linapokua suala la ndoa.
Lakini wazazi wengine sasa wanasahau kushauri bali wanatoa masharti.
 
Kwani ameambiwa asipofata ataadhibiwa?

Hakuna sharti hapo ni ushauri tu, kama hataki kufata ushauri wa baba yake basi.

Sio kumleta hapa kudhihakiwa.
 
G mpaka na interview ? Asipopita huo usaili wa baba si basi amefeli kigezo kimojawapo?
sasa huo ni ushauri gani basi...
 
Kwanza kuna kitu waswahili wamesema "msema pweke hakosi"

Hivi unaamini kuwa baba yake kamwambia ende akamu interview? Naamini hakuambiwa hivyo.

Usikute kaambiwa "mlete tumuone mapema, tuzungumze nae, tuone kama tunaelewana kwa kuwa ndoa si ya wawili tu kwa mila ya kwetu"
 
Mmh Gaijin, msema pweke hakosi maana yake nini?

Inawezekana kweli baba hakusema ampeke akamsaili jamaa kaongeza ndimu ya unga na pilipili. Vinginevyo ningemuona mdingi mkoloni kwa kweli.
 
Msema pweke hakosi ina maana anaehadithia kitu peke yake huwa hawezi kujuulikana kama kakosea kwa kuwa hakuna hadithi kutoka upande wapili.
Yeye kamchora baba yake hivyo na sisi tunaamini kwa kuwa ni msema pweke ndo hakosei :(

Soma maoni ya watu uone alivyomtukanisha kwa kuwa tu yeye mwenyewe hakuonyesha kumuheshimu.
 
Msema pweke hakosi ina maana anaehadithia kitu peke yake huwa hawezi kujuulikana kama kakosea kwa kuwa hakuna hadithi kutoka upande wapili.
Yeye kamchora baba yake hivyo na sisi tunaamini kwa kuwa ni msema pweke ndo hakosei :(

Soma maoni ya watu uoni alivyomtukanisha kwa kuwa tu yeye mwenyewe hakuonyesha kumuheshimu.

Asante G, sisi wengine uingereza hatupo na uswahili hatupatikani!

Unayosema yana maana sana na haya ndo madhara ya simulizi ya upande mmoja na pia habari za mkono wa pili!
Ukute hapo the original conversation ilikuwa tofauti kabisa. Basi hapa ni kubahatisha na kuweka 'Kama' na '-Nge' (tunaotea)
 
Na zaidi ubaya uko kwenye namna ya kuwasilisha hoja. Ukileta kizembe zembe na watu watachangia hivyo hivyo kizembe zembe.

Acha twende na hizo 'kama' na 'nge' tu ndo lilobakia :s
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom