Mzee wa Upako: Kufa masikini ni ufala!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,480
17,677
1390464_651468914928406_1519651006_n.png

Mzee wa Upako

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo alimaarufu kama 'Mzee wa Upako' amefunguka na kusema mtu kufa maskini si jambo la kusifiwa hata kidogo kuwa ni uzalendo bali ni Ufala.

Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha UJENZI cha EATV kinachoruka kila Jumapili.

Mzee wa Upako anasema mtu anapokufa akiwa ameacha mali za kutosha ni jambo jema kwani familia yake nyuma haiwezi kupata taabu wala watoto hawawezi kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa na kitanda tu kwani watoto wake watapata shida na mateso.

"Watu wanamsifu mtu amekufa bila mali eti alikuwa mwadilifu yaani unakuta mtu amefanya kazi serikalini miaka na miaka, sijui miaka 35 au 40 anakufa hata kitanda hana.

"Wapo watu wanasema huyu jamaa alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa fala umenielewa?, huyu alikuwa fala na hastaili kuwa kielelezo cha msingi tuhoji mtu kapata mali wapi?

"Ndio jambo la msingi sababu unaacha watoto duniani unadhani wataishi vipi? Mama anakuwa na nyumba pale anachota kodi anapeleka watoto shule maisha yanaendelea" alisisitiza Mzee wa Upako.
 
Mzee wa upako ni one of a kind pastor
 
uyo bapa alichobakisha kutukana madhabahuni ni matusi machache sana. kuna siku atatukana watu ''WASSENGE" au atataja lile tusi la kutukania mama. kwasababu ukienda kanisani kwake nafikiri matusi kama mshenzi, pumbavu, mjinga, fala etc ni vitu vya kawaida. sasa sijui mungu gani anamwabudu hata huwa sielewi. hata nyumbu wanaomiminika pale kibangu pamoja na kuonekana kabwia konyagi, na anatukana mtu kuwa akikutana naye atamuua, bado wapo tu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom