Mzee wa Upako, CHADEMA hawana muda wa kukuchafua, Mungu ameamua kuanika tabia yako

Mpira wa kona

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
350
338
Nimeshangazwa kauli ya Mchungaji Lusekelo "Mzee wa Upako" akilalamika eti Chadema wanamchafua eti wanamwonea wivu wa kujengewa Barabara Na Mh.Rais.

Haingii akilini mhubiri huyo kudai eti Mh.Lowassa hawezi kushinda uchaguzi 2020 Kwa sababu Chadema wamemchafua.

Napenda kumhakikishia Mchungaji Lusekelo Mungu ameamua kumwanika Mchungaji huyo kutokana Na matendo yake maovu ili waumini Na wasio waumini wamjue tabia yake Na kweli amejulikana Leo unawasingia Chadema wanakuchafua uliwakosea nini?

Mchungaji Lusekelo acha kusingizia watu ili kuficha dhambi zako unachotakiwa ni kuomba msamaha Kwa waumini wako Na watanzania Kwa ujumla.

Kumbuka Barabara unayojengewa ni kodi za masikini Na wanyonge wa Tanzania.Umewaambia waandishi wa habari eti wale waliokuandika watakufa, haikuwa kauli sahihi Kwa kiongozi wa dini kama wewe waandishi walikuwa wanafikisha ujumbe wa waumini wako.

Mchungaji acha vitisho.
 
Yaani hata Mimi siamini yangu lini chadema imuandame mzee wa upako? Kwa kosa gani? Kwani yeye amekua mwanasiasa?
Mzee wa upako matatizo yanapotokea usitafute w kumsingizia Bali pambana nayo usimsingizie MTU. Kwa kweli umenitoa imani sana kama muumini wako. Jua kitu kimoja Mungu ni wetu zote, habagui wala hana hiana na huumpa ampendae.
 
Kiukweli za mwizi huwa ni arobaini. Kazi ya shetani ni kumuingiza mtu dhamini na kisha kumuumbua. Mzee wa upako, dawa ya dhambi ni toba. Chadema haihusiki kwa namna yoyote. Umepata kipato kutokana na biashara unayoifanya na ukatumia kipato hicho kujidhalilisha.
 
Kazi hipo,
1: Gwjima- Mbasha
2: Efatha- Mke wa Docta Mkameroun
3: Malasusa- Mke wa mtu
4: Mokiwa- nidham mbovu
5: Mzee wa Upako- Cha Pombe

Hivi Kanisa lake halina wana Chadema au Wapenzi wa Lowassa?, kwa nini anajitengenezea maadui bila sababu
 
Mabapa ya negative effect kwa mtapta huyo mpiga dili! Barabara ni ya umma sio yake na itabaki hivyo siku zote; limekuwa poyoyo!
 
Back
Top Bottom