Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,895
- 31,106
MCHUNGAJI wa Kanisa la Gospel Revival Centre, Antony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, ameishukia serikali na Idara ya Usalama wa Taifa kwa kukumbatia zaidi madhehebu ya Katoliki na Lutherani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mzee wa Upako aliwaonya viongozi wakuu wa serikali kutoichezea amani iliyopo kwa kubagua madhehebu mengine yanayoitwa ya vichochoroni.
Alionya kwamba ni rahisi kuipoteza amani iliyopo sasa kuliko kuitafuta, hivyo aliwataka viongozi wa serikali kuacha kuyadharau baadhi ya makanisa kutokana na ukweli kwamba wanaohubiri injili ni walinzi bora wa rasilimali watu katika kutunza amani ya nchi.
Makanisa ni kama makabila, hivyo kitendo cha serikali kuwapendelea zaidi baadhi ya viongozi wa dini ni kutishia ustawi wa amani iliyopo.
Serikali inalea sana makanisa haya, maaskofu wengine wanapewa passport za diplomat, wakipita popote hawakaguliwi, wakati wengine tukipita uwanja wa ndege pale tunakaguliwa hadi soksi hii inaonyesha kwamba hawatuamini, alisema na kuongeza kwamba sheria ya usajili wa makanisa ni moja hivyo anashangazwa na ubaguzi wa aina hii.
Aidha, aliwatahadharisha viongozi wa serikali kukumbuka yaliyotokea Rwanda ambako kwa asilimia kubwa kanisa lilichochea mauaji ya kimbari hali iliyosababisha washitakiwa wakuu katika kesi ile kuwa viongozi wa dini.
Huku akionyesha kujiamini sana, alisema vyombo vya usalama wa taifa vimelala na kwamba havitambui wajibu wao kutokana na ushauri mbaya hasa kwa upande wa madhehebu aliyosema huitwa ya kikanjanja kutothaminiwa.
Mchungaji huyo ambaye makao makuu ya kanisa lake ni Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam alisema pasi na shaka kwamba dharau ya viongozi wa serikali dhidi ya makanisa hayo imekithiri kiasi cha kutodiriki kujibu hata barua za mwaliko wanazopewa na wachungaji.
Akitolea mfano aina ya ubaguzi huo, aligusia sakata la upitishwaji wa umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 132 kwenye Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililo chini ya Askofu Zachary Kakobe.
Hili suala linalomsumbua Askofu Kakobe pale, kama umeme huo ungepitishwa St. Joseph akatoka Pengo kulalamika mngesikia Waziri Mkuu amekwenda na angemwomba kwa kumtuliza na mambo yangeisha, lakini sio Kakobe hadi leo anahangaika, alisisitiza Mzee wa Upako.
Katika hilo aliishauri serikali kumsikiliza Kakobe na kutafuta njia nyingine ya kumsaidia, na kwamba yupo naye bega kwa bega ili kuhakikisha suala hilo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
Aidha, alibainisha kwamba wanasiasa wote waliofilisika kisiasa wanakimbilia makanisani hivyo kutahadharisha upatikanaji wa rais ama viongozi wa kiserikali wasiostahili kutokana na shinikizo la viongozi wa dini wanaoonekana kuaminiwa zaidi na serikali huku usalama wa taifa ukiwa kimya.
Ni hao wanaopewa passport za diplomat ndio wanaoonekana viongozi wa dini, wametusahahu kabisa sisi. Huku tunakoelekea tutawekewa rais hata kichaa kwa sababu tu amepitia kwao.
Haya makanisa mnayoyaona yana watu wengi mkitoka nje ya mipaka yetu hayana waumini. Yanaheshimika hapa tu, hawajui kuhubiri hadi wawashe mishumaa. Wataishia kubusu pete za viongozi wao huko nje, alisema alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
Hata hivyo, aliweka wazi mapenzi yake kwa Rais Jakaya Kikwete na kusema anatamani aendelee kuongoza Tanzania. Binafsi mimi kama Lusekelo, namfagilia Rais Kikwete, natamani aendelee kuongoza, alisema.
Source: Tanzania Daima.
My take.
Mtandao wa makanisa ya Lutherani na Katoliki ni mkubwa sana na umeenea karibu kila sehemu Tanzania.Madhehebu ya akina Mzee wa upako yako mengi sana lakini yako disorganise kiasi kwamba serekali inapata taabu sana jinsi ya kuwasiliana nayo.Utakuta mtumishi wa Mungu anaongoza kanisa lisilokuwa hata jengo [anatumia majengo ya shule] anajiita Askofu na anataka heshima anazopewa Askofu wa kanisa katoliki/Lutherani.Mwingine unakuta kaanzisha kanisa nyumbani kwake kaamua kujita nabii xyz,kanisa lake lina waumini 100 atataka naye kujifaninisha na kina Pengo au Malasusa kwa kweli serekali ipo sahihi kabisa.Makanisa mengine ukiyatazama kwa makini utagundua ni mali ya viongozi,makanisa ya jinsi mara nyingi yanasambaratika wakati viongozi wao wanapofariki au wanapojitokeza baadhi ya waumini wajuaji watakaohoji mambo ambayo viongozi/waanzilishi hawataki kuyaweka wazi.
Makanisa yanayoongozwa na kina mzee wa upako na Askofu Z Kakobe yatatetereka sana siku viongozi wake watakapotangulia mbele ya haki kwasababu misingi yake imejikita zaidi katika vipaji vya uongozi ukilinganisha na makanisa ya Lutherani na Katoliki.
Mzee wa upako ameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba wahubiri wa makanisa ya Lutherani/Katoliki hawajui kuubiri wamebaki kubusu pete tu.Mimi ni muumini wa madhehebu ya Lutherani kila j2 na kwenda kanisani kusali kama ningekutana na mahubiri mabovu/hovyo kwa vyovyote ningekubali kupoteza muda wangu nadhani mzee wa upako kaamua kubwabwaja tu labda ana jambo lingine kaamua kulificha.