Mzee wa Mchemsho Ezekiel Maige umechanganyikiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee wa Mchemsho Ezekiel Maige umechanganyikiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, May 30, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  KELELE anazopiga Mbunge wa Msalala, Ezekiel Magolyo Maige, zinanichefua. Analalamika kila uchao na kibaya zaidi anatumia vyombo vya habari.

  Malalamiko yake yanasababishwa na kupokwa dhamana ya uwaziri wa Maliasili na Utalii aliyopewa kwa muda tu na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete.
  Anasema kilichomtoa kwenye nafasi hiyo ni majungu na fitina za kipumbavu zilizotengenezwa dhidi yake na makada wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Rais Kikwete, ambaye ni mwenyekiti wa taifa wa chama hicho tawala.

  Dakika za mwisho na punde baada ya uamuzi wa mwajiri wake kumfuta kazi ya uwaziri alinukuliwa akitamka maneno ya kiungwana yenye kutaka imani ya Watanzania juu yake na kuonyesha wazi kwamba husuda na chuki za wenzake zimetokana na ununuzi wa hekalu lake la dola 700,000 za Marekani.Ezekiel Maige anatamani kuenguliwa kwake kwenye nafasi hiyo kuwe ajenda ya taifa ndiyo maana anatumia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, watu mmoja mmoja, vikundi na hata wazee kwa kuwapa ‘mshiko' ili wamwamini na wakubali kwamba Rais Kikwete amemwonea.

  Huyu mtu baada ya kutimuliwa kwenye uwaziri anarudi jimboni eti kuzungumza na aliowaita wazee na wapiga kura aliowapa cha kuwapa nao wanajifanya kumwonea huruma na kudiriki kusema watamuunga mkono kwa uamuzi wowote atakaochukua hata ikibidi kukihama chama kilichompa dhamana ya kukiwakilisha kwenye ubunge.

  Hebu wajiulize enzi za uwaziri wake alikwenda mara ngapi jimboni kuzungumza na waliomchagua kuwa mbunge? Ni kweli Ezekiel Maige alikuwa anaketi nao kwenye vilabu vya pombe kama ilivyokuwa enzi za kampeni mwaka 2005?
  Au kwa vile sasa hana gari lenye namba za W MU? Hatumii tena mafuta ya serikali, hataalikwa tena kwenye mikutano ya kimataifa kuiwakilisha nchi kama waziri? Akirudi bungeni atakaa kwenye viti vya nyuma na kuwa muuliza maswali si mtoa majibu? Nini kinamhangaisha Ezekiel Maige?

  Hizi filamu za wasanii wa serikali ya awamu ya nne tulianza kuziona mwaka 2008 wakati aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alipowajibika kwa hiyari baada ya watendaji wa chini yake kuboronga kwenye mkataba tata wa Kampuni ya kufua umeme kutoka Marekani ya Richmond.


  Lowassa na mawaziri wenzake wawili waliwajibika. Wenye busara tuliwapongeza licha ya wao kuamua kutafuta faraja kama anavyofanya Maige ambaye mtindo anaoutumia unampambanua kuwa si mvumilivu.


  Nawashauri wapiga kura wa Msalala wasikubali giriba wanazofanyiwa na mbunge wao wa sasa kwa sababu kufukuzwa kwake kwenye uwaziri kulitokana na uroho wa madaraka aliokuwa nao, kwa kuwa alishindwa kuwajibika kama watangulizi wake.


  Nilizungumza na rafiki yangu akaniambia zamani watoto wa kiume waliokuwa wakipelekwa kufanyiwa tohara kikubwa walichousiwa huko ni uvumilivu, ndiyo maana walikuwa wakitahiriwa bila ganzi.


  Hali hiyo ipo kwenye baadhi ya makabila hadi sasa.
  "Tohara ya kienyeji ina maumivu sana ndiyo maana watoto wa kiume wakiwa jando kila siku wanaambiwa kuwa wavumilivu kwenye kila jambo watakalokutana nalo maishani… mtoto wa kiume ukimwambia siri lazima awe na kifua cha kuitunza. Huyo tunamwita jasiri," alisema rafiki huyo.Kwa maelezo hayo nimejiridhisha kwamba Ezekiel Maige si mvumilivu, hana ujasiri, tena ni mwoga aliyeamini kwamba uwaziri ni sehemu ya ngozi ya mwili wake, atakufa nao, ndiyo maana hakujiandaa kuondoka kwa wakati ule.

  Ninalazimika kuamini kwamba Ezekiel Maige alikuwa na biashara inayoitwa ‘uwaziri', sasa amepata hasara kwa sababu biashara imefilisika kabla hajapata faida aliyoitegemea ndiyo maana anawayawaya, hana pa kushika, analia moyoni, machoni na hadharani, hataki kuamini.

  Nawashauri wapiga kura wa Msalala mwaka 2015 wajiandae kumpata mbunge mwingine jasiri mwenye uvumilivu, atakayekuwa karibu yao muda wote, si wakati mgumu pekee kama anavyofanya Ezekiel Maige sasa.Naamini maumivu ya uwaziri yakipoa hatarudi tena jimboni hadi wakati wa kampeni, kwa hiyo kuweni makini naye, atakachowapa pokeeni, akili kichwani kwenye sanduku la kura, unachokifanya ni siri yako.

  Ezekiel Maige anahitaji ushauri nasaha.

   
 2. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ajutie madudu yake aliyoyafanya Maliasili mbona hayo hakuyasema kabla mpaka Mwenyekiti alipomuumbua hongera Mh Lembeli.
   
 3. I

  Iramba Junior Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu this is very true and serious!Hana lolote mbona haya yote hakuyasema muda wote?, haya ni maumivu ya kuukosa uwaziri! Kama ametolewa kwenye uwaziri ya nini kwenda kulalama jimboni? Je wana jimbo lake walimchagua kuwa waziri au mbunge! Mimi nadhani hata wapigakura wake wangefurahi kuona kwamba mbunge wao kapunguziwa majukumu na kupata fursa ya kuwa karibu naye ili kulijenga jimbo kimaendeleo na siyo kutamka kwamba aseme lolote na sisi tuko tayari kumfuata!
   
 4. KML

  KML JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  umaarufu wote alioupata bado tu hajaridhika, haaaaa maige
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  serikali ichukue lile hekalu kabla hajalipiga bei kwa sababu amechanganyikiwa na hana amani nalo.
   
 6. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,021
  Likes Received: 2,633
  Trophy Points: 280
  Hofu iko kwenye kupoteza hakalu la $700,000,lazima uchanganyikiwe,hell has broken loose nilijua tu siku yenu itafika hakuna dhambi nzuri,feel the pains of sufferer Tanzanians due to your selfishness.
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Huyu mpuuzi hajui kazi yake ilimtaka nini, mbona KAGASHEKI kaweza kuukata mbuyu uliomshinda maige,huyu ni kibaraka wa mafisadi walimpa hongo akashindwa kutekeleza majukumu, kubwa jinga na CPA-T yake umewaangusha wahasibu kwa kushindwa ku-apply QT katika kufanya infomed decisions.kwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 8. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Analalama kama mwanamke aliyepewa talaka na kujisafisha mitaani kwa kumtangaza huyo mtalaka wake kuwa si chochote si lolote hali anaumia roho kwa kuachwa. Miage hukubatizwa kuwa waziri ulichoiba kinatosha, kwanza unastahili kwenda mahakamani kwa ufisadi ni kwa vile hii Takukuru yetu ni Taasisi ya kuendeleza na kuboresha rushwa
   
 9. G

  Galaticos Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huyu ni gamba kweli....hata demu akiachika halalamiki kiasi hiki....kwani alizaliwa kuwa waziri?
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi jamaa mpya aliyeingia maliasili hakuamini aliyoyakuta. Maana hajui hata aanzie wapi. Watu wanagawana taratibu taratibu tu
   
 11. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  mimi simuonei huruma kabisa huyu MAIGE. lipi huyu anaweza kujivunia ameifanyia hiyo wizara achilia mbali jimbo lake. hata 2015 naomba aangukie pua!!!!! nitafurahi wewe.
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Namshauri Maige arudi kufundisha CPA review classes siasa imemshinda
   
 13. naninibaraka

  naninibaraka JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  alilewa madaraka akasahu kuna siku atayakosa na kuwa mtu wa kawaida,leo tungekuwa seriously huyu alipaswa apandishwe mahakamani
   
 14. M

  MTK JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Maige awambie watanzania hicho anachokiita majungu, husuda na Chuki dhidi yake ni kipi katika ripoti ya mheshimiwa Lembeli?! aache ngonjera awe muwazi ataje jungu, husuda etc 1,2,3 ili watu wachambue, kwa sababu tuhuma ziko wazi, kama tuhuma yaTwiga kuuzwa kinyemela ni majungu kwa nini alimtimua kazi aliyekuwa mkurugenzi wa wanyama pori? Je usafirishaji wa magogo nchi za nje kinyume cha sheria ni majungu, kugawa vitalu vya uwindaji kinyume cha taratibu zilizowekwa ni majungu? ubadhirifu wa fedha TANAPA na Ngorongoro conservation ni majungu na husuda? Maige wacha kuwahadaa wanyantuzu wako, wambie ukweli hata mungu atakusaidia acha kuendeleza uongo wa kuisafisha dhambi.
   
 15. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kama alidhani UWAZIRI NIG*VI SASA KATAHIRIWA. ATULIE APONE NA AWE MWANAUMME WA KIUKWELI!!! WAJINGA SANA WATU WA NAMNA YAKE WANADHSNI HIZI NAFASI ZA KUWATUMIKIA WANANCHI NI UFALME...HADI AFE NDIO ANACHUKUA MWINGINE
   
 16. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,559
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu atawafundisha wahasibu wetu namna bora na nzuri ya kuiba.Huyo hata kufundisha hatakiwi kabisa.Kwanza inabidi kuishauri Bodi ya Wahasibu kuwa wahasibu wote wanaokutwa na Ufisadi na wezi wa mali ya umma wanyanganywe certificates zao za CPA maana hawafai kuitwa wahasibu wanatuaibisha.Namuomba Maige atuombe radhi wahasibu ametutia aibu kubwa.
   
 17. mjomba wa kale

  mjomba wa kale JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Anadhalilisha vijana kiasi kwamba wataonekana hawana uvumilivu hivyo kwakuwa amechanganyikiwa serikali imzindue kwa kumpandisha kizimbani
   
 18. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Unamnyanganya Simba nyama mdomoni?Unategemea nini?Huyo jamaa alikuwa akilamba mpaka dola laki tano kutoa kibali cha kitalu kimoja tu cha kuwindia!!Amechanganyikiwa alitegemea amalize na uwaziri huo awe billionea na hata kugombea Urais!Lakini mipango yake yote imeharibika?OOOOhh nimeonewa!nimefitiniwa"?yeye anafikirii vyombo vya dola vimelala?
  Analamba madola ya vitalu akajisahau !!!Kila la kheri Maige!Get well soon!kwa maumivu ya kuukosa uwaziri!
   
 19. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Da nyuzi imetulia ila heading ya mchemsho kumbe ni kuchemka mi nikafikiri ile michemsho ya mbuzi maige aliyovimbishia shavu. Analalamika wkt b*kir* keshatolewa. Umeharibu kaa kimya msifie JK anaweza kukupa ukuu wa mkoa sasa umelikoroga ubunge utapigwa chini labda ugombee ujumbe wa nyumba kumi.
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kupewa dhamana ya kukodisha vitalu vya uwindaji sio mchezo mazee, kuna dili za mabilioni pale. Hizo $ 700,000 za hekalu ndogo saana.
   
Loading...