Mzee wa Chato: Mimi ni mwanachadema mtiifu kwa chama changu lakini Rais Magufuli anapofanya mazuri lazima tumuunge mkono

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,240
Nimeupenda sana huu msimamo wa yule mzee wa Chato ambaye ni Chadema damu aliyesema Rais Magufuli kwa mazuri anayolitendea taifa hili ni lazima tumuunge mkono bila kujali itikadi za vyama vyetu

Ni matumaini yangu kuwa wanachadema wenye mapenzi mema duniani kote ikiwemo kamati kuu ya Chadema watauchukua ushauri wa kigogo huyu wa Chadema kutoka Chato - Geita.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna mtu anaweza kuhojiwa na vyombo vya habari sasa hivi enzi hizi za kundi la watu wasiojulikana kisha akasema tofauti na hicho huyo mzee alichoongea? Tundu Lissu tu ndio anaweza kuongea kutomkubali Magufuli hadharani na wapinzani wachache. Wengine wote ni kumsifu mungu wa Tanzania.
 
Umemuelewa lakini kigogo huyo wa Chadema kutoka Chato?!
 
MTU AKIFANYA VIZURI APONGEZWE AKIFANYA VIBAYA AKUBALI KUKOSELEWA(SIO KUKASHFIWA ETI DIKTETA UCHWARA)
 
Back
Top Bottom