Mzee wa Chato: Mimi ni mwanachadema mtiifu kwa chama changu lakini Rais Magufuli anapofanya mazuri lazima tumuunge mkono

B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2011
Messages
1,228
Points
2,000
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2011
1,228 2,000
Nimeupenda sana huu msimamo wa yule mzee wa Chato ambaye ni Chadema damu aliyesema Rais Magufuli kwa mazuri anayolitendea taifa hili ni lazima tumuunge mkono bila kujali itikadi za vyama vyetu

Ni matumaini yangu kuwa wanachadema wenye mapenzi mema duniani kote ikiwemo kamati kuu ya Chadema watauchukua ushauri wa kigogo huyu wa Chadema kutoka Chato - Geita.

Maendeleo hayana vyama!
Huyo mzee ni wa Karagwe. Alitoa ya moyoni bila kupepesa macho. Sasa sijui watamkataa wenzake kuwa ni msaliti!
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
4,245
Points
2,000
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
4,245 2,000
Magufuli anapatia sana kwenye mambo Mengi ila kuna watendaji wake wanaingiza siasa za Chuki na ukabila .
Mtu kwa kosa kama ni mchaga utasikia akitajwa Mara mbili mbili kwa kabila lake.
Utasikia ni mchaga kwa kurudia rudia.
Ni siasa za kishamba.

Upande wa Domokrasia, uchumi na Elimu serikali ya awamu ya tano inafeli sana.
Na hayo ndiyo msingi mkuu wa maendeleo kwa karne hii.
Ukirudi karne ya 17 utaachwa mbali sana mana dunia inakimbia kwa kasi ya ajabu.
Domokrasia haikwepeki duniani.
Wanaoikwepa wanatumia nguvu kubwa sana lakini baada ya miaka 20 ijayo dunia nzima itakua na mifumo ya kidemokrsia. Ili kuwatenga wema na waovu.
Waovu wasipate nafasi tena ya kuongoza kwa mitutu ya bunduki.
Tunaona Jimbo la Taiwani linavyogubikwa na maandamani ya kupinga Utawala wa China wenye hisia za kidikteta.

Elimu napo Mama hana jipya anajichanganya changanya tu na matamko yasiyoisha wakati wapo watu ambao wangeweza kuibua suluhisho la Elimu.
Maendeleo yangekua hayana vyama kwa vitendo Mbatia alikua anafiti nafasi ya uwaziri wa Elimu.
Hata Jimbo analoongoza na mkoa anaotokea ameweza kuhamasha ukuaji wa Elimu lakini sio Mama Ndalachakaa.
Uchumi nao ni shida awamu hii.
Bado sana maeneo yenye kuweza kuzalisha ajira hayajaguswa tumebaki na nadharia tu ya viwanda wakati kuna maeneo mengi sana yamebaki kama makumbusho tu.
Bado serikali inanunua magari ya kifahari sana na kijenga maofisi tu ambayo hayazalishi chochote zaidi ya kutumia kodi za wananchi.
Kiwanda cha Nyumbu cha magari kilipaswa kizalishe sasa na magari yote ya majeshi yetu yalipaswa yatengenezewe Nyumbu.

Wana kiwanda lakini wananunua mabasi ya kutoka India.
Ni ajabu kabisa.

Ni wakati sasa wa JPM kurekebisha hayo maeneo matatu ili tuondoe kabisa ukomo wa Urais awe rais wa maisha mana atakua amekidhi vigezo vyote.
Watanzania tumsaidie Mh. Rais kwa kuwaondoa wabunge na madiwani wa CCM wasiokua ana tija kabisa kwa taifa zaidi ya kugonga meza.
Bora hata bunge lifutiliwe mbali kuliko kuwa na wabunge zaidi ya 55% wa CCM.
Wanakula kodi zetu bure na hawana msaada wowote zaidi ya kukomoana na kudhibiti wabunge wenzao wa upinzani na kuzuia hoja ambazo ndizo Rais angependa azisikie.
Matokeo yake Rais anapata wakati mgumu na gharama kubwa kwa kufanya mikutano kujadili yale yale waliyozuiwa wapinzani kuyajadili bungeni.
 
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
11,536
Points
2,000
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
11,536 2,000
Nilimuona Mhe Rais kwenye runinga akiwataja baadhi ya wateule wake na kusema wakati mwingine hulazimika kuwapigia simu usiku na hata kuwaita wapumbavu. Nilistuka. Lakini baada ya kuona mijadala hivi karibuni iliyoanzia BBC, nimeamini Rais MagufuliJP alikuwa sahihi." - Khamis Kagasheki
 
hp4510

hp4510

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Messages
1,450
Points
2,000
hp4510

hp4510

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2012
1,450 2,000
Nimeupenda sana huu msimamo wa yule mzee wa Chato ambaye ni Chadema damu aliyesema Rais Magufuli kwa mazuri anayolitendea taifa hili ni lazima tumuunge mkono bila kujali itikadi za vyama vyetu

Ni matumaini yangu kuwa wanachadema wenye mapenzi mema duniani kote ikiwemo kamati kuu ya Chadema watauchukua ushauri wa kigogo huyu wa Chadema kutoka Chato - Geita.

Maendeleo hayana vyama!
Then wahame wote kutoka chadema waende ccm au sio
 

Forum statistics

Threads 1,316,115
Members 505,494
Posts 31,879,532
Top