Mzee wa Bwax ni msanii namba moja wa Singeli nchini. Msanii gani wa Bongo fleva wa kupambana naye jukwaani?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,068
Salaam wana jamvi.

Toka muziki wa singeli umeanza kuwaingia vichwani na masikioni Watanzania, kumekuwa na ujio tofauti tofauti wa wasanii wa singeli lakini ni ukweli ulio wazi Msaga Sumu alikaa kileleni muda mrefu sana na ndiye masanii aliyeweka chachu sana kwenye muziki wa singeli na kuutangaza.

Lakini miaka ya hivi karibuni muziki wa singeli kama ilivyo Bongo Fleva umekuwa ukizalisha vipaji vingi kama wakina Man Fongo, Dullah Makabila, Mzee wa Bwax na wengine wengi.

Na muziki huu umekuwa ukileta changa moto kubwa sana kwa wasanii wa Bongo Fleva, hasa stejini na kucheza na mashabiki.
MZEE-WA-BWAX-1.jpg
Mzee wa Bwax ameongeza chachu sana hasa jinsi ya kucheza na mashabiki stejini tofauti na wasanii wengine wa singeli na ukweli ni kwamba wasanii wa singeli hawahitaji kuwalazimisha mashabiki kushangilia au kupiga kelele bali mashabiki hulipuka na kujikuta kama vichaa vile.

Mzee wa Bwax ni mmoja ya wasanii nchini wenye nguvu kubwa na uwezo sana wawapo stejini na ninadiriki kusema ni msanii namba moja wa singeli kwa sasa.

Wasanii wa Bongo Fleva wanapata wakati mgumu sana wanapokutana na wasanii wa singeli stejini; ni wazi wanalo la kujifunza, hasa jinsi ya kucheza na mashabiki.

Bado najiuliza ni msanii gani wa Bongo Fleva anaweza pambana na mzee wa Bwax stejini.

Je, muziki wa Bongo Fleva umepata upinzani kamili stejini?

Wasalaam
 
Eti nani???
Mzee wa Bwax

Eti nani????
Mzee wa Bwax


Mzee wa Bwax wa Bwax wa Bwax wa Bwax

Booooooooom.

Namkubali maishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Wahuniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiìiiiiiiii



Naunga mkono; mzee wa bwax hana mpinzani kwa sasa,Na kidemu chake kilokole kikilewa kinahubiri
mimi nikienda kwa show ntakua kama wengine namngoja mzee wa bwax... "Ukichkua simu ya bwax na mziki utazimwa,,masela viroba tupa kule skuizi mwendo wa safari" Vibe lake sio la kawaida.
Unajua wanapokwama bongofleva wengi hawana nyimbo za amsha amsha, na concert nyingi zinabebwa nyimbo zenye Vibe.
Halafu singeli inaishi mziki wa zamani, kwamba msanii habebwi na jina, toa mziki mzuri ukubebe, ndio mana kila mwaka unaona anaibuka mtu mwingine na huo ndio mziki halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajiuliza Hilo swali ukiwa dar es salaam vp unafikiri huyo mzee wa bwax akienda Arusha au mikoa mingine ataendelea kufunika km ilivyo dar ..hebu jaribu kufungua ubongo wako na sio kuandika kimhemko tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi show ilikua Tanga, huyu dogo kapanda baada ya Harmoniser kushuka.

Harmo alikua akiwalazimisha mashabiki kuvua mpaka mashati, alipopanda huyu dogo watu walivua mpaka chupi

Namaliza kwa kukuuliza mkuu kwani Tanga ni Dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom