Mzee Victor Kimesera: Mzee Ndesamburo aliiwezesha CHADEMA kununua ofisi ya makao makuu

Mzee Victor Kimesera,mwasisi wa CHADEMA ametegua kitendawili ambacho kimekuwa kikitumiwa sana na watoto wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Just see for yourself

Wanamiliki ofisi au banda pale waweza ita ofisi ya makao makuu Ya chama kikubwa kama chadema? Huyo mzee alitakiwa Kusema chadema wanamiliki banda mtaa wa ufipa
 
Ukimsikiliza Bw. Kimesera utadhani anazungumzia harakati za uhuru enzi za TANU miaka ya 1950, lakini kumbe anazungumzia mambo ya karne ya 21 kwenye Tanzania ya utawala wa CCM.

Hii inatupa moyo kuwa na hawa Watawala Weusi pia nao wana mwisho.
 
Mzee Kimesera amemuelezea vyema sana Mzee mwenzake.
Chadema waenzini wazee wote hao na wala msiwabague kikabila
Kadanganya huyu mzee chadema kilipoanza nakumbuka mkutano wao pale mnazi mmoja wa uzinduzi kilianza kwa kishindo walikuwa Na malandcrusser magari Ya chama kibao CCM tulikuwa hatuna kilianza kitajiri mno waliKuwa na Wafadhili wa kaskazini kibao mmojawao alikuwa akikusanya michango marekani kwa niaba Ya chadema alikuwa balozi wa Tanzania umoja wa mataifa kwa jina Nyaki. Mzee mwongo chadema haikuanza kimaskini ilikuwa chama cha mabwanyenye na matajiri.
 
Mzee Kimesera amemuelezea vyema sana Mzee mwenzake.
Chadema waenzini wazee wote hao na wala msiwabague kikabila
Kuna kitu haweki wazi huyu mzee kuwa pesa walizokuwa wakichanga hao wafanyabiashara waliojificha zilikuwa zinaenda kwa ndesamburo sio hizo tu bali na zile za kutoka nje ya nchi kwa Wafadhili walioficha nyuso zao na agenda zao. Zikifika kwa ndesa anazitakatisha na kuwapa chadema akisingizia zinatoka kwenye biashara zake. Wakati ule sheria za utakatishaji pesa zilikuwa bado mwanya huo ukatumika. Yeye alikuwa bomba la kupitishia hela anapokea huku halafu anatoa mkono huku akifanya kuwa yeye tajiri anatoa pesa zake kumbe zimo za akina mtei, lowasa, sumaye nk
 
Mimi nafikiri tumuache Marehemu apumzike kwa amani. Haya mafigisu mengine yaendelee kutuhusu sisi ambao bado tupo hai kwa uwezo wa Mungu tu, kwakuwa bado tunayo nafasi ya kutolea maelezo na ufafanuzi wa jambo lolote. Hebu tuwaheshimu marehemu wetu kwakuwa ndio utamaduni wetu.
 
Mwaka jana si mliletewa notes ya pango? Imelipiwa lini? By the way hata kama kumnunua hilo si banda kabisa? Nyumba ya national housing imejengwa 1964 tena uchochoroni kwa mateja?
 
Back
Top Bottom