Mzee Victor Kimesera: Mzee Ndesamburo aliiwezesha CHADEMA kununua ofisi ya makao makuu

Tatizo la makani na mtei hawakuwa typical politicians bali walikuwa wataalamu..technocrats ...,ndio maana walifanikiwa kuandika sera nzuri sana ,lakini wao wawili walikuwa na ugumu sana wa kujieleza jukwaani wakaeleweka ....,unajua kuna watu aina hiyo wenye akili sana lakini hawawezi kujieleza
Mfano Makani pale SHINYANGA alijitajidi sana pamoja na kuwa walikuwa hawamuelewi
Sera ya Chadema ilichotwa kutoka NCCR Mageuzi. Mzee mtei alifanya copy and paste tu.
 
Kuna kitu haweki wazi huyu mzee kuwa pesa walizokuwa wakichanga hao wafanyabiashara waliojificha zilikuwa zinaenda kwa ndesamburo sio hizo tu bali na zile za kutoka nje ya nchi kwa Wafadhili walioficha nyuso zao na agenda zao. Zikifika kwa ndesa anazitakatisha na kuwapa chadema akisingizia zinatoka kwenye biashara zake. Wakati ule sheria za utakatishaji pesa zilikuwa bado mwanya huo ukatumika. Yeye alikuwa bomba la kupitishia hela anapokea huku halafu anatoa mkono huku akifanya kuwa yeye tajiri anatoa pesa zake kumbe zimo za akina mtei, lowasa, sumaye nk
Pesa za Lowasa na Sumaye?Unapaswa ujidharau mwenyewe kabla ya kudharauliwa!
 
Hauko mbali na ukweli. CHADEMA kilianzishwa na Benki ya Dunia, na wakamtumia mzee Mtei. Sababu unazijua.


Baada ya Mwalimu kutofautiana na Mtei na alipoona kweli alichomuambia ni kweli ,kwanza alimuheshimu ...[tofauti na kambona ambaye alitofautiana naye akamkashifu na kukimbia] Mtei baada ya ushauri kukataliwa alichukua pensheni yake akaenda kuanza kulima kahawa wilayani Meru kwenye shamba alilonunua la heka 100 ....akiongezea na pesa alizopata kwa kuuza nyumba yake masaki[citing from Gotherd to governor ] ....KILIMO cha kahawa kilianza kumuingizia pesa ..ambazo pia akanunua hisa kiwanda cha kusaga kahawa moshi..
Nadhani kwa kushauriwa Mwalimu aliona haingekuwa bora kwa mtei kubaki nchini ....hivyo alitumia infuluence yake akamtafutia kazi IMF ..ambako Mtei alipewa kazi ya kuwa Mkurugenzi [AFIRICA] IMF hadi alipostaafu rasmi ...1988 ..huko pia alipata kiinua mgongo kizuri na nafikiri hadi sasa analipwa pensheni huko......
Aliporudi rais Mwinyi , alimpatia kazi ya kuiunda upya mamlaka ya mapato TRA ...[REFER TUME YA EDWIN MTEI] ..ambayo ndio iliyokuja na mfumo wa TRA ya leo akitumia uzoefu aliopata IMF ..Zamani ilikuwa ikiitwa Customs .[idara ya forodha] na makusanyo yalikuwa ni kidogo sana ..na muundo ulikuwa kama wa kipolisi wa kukimbizana na walipa kodi ...mfumo mpya TRA ndio ulioleta ukusanyaji kodi kwa kutumia weledi na sheria .
 
Ni bahati mbaya kuwa historia ya mageuzi ya vyama vingi hapa nchini bado haijaandikwa, na pengine haitaandikwa. Waliostahili kuandika hawakuweza kufanya hivyo kiasi kuwa sasa wapotoshaji wanapata mwanya wa kupotosha. Chama kilichokuwa na nguvu ya wasomi na wananchi wa kawaida tangu kuanzishwa kwake hadi 1997 ni NCCR Mageuzi. Kwa wasiojua hata Katiba ya Chadema, Mzee Mtei alifanya copy and paste ya Katiba na lilokuwa andiko la sera la NCCR - Mageuzi na kisha kupata jina pamoja na Katiba ya chama chake. Historia ni ndefu. Kunako majaliwa tutaweza kuandika historia hii. Muda mfupi ujao nitawawekea kadi za awali za NCCR-Mageuzi zilizotengenezwa Harare, Zimbabwe mwaka 1992. Katika picha hiyo mtaona jina la Chadema lilikopakuliwa.

Kijana tulia tukupe historia kwa kuwepo na kwa kusoma ,nadhani historia ya nchi hii iandikwe upya ili watoto wetu wafundishwe kwa usahiihi kuanzia uhuru

NCCR - Hakikuwa chama cha siasa bali ulikuwa umoja tu wa kudai katiba kama ukawa ya leo , NATIONAL CONSTITUTION ,CONSTRUCTION AND REFORMS ...., Hapa unakutana na umoja wa vyama ambavyo vilikuwa vikidai katiba mpya na mfumo wa vyama vingi ......, kwakuwa PRINCE BAGENDA yupo hai ni bora aombwe aje hapa aeleze vizuri , lakini pia wako waandishi kama kina NDIMARA TEGAMBWAGE ...kuna vichwa humo ambavyo vingine vimefariki hata kabla ya kuona matunda ....,wako kina mzee DANSTAN CHIPAKA,KASANGA TUMBO ,CHRISTOPHERER MTIKILA ..CHIFU FUNDIKIRA , EDWIN MTEI ,mabere NYAUCHO MARANDO etc...
Baada ya vyama vingi kuruhusiwa kwa ushauri wa mwalimu nyerere kuitaka NEC wakubali .....basi hawa waazilishi wa hili kongamano la katiba walishindwa kufikia muafaaka wa kuunda chama kimoja ndio .....wakasajili vyama tofauti ..
UMD-fundikira
CCW [CUF incorporating KAMAHURU A chapter of NCCR znz ya kina shaaban MLOO] MAPALALA
CHADEMA - mtei and the clique
NCCR-MAGEUZI , Hiki kilikuwa chama kamili kwa kuongeza neno Mageuzi tu, na kikiasisiwa na vijana wasomi walikuwa na msimamo mkali ...., asili yake ikiwa UDASA[ university of dsm staff ass] hawa walikuwa ni wahadhiri vijana na wanafunzi wa chuo kikuu ndio walioanzisha hiki chama , pamoja na wanasheria machachari kama kina RINGO TENGA and the clique ....
DP - Christopher Mtikila

so sio kweli kuwa NCCR MAGEUZI Ndio walioanza bali NCCR ilikuwa hakikuwa chama bali ni kama baraza au kongamano ...na mkutano unaokumbukwa ulifanyika pale DIAMOND JUBILEE ndio uliozaa maazimio makuuu ya kupigania vyama vingi
 
Labda nikwambie kitu wachaga kuna tatizo mahali. Chadema ilivyoanza ilikuwa na nguvu kuliko NCCR wachaga wakajaa Chadema. aliyekuja kuidhoofisha chadema ni agustino lyatonga mrema mchaga mwenzao alipofukuzwa uwaziri akajiunga na upinzani aligoma kujiunga chadema akaenda NCCR mageuzi kule akapewa Kugombea uraisi wachaga wakalewa wakasema mchaga mwenzetu maarufu anagombea uraisi tukamuunge mkono wakaondoka chadema wakaenda NCCR mageuzi wakambwagia chadema mtei na mbowe wake wajijue. uchaguzi ulipokuja akashindwa na akahama chama kwenda TLP baada ya kufanyiziwa na akina marando aliowakuta. Wachaga waliomfuata wakaona waungame dhambi warudi kwa Mzee mtei walikotoka kwani zimwi likujualo halikuli likakwisha waliporudi chadema iliyokuwa imedorora ikapata nguvu tena .lakini kutoka mwanzo chadema ilikuwa na nguvu hasa Ya kipesa
Acha kuchochea ukabila chadema wewe Victor kimesera ni mmasai wa simanjiro huko unakuja kudangaya watu hapa. Huna aibu
 
Mzee Victor Kimesera,mwasisi wa CHADEMA ametegua kitendawili ambacho kimekuwa kikitumiwa sana na watoto wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Just see for yourself

Apongezwe kwa kuwaachia servant quarter wanachama hai wa CDM.
 
Kasema ukweli chadema inahitaji ofisi inayoendana na hadhi yake,ikiwezekana upitishwe mchango nchi nzima tuchangie kama watanzania walivyoichangia ccm enzi hizo,kile kibanda hakifanani kabisa na chopa tunazoruka nazo hewani
 
tatizo hata hilo Banda CCM hamna.Majengo yote ya CCM mlikwapua toka serikalini.
Mkuu nakushukuru kwa jibu mujarab, hakuna ata mali moja ccm wanaoweza kusema hii niya kwetu, asilimia kubwa ya mali zao walizipata enzi za chama kimoja au kwa figisu figisu za baadae ya mfumo wa vyama vingi kuingia.
 
Back
Top Bottom