moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,900
- 4,865
Ninarudia kusoma Kitabu Cha Mzee Ludovick Utouh ili kuona kama kumewahi tokea ukinzani wa CAG na Bunge huko nyuma na Viongozi walichukua hatua gani. Nakutana na kisa Cha Jairo kuanzia Ukurasa wa 77 mpaka 80. Mzee Utouh anaandika “ .... Rais Jakaya Kikwete alieleza wazi Kwamba si Bunge wala Serikali zenye uwezo wa kumwadhibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, bali ni mahakama pekee tena kwa utaratibu ulioanishwa kikatiba....”
Kabla ya hapo Mzee Utouh anaandika “ ... Hili ni mojawapo ya mambo yaliyonitesa sana kwenye Uongozi wangu. Baadhi ya Wabunge walionesha kupoteza imani nami....”
Hii sio mara ya kwanza Bunge kujaribu kutomasa Katiba. Lakini wakati wa Mzee Utouh Viongozi wakubwa kama Rais waliingilia kati na kusema waziwazi BUNGE HALINA MAMLAKA NA CAG. Sasa hivi inawezekana Viongozi wakubwa Ndio wapishi wa mgogoro huu ambao hauna maana kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app